Serikali futeni utaratibu wa kudai maiti Hospitali za Serikali

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,542
Salaam, Shalom!

Tamaduni zetu za kiafrika, huwa hatuna utaratibu wa kudai maiti. Mtu akishaaga Dunia huwa tunasamehe.

Bwana bwana, juzi tena TABIA hii isiyofaa imeibuka tena mkutanoni Furahisha Mwanza katika ziara ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCCM,

Kada mmoja wa chama tawala akanyosha mkono kuuliza swali, Mwenezi wa CCM ambaye ni Kijana wa Kanda ya ziwa Kutokea Kijiji Cha Kolomije Misungwi, akampa nafasi Kutoa dukuduku lake, kada huyo akasema yafuatayo.

Ombi/Swali: "Tumepata misiba miwili ya wanachama wa chama chetu, tunadaiwa Tsh. 2,100,000/= Hospitali ya Sekeu Toure Mwanza, ili kutoa miili hiyo hospitalini, tunakuomba utusaidie ili tukazike".

Mwenezi akijua kuwa, ni aibu maiti kudaiwa, akapiga chenga kama ifuatavyo;

Jibu: "Naagiza mpewe ambulance ili mwende mkazike, na ikiwa ambulance haipo, chukueni gari yangu mkazikie".

Pamoja na chenga za kisiasa ulizopiga ndugu Mwenezi, bado tatizo liko pale pale. Najua off kamera, ulitoa pesa hiyo 2,100,000/= Kutoka mfuko wa chama.

Haiwezekani ndugu wauguze mgonjwa, inatokea bahati mbaya, mgonjwa anaaga Dunia halafu Hospitali ya Serikali igome kutoa mwili kwa maziko hadi ndugu watoe pesa zote.

Serikali ni yetu sote walipa Kodi, futeni hii adha kwa wananchi maskini. Serikali ilipe gharama hizi jamani.

Chonde chonde tafadhali, maiti isidaiwe!

Karibuni🙏
 
Mi nadhani ni utaratibu mzuri kulipia gharama za matibabu. Hiyo maiti inaweza kuwa na mali pia ina ndugu.

Msamaha utolewe kwa vigezo maalum. Wabongo tuache kupenda mserereko eti kisa mtu kafa gharama ndo basi. Mbona marehemu akiwa na madeni mtaani familia inalipa. Pia marehemu hulipwa madeni yake ikiwa anawadai watu wengine.
 
Mi nadhani ni utaratibu mzuri kulipia gharama za matibabu. Hiyo maiti inaweza kuwa na mali pia ina ndugu.

Msamaha utolewe kwa vigezo maalum. Wabongo tuache kupenda mserereko eti kisa mtu kafa gharama ndo basi. Mbona marehemu akiwa na madeni mtaani familia inalipa. Pia marehemu hulipwa madeni yake ikiwa anawadai watu wengine....
Kwamba unamaanisha maiti alikuwa bahiri?

Kwamba alikuwa na Mali akaona ni HASARA Mali zake kuuzwa Ili atibiwe, akaona Bora afe?

Hivi ujasiri huu wa kutojali ubinaadam mnautoa wapi?
 
Mi nadhani ni utaratibu mzuri kulipia gharama za matibabu. Hiyo maiti inaweza kuwa na mali pia ina ndugu.

Msamaha utolewe kwa vigezo maalum. Wabongo tuache kupenda mserereko eti kisa mtu kafa gharama ndo basi. Mbona marehemu akiwa na madeni mtaani familia inalipa. Pia marehemu hulipwa madeni yake ikiwa anawadai watu wengine.
Wabongo wanataka kila kitu kiwe bure,
Elimu bure
Afya bure
Maji bure
Umeme Bure 🤣🤣

Kikubwa kama jamii tuhimizane kukata bima ya Afya
 
Wabongo wanataka kila kitu kiwe bure,
Elimu bure
Afya bure
Maji bure
Umeme Bure 🤣🤣

Kikubwa kama jamii tuhimizane kukata bima ya Afya
Uwe na adabu,

Wananchi ndio waajiri wa Serikali yote, wanalipa mishahara na matumizi yote ya Serikali kupitia Kodi na TOZO mbalimbali.

Kodi za wananchi ndizo zimejenga hospitali.

Hivyo Mwananchi akiomba apunguziwe gharama wakati wa shida ni HAKI yake.
 
Sina HAKIKA kama mabenki yana Utaratibu ya kudai maiti ikitokea mdaiwa amefariki na alikuwa anadaiwa.

Serikali iache TABIA hii ya kudai maiti Ibebe Mzigo huo.
 
Back
Top Bottom