Maiti tisa za mauaji yaliyofanywa na polisi leo Mbeya ziko mochwari

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,856
Watu tisa waliouawa leo wako kwenye mochwari ya Rufaa.
Polisi mpaka muda huu wamekaa kimya wakati ni wao waliowaua kwa risasi. Nimezipiga maiti hizo picha kwa camera ya simu ndo maana sijaziatach, kesho zitakuwa hewani
 
Jitahidi leo leo mkuu picha hizo tafadhali, vp hali ikoje usiku huu lkn? vituo vya polisi vingapi vimechomwa moto?
 
TBC wamenishangaza sana kwenye taarifa yao ya habari(redio), badala ya kutuambia kilichojiri na maafa yaliyotokea, wanatanga maazimio ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mbeya. Aibu tupu.
 
Halafu naona kama vyombo vingi vya habari havikutoa hii habari kwa kina zaidi cjui tatizo nini yani hata bbcswahili nao kimya kabisa....
 
He! hivi nchi hii tumefikia kiwango cha kuuana kama wanyama. Tafadhali tuoneshe picha hizo
 
Sijaelewa ni kwa vipi TBC1 wamefikia uamuzi wa kuoneshwa wachina wanatembelea makuburi ya ndugu zao lakini wasioneshe matukio ya Mbeya! It does not matter machafuko ya Mbeya yamesababishwa na nini au nani ana makosa lakini inakuwaje chombo cha umma kama TBC1 waipige hii habari blanket na kujikita kwenye matembezi ya wachina? Kwamba ccm sasa hivi could not care less kuhusu uhai wa watanzania kwao wachina come first?
2015 watasomba wachina wawapigie kura maana polisi watakuwa wameshaua watanzania wote!
 
yaleyale unatumia nguvu kupita kiasi mwishowe wananchi wanalipa kisasi sijui tunaenda wapi?
 
Hali bado ni tete hivi sasa magari yanapita barabarani kutangaza hali ya hatari na wanawaomba wananchi waingie majumbani mwao.
 
Hali bado ni tete hivi sasa magari yanapita barabarani kutangaza hali ya hatari na wanawaomba wananchi waingie majumbani mwao.
 
Back
Top Bottom