Maisha yangu nimeyaharibu mwenyewe

Maisha yangu nimeyaharibu mwenyewe

SEHEMU YA TATU (3)
Iliyopita….
Wakati huo kaka angu alikua form 3 na mimi nilikua form 1. Baada ya kurudi mwanza ilibidi nirudi ile shule ya kata niliyochaguliwa kwani hakukua na mtu wa kulipa ada kule private coz tumekataa kusoma Bukoba. Kaka yangu yeye ilibidi amalize pale pale

Tuendelee sasa

Maisha yaliendea na changamoto zilikua nyingi kwani Kaka yangu alikua busy sana na shule, ilikua shule ya kutwa ila walikuwa na itaratibu wa kulala shule wakijisomea hivyo alikua akionekana nyumbani kwa nadra.

Kwa upande wangu maisha ya shule ya kata yaliendelea na nilifurahia maisha yale sababu wengi wao tulisoma pamoja primary hivyo nilikua nafahamiana nao vizuri.

Tatizo lilianza pale ambapo nilianza kuwa kijana wa mtaani maana sikua na msimamizi wa kunisistiza kusoma. Kama nilivyosema hapo awali mimi nilikua slow leaner sababu ya kupenda michezo mpira ukiwa namba moja.
Ilikia nikisikia kuna disco basi lazima twende na wenzangu hata kama hatuna hela. Ila nilikua naenda mchana tu, mambo ya usiku sikuwa nimezoea.

Mzee alikua akisafiri tunabaki na mama mdogo pale home na akirudi basi ni mimi na mzee full kupishana ndani.

Asubuhi kabla sijaenda shule nilikua lazima nioshe vyombo vya jana usiku then mzee wangu yeye ni mtu wa usafi sana so atafagia nyumba na kuweka safi ndo aende kazini. Yes yalikua maisha ya namna hiyo.
Shule niliyokua nasoma ilikua kama umbali wa 2.5KM hivi from home na nilikua nachelewa sana shule maana hakuna daladala za kwenda kule pia kazi za home asubuhi zilinichelewesha. Jioni nilikua narudi napika msosi then ndo mambo mengine yataendelea. Mzee alikua mtu wa kuchelewa kurudi.

Nilipambana na maisha ya shule na changamoto za ujana kwani balehe yangu ndo ilikua inaanza. Kaka yangu kwa wakati huo alikua form 4 so hakua anaonekana nyumbani ni yeye na shule. Dogo alikua kaanza form 1 tayari na yeye alipelekwa Bukoba (shule sitoitaja) ila alikua boarding

Nilijikuta home nimebaki mimi na mzee tu na nilikua form 2 wakati huo.
Niliendelea na masomo kwa challenge kidogo siwezi laumu maana sikuteseka kiivyo, niliwahi rudishwa home sababu ya pesa ya dawati.

Wakati huo nilikua najifunza vitu vingi vya huko ikiwemo kuogelea, nimetoroka sana home tunaenda kuogelea ziwani.
Sikuwa mlevi wala mvutaji. Sikuwa hata namjua mwanamke kipindi hicho.

Matokeo ya form 2 yalitoka na nilikua na wastani wa 48% wakati kaka yangu alipata wastani 76% alipokua form 2 so hapo ndo mzee alimind sana na kumpigia aunt simu kuwa nimekua muhuni na sisomi.
Aunt aliongea na mimi kupitia simu ya mzee na nikamwelezea stuation yote, kidogo alielewa. Akasema ntahamishwa shule na sikua na pingamizi wakati huo.

Kabla ya matokeo yangu ya form 2… Kaka yangu alikua kashaondoka home kwani alifaulu kwenda advance kwa 1 ya 13 na alichaguliwa Tabora Boys.

Niliingia form 3 nikiwa mchepuo wa Science kwani kwenye hiyo shule ya Kata sikua kati ya waliofail… Yani Science walichukua wenye wastani kuanzia 40% hivyo nilikua miongoni mwa wanafunzi 48 wa Science na hiyo ilinipa faraja nikajiona kama sikufail hivi..

Mwezi wa 2 mwaka 2009 ndo nilihamishwa kutoka Mwanza kwenda Bukoba na taratibu zote alifanya mzee kwa kushirikiana na Aunt yangu. Nilipata shule ya kutwa ntaitaja tu (BUKOBA SEC) hivyo nilikua nikikaa kwa aunt yangu wa Bukoba. (Nna aunt Bukoba na Dar) ntakuja kusimulia mbele huko.

Maisha mapya ndani ya BUKOBA SEC yalianza huku nikiwa chini ya uangalizi mkubwa wa Aunt.. Kwakweli alininyoosha kwa wema lakini.
Sasa wakati naenda kuanza pale Bukoba Sec walikataa kunipokea kama mwanafunzi wa science sababu ya matokeo yangu ya form 2… Kwakweli nilijisikia vibaya sana na nikaona ndoto zangu zote zimekufa. Niliambiwa kama ntafanya vizuri mtihani wa midterm hasa somo la hesabu basi ntaenda science. Aunt alinipa moyo na wakati huo nilikua busy sana na tuition pamoja na shule.
Wakati nahamia pale kulikua na wanafunzi wengine wawili wamehamia pale na mmoja tulikua na case inafanana (ya kuwekwa arts badala ya science) yule jamaa nakumbuka kauli yake hadi leo, aliniambia “Kila kitu kinatokea kwa sababu tukaze tu humu humu arts”
Lile darasa tulilowekwa lilikua la watukutu haswaaa si unajua mambo ya Arts. Yani miaka miwili nyuma lilikua linatoa mwanafunzi mmoja au wawili tu waliofaulu hivyo hata waalimu hawakua wanakuja kufundisha sana mle. Kwa waliosoma BK Sec wanajua vizuri miaka ile ukiwekwa form 3 B basi wewe ni mtukutu wa Arts .
Sasa ile mindset kwamba darasa hili ni watu wa kufeli ilikua inanitafuna sana ila rafiki angu (Tumuite V) alinipa sana moyo akasema tunaenda kubadili Historia ya darasa hili.

Wakati naanza pale BK SEC kuna mtoto wa aunt yangu alisoma hapo na ndo alikua amegraduate ila hakufaulu na yeye alikua Darasa lile lile la form 3 B. (Watoto wa aunt karibia wote wamesoma BK SEC so kama ntamtaja mwingine mbeleni msisahau)
Sasa huyu Dada yangu aliniunganisha na dada flani jirani yetu ambaye alikua anasoma pale BK SEC na alikua form3 B.

Nakumbuka ilikua majira ya saa moja jioni alinipeleka kwao na kunitambulish kuw mimi ni mdogo wake hivyo anisaidie notice angalau niandike maana wenzangu walikua washasoma soma topic kadhaa.
Asee yule dada alivyotoka nje nilibaki nimeduwaa sana, alikua ni mzuri mnoooo (mweupe na mrefu kiasi, alikua mtu wa Singida) huyu tumwite Jane.

Jane alinipokea fresh na akanipa ABC za pale shuleni na akaniazima madaftari nikaandike notice. Jane ndo alikua rafiki yangu wa kwanza BK sec.

Maisha yaluendelea shuleni na hadi kipindi hicho sikuwa namjua mwanamke kabisaaa ila ukaribu wangu na Jane ulinipa shida sana shuleni. Washikaji walikua wananidiss sana sababu tu niko close na Jane na si a hata mwezi shuleni.
Mazoea na Jane yakafanya akawa ananipitia home ndo tunaenda shule (Kwao ni mbele ya kwetu kama mwendo wa dak 5) ila Jane alikua anarudi nyuma yaani anakuja kwetu then ananipitia ndo tunaenda shuleni.

Wanafunzi wa science mara nyingi walikua wanakuja kwetu form 3 B kupiga story muda ambao hawana vipindi na wengi walikua wanafata wadada pia. Si mnajua Arts walikua wanakua warembo sana. Sasa wale jamaa wa Science walianza kuniulizia maana washasikia niko close na Jane wakati wao kila wakijaribu Jane anawakaushia.

Nakumbuka siku moja jioni nikiwa natoka tuition, nilipita kwa Jane kumsalimia then akanisindikiza, tulifika mahali kuna shamba flani la miwa na story zilikua nyingi. Tulijikuta tunakiss na Jane na sikusema chochote na yeye alinambia byee huyo akaondoka kurudi kwao.

(Asee Jane alikua mzuri na wakati huo nilikua sijui kitu kuhusu mapenzi, kuna muda nilikua nikitembea nae najikuta Nasimamisha tu)

Baada kama ya wiki 2 mimi na Jane tulikua wapenzi na kwakweli namkumbuka hadi leo maana ndo mwanamke wangu wa kwanza ( Ntasimulia mbeleni huko)

Turudi shuleni sasa, midterm ilifika na tulifanya pepa na kwakweli nifanya vibaya. Jumla wanafunzi tulikua 240+ , sasa matokeo wanapanga haijalishi uko mchepuo gani kikubwa ni Average… Nakumbuka nilikua mtu wa 92 kati ya 240+.
Asee aunt alimind sana akasema mwanza nilikua nacheza tu na kwakweli alinikazia zaidi.

Yale matokeo yakafifisha ndoto zangu za kwenda Science jumla…

TUTAENDELEA
 
SEHEMU YA NNE (4)

Tulipoishia…

Yale matokeo yakafifisha ndoto zangu za kwenda Science jumla…

Tuendelee Sasa…

Familia ya pale home kwa aunt ilikua poa tu maana hakukua na challenge sana na nisingependa kugusia part hii maana sio muhimu sana.

Baada ya matokeo yale ratiba ilibadilika, ilikua hata nikitoka tuition lazima home nisome usiku, uncle (mume wa aunt) alikua lazima aje usiku kuchungulia room kwetu kama tumeamka kusoma (Kuna mtoto wa mwisho wa aunt mwingine alikua pale ma alikua primary bado ndo tulikua tunapeana kampani kusoma)

Kwa upande mwingine maisha ya kiroho pia yalikua yanakaziwa pale, kila jumapili lazima kwenda kanisani, ilikua ni lazima so nilinyooka na kuwa kijana mzuri tu, sikua na makundi kama Mwanza kule.

Turudi kwa Jane kwanza… Wakati wote ambao niko kwenye mahusiano na Jane sikua nimewahi kufanya chochote. Kuna siku tulipanga kwamba weekend twende mlimani huko ( kulikua na mlima flani una majani na miti miti na hakukuwa na nyumba karibu na maeneo yale) ukipanda huko juu unaiona Bukoba vizuri kabisaaa, mlima uko maeneo ya Buyekera karibu na shule ya msingi Buyekera. Kwa watu walioishi Bukoba mjini wanapafahamu ingawa kwa sasa mlima huo una nyumba kibao tu.
Tuliplan twende kule tukashiriki tendo wakati huo mimi ndo mara ya kwanza na mwenzangu yeye alikua ashapiga show kadhaa huko nyuma.
Maisha yaliendelea na weekend ilifika tukaenda zetu juu huko mi nilibeba maji ya kunywa tu. Tulikutana mahali na tukaanza safari.
Baafa ya muda kama 20 min tulikua kule juu tukajichimbia mahali ma story ziliendelea huku nisijue naanzia wapi.
Kufupisha, tulishiriki tendo na ndo ilikua mara yangu ya kwanza. Siwezi sema nilienjoy sana maana sikua najua mambo mengi na niliishia bao la kwanza wala sikutaka kuendelea.

Sasa baada ya yote Jane alizidi kunipenda na mimi nilikua nampenda sana kwakweli. Kule shuleni walikua wanasema tu mi napata story ila hatukuwahi kuweka wazi mapenzi yetu mbele za watu. Baadhi ya washikaji walikua na chuki na mimi kisa Jane. Jane alikua na mwili mkubwa kidogo kunizidi na alionekana kunizidi kama mwaka hivi (nilijua baadae kuwa ananizidi)
Sasa wakati penzi likikolea Jane alikua na Kaka yake ambaye nilikua tu namwona na kwa kipindi kile jamaa alikua anakula moshi (anavuta Bangi) yule Kaka yake sikuwahi kuwa karibu nae ila nilikua najua anamtaka mtoto wa aunt yule aliyefanya nijuane na Jane.
Siku natoka tuition mida ya saa 12 jioni nilikutana na kaka yake akiwa na kundi lake na wanilisimamisha nilikua naendesha baiskeli kwenda home. Jamaa alinipiga beat na kusema natoka na dada yake, atanitafuta, pale asingeweza kufanya kitu kwani tulikua road.
Asee niliogopa sana nikaenda home straight kwa Dada (yule mtoto wa aunt tumwite Tiva)
Tiva alimind sana akanambia twende, kufika kule alimfokea sana jamaa na jamaa akasema hajasema kitu kibaya kwangu na hawezi kunigusa maana sijamkosea kitu.

Kun siku tuko shuleni, muda wa break Jane alikua ananifata kwenye dawati langu na kuongozana hadi jikoni kupata chai (BUKOBA SEC ilikua na utaratibu wa kugawa maandazi na chai kwa kila mwanafunzi na ilikua buree, utaratibu uliwekwa kwa members yaani wanafunzi mnakua na makundi ya watu 12 na kiongozi ndo anafata maandazi na chai then anawagawia)
Sasa huu utaratibu sikua nimeuzoea sababu kule Mwanza hamna mambo hayo, pili sikua nimezoea sana kuongea na watu, tatu kulikua na vurugu flani hivi. Jane ndo mtu pakee alikua ananichukulia maandazi na kuniletea kwenye Table yetu pale canteen then tunakula. Siku nyingine nilikua siendi kabisa Canteen. Sasa kuna siku nilimwambia siendi yeye akatangulia then baadae akili ikanambia niende nikanunue Karanga za bubu (zilikua maarufu sana na muuzaji alikua bubu). Wakati nanunua karanga nikamwona Jane yuko Posta (Bukoba sec iko karibu na ofisi za posta) anaongea na jamaa hivi ambaye sio mwanafunzi. Wivu ukanijaa na nikachukia sana na aliniona.
Nikarudi class na sikusema kitu, jioni muda wa kutoka akaja kunichua kwa desk yangu tuindoke nikamwambia asinifate tena na asinizoee, nilikua na ujinga mwingi asee.

Jane aliondoka hakutaka kudraw atention yoyote pale maana wengi walikua hawajui kama tunadate.
Jioni alikuja home kuniulizia na akaambiwa niko Tuition. Home hawakua na wasiwasi wanajua tunasoma wote. Usiku akaja tena na nikamkazia nikasema sitaki mahusiano tena. Aliniomba msamaha na kunidanganya yakaisha.
Nakumbuka Jane alikua akiniletea pesa na vijizawadi sana.

Sasa kumbe sakata la yule kaka yake Jane kusema atanitafuta lilikua limetengenezwa na jamaa flani alikua anamtaka sana Jane ila Jane anakaza, jamaa aligundua Jane ana mahusiano na mimi.

Nakumbuka hiyo siku nikua natoka tuition, mida ya saa moja jioni giza tayari limeingia, nikiwa njiani kabisa kufika home, ile sehemu yenye shamba la miwa ambako nilikiss mara ya kwanza na jane. Nilikutana na jamaa wawili wakanisimamisha, wakati nashuka kwenye baiskeli niwasikilize asee nilipigwa ngumi moja ya uso hadi chini… Sikujua napambana nao vipi nikajikuta nimebaki chini pale kama nimezima ili wasiendelee maana wangenipasua.. Jamaa wakakimbia (mmoja alikua yule anayemtaka Jane na nilikua namjua sababu Jane aliwahi nionyesha)

Walivyokimbia nikaamka nduki nikaenda nyumbani na nilikua na uoga sana ikabidi nimwambie Aunt kuwa watu flani wamenivamia na kunipiga kisa Jane (nilikua na utoto mwingi). Aunt alichukia na akasema twende kwao Jane ila tupite kwa balozi kwanza kutoa taarifa then tukaenda kwao na Jane

Itaendelea…
 
Waiting for part 5🌝
 
SEHEMU YA TANO (5)

Tulipoishia….

Walivyokimbia nikaamka nduki nikaenda nyumbani na nilikua na uoga sana ikabidi nimwambie Aunt kuwa watu flani wamenivamia na kunipiga kisa Jane (nilikua na utoto mwingi). Aunt alichukia na akasema twende kwao Jane ila tupite kwa balozi kwanza kutoa taarifa then tukaenda kwao na Jane.

Tunaendelea….

Kwao na Jane tulimkuta mama yake na wanafahamiana vizuri na aunt.. Sasa aunt sijui hakunielewa au alikua ashasikia tetesi za mahusiano kati yangu ma Jane..

Aunt akasema nisimulie ilivyokua na mimi nikasema kama nilivyomwambia home, asee aunt akaongeza na maneno mengine ikaonekana Jane ndo ana makosa. Mama yake alimpiga sana mbele yangu huku akitamka “Nishakuzuia mambo ya wanaume” mimi na Aunt tuliondoka tukuacha Jane anapurukushana na mama yake.
Tumerudi home napo nilipata nasaha ndefu sana siku hiyo.
Sasa kesho shule mimi na Jane tukawa maadui. Asee Jane alifanya maisha yangu ya darasani yakawa magumu sana. Kuna siku nilikutana nae mtaani akanambia atanionyesha. Sasa wale jamaa wote waliokua wakimfatilia akaanza kupiga nao story. Nilikua naumia sana maana nilikua nampenda bado ila sikuweza kumfuata hata siku moja kumwambia yaishe au samahani, hivyo ni miongoni mwa kitu kilichomchukiza sana ( nilijua baadae). Maisha ya shule yaliendelea na niliamua kufocus na masomo zaidi na wakati huu mwezi wa sita ulikua umefika na tulifanya mtihani vizuri. Matokeo yalitoka na this time nilikua mtu wa 9 kutoka 92 mwezi wa 3. Licha ya matokeo haya Aunt bado alisema ongeza bidii kuna masomo hufanyi vizuri. Dah nilijisemea huyu mama anataka nisome vipi.
Yule rafiki yangu V tuliyehamia wakati mmoja hapo alikua close na mimi na ndoto yetu ya science ilishakufa muda tushakua watu wa Arts na tushazoea mazingira. Ilibidi nimwambie kuhusu Jane na akasema alisikia maneno kuwa nimepigwa na mchumba wa Jane, akanicheka sana. Kumbe story watu wanazo class na wananicheka chini chini.
V aliniahidi ataongea na Jane maana nilikua nammiss sana zile care amd everthing alafu ulizingatia ndo nilikua nimeonja utamu wa tunda mara moja tu.

V alizungumza na Jane lakini Jane alinikazia kabisaaa na wakati huu nilijua mambo mengi kuhusu yeye. Kumbe zile pesa Likua akinipa alizitoa kwa jamaa mmoja alikua anadate nae. Jamaa ni mkazi wa Bukoba ila alikua anafanya kazi Dar. So Jane alinunua simu flani hivi (Kipindi hicho simu za mchina zilikua zinatrend sana Bukoba) mimi sikua hata na simu, nilikua natumia ya sisy Tiva kuwasiliana.
Kwenye desk langu pale class nilikua close na wadada flani na mmoja nakumbuka alikua akinionyesha sign za kunipenda hata wakati niko na Jane. Sasa huyu na wenzake ndo walikua wakinipa umbea namna Jane anaongea huko, anadate na nani na mengineyo.

Maisha yaliendelea japo niliteseka sana na Jane hadi tukaingia form 4…….

Tulifanya mtihani wa Mock miezi miwili kabla ya NECTA na kiukweli matokeo ya Mock nilifeli… Nilipata 4 ya 29. Yule rafiki yangu V alipata 4 ya 28 na rafiki yetu mwingine alipata 4 ya 28.

Matokeo haya hayakumfurahisha kabisa aunt na alitoa kauli ya kunikatia tamaa akasema nijitahidi NECTA nipate hata 4 ya 28 nikasome Ualimu.
Dah nilikua mnyonge sana na sikuelewa hatma ya masomk yangu. Tulikaa kikao mkakati na wale rafiki zangu wawili tukakubaliana kwa muda huo mchache uliobaki tukakae Gheto tuwe tunakesha.
V alikua na gheto aliachiwa na dada yake pale mjini ila halikua na umeme.

Niliwasilisha ombi langu kwa Aunt, na hakukubali moja kwa moja akasema nikamwambie uncle. Baadae nilikubaliwa na mapambano yakaanza.
Nakumbuka ilikua imebaki mwezi na siku kadhaa tufanye NECTA, tulipiga book haswaaa, tulikua tunalala kwenye mkeka. Tuliweka sheria kulala kitandani ni kuanzia saa 10 usiku. Kwakweli nilipigika sana na rafiki zangi wale. Tulichambua past papers, tulifanya Duscussion na mengineyo mengi.
Nilikua naenda home jumatano na ijumaa kubeba misosi. Jumamosi jioni nilikua narudi kulala home ili j2 niende kanisani.

Siku zikakatika hatimaye tukafanya NECTA, mimi nikiwa kwenye bifu zito na Jane ila sikujali tena nilikua nawaza future yangu tu.
Jane hakua vizuri sana class so hakujali matokeo wala nini.

Baada ya kumaliza NECTA nilirudi mtaani na nikaendelea kumsaidia aunt pale ofisini kwake. Alikua akiniamini sana na wakati mwingine akisafiri mimi ndo nashinda ofisini kwake na natunza pesa zote home hadi arudi.

Nilianza kumshinikiza nirudi mwanza lakini hakukubali na Mwanza nilikua na crush wangu wa tangu utotoni sasa nilikua nammiss sana na kila tukiongea kwenye simu alikua anauliza narudi lini
Marafiki pia walikua wakiuliza narudi lini. Wakati huu nilikua na kisimu cha tochi tayari ambacho alinitumia kaka yangu akiwa kule Tabora Boys.

Matokeo ya Necta yaliyoka na siku hiyo nilikua nyumbani, nilipokea simu za watu kadhaa wakisema matokeo yametoka. Sikuwa na uwezo wa kwenda internet Cafe maana nilipatwa na wasiwasi hadi tumbo likaanza kuuma. Nakumbuka nilienda toilet nikamaliza matatizo yangu nikarudi kitandani kulala nikaweka biblia kifuani.

Baada kama ya saa hivi Aunt alinipigia na nilikua naogopa sana kupokea ile simu. Niwarudishe nyuma kidogo, nilisema watoto wengi wa Aunt wamesoma BK SEC, Sasa aunt ana mtoto wa kiume alikua UDSM wakati huo na alisoma BK SEC O-level.
Kipindi hicho matokeo walikua wanaandika majina kama sikosei (mtanirekebisha kama nimekosea) . So yule mtoto wa aunt alikua anajua namba ya shule ya BK SEC, nakumbuka ilikua S.0307/….. ndo namba ya mwanafunzi inafuata.
Nilipokea simu ya aunt na alikua akinipa taarifa za matokeo yangu.

Tunaendelea….

Kama watu wako active nishushe epsode nyingine…
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom