Maisha yangu na JamiiForums

dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,822
3,650
Baada ya kumaliza kidato cha nne nilibahatika kumiliki smartphone yangu ya Kwanza. Nilikuwa so excited kujua Jamiiforums inafananaje hii ilitokana na baba yangu kuwa msomaji Sana wa magazeti ya Raia Mwema na Mwanahalisi na mara nyingi wachambuzi wa magazeti hayo walikuwa wanafanya reference zao kutoka Jamiiforums.

Akina Jenerali Ulimwengu, Chahali, Nyaronyo Kicheere, Padri Privatus Karugendo na waandishi wengine kuitumia Jamiiforums Kwa reference ilinifanya niamini Jamiiforums wapo vipanga tupu! (Hii ni kweli kulingana na jukwaa husika, kila jukwaa lina magwiji wake)

Kitu kingine kilichofanya niwe na hamu na Jamiiforums ni sister wangu. Yeye alikuwa member kindakindaki wa Jamiiforums. Kila nilipoenda kwake alikuwa akiitaja taja Sana Jamiiforums! Sasa najua alikuwa addicted nayo bila kujijua ingawa kwa sasa huwa anaingia mara chache Sana!

Nikawa msomaji tu, sister alipogundua napenda JF akaniunganisha rasmi. Taratibua nikaanza kuizoea Jamiiforums, nikawajua manguli akina Kiranga, Mentor, Mshana, Lala 1, Watu 8, Mzizi Mkavu, Nguruvi, Faizafox, na wengine kibao wenye uwezo katika kujenga hoja na kuisimamia iwe sahihi au sio sahihi.

Nakumbuka comment yangu ya Kwanza tu nilishambuliwa Sana! Niliitwa mbulumundu, eti natumia makalio kufikiri! Niliambiwa maneno makali halafu kwa hoja zilizosimama yaani ile mtu unatukanwa ila ukisoma hoja unasema mmh huenda kweli! Ilikuwa siku chungu ila haikunifanya niachane nayo!

Haikuchukua muda nami kuwa addicted kabisa, nisipoingia Jamiiforums nahisi Kama naumwa! Kila mia tano ninayopata nawaza kifurushi tu!

Kukutana na hoja za watu wa Jamiiforums ikanifanya nianze kuwaona watu wa huku mtaani wajinga, hawajielewi! Hawana akili. Nikaanza kutofautiana nao kimitazamo! Uongo dhambi Nilikuwa na uelewa wa Mambo mengi kuliko wao! Nilikuwa updated Sana kuhusu siasa, teknolojia, mahusiano, entertainment, nilikuwa vizuri! Ila tu sikuwa mvumilivu na ujinga wa watu, niliwafokea kwa hoja kuntu na sikujali Wana feel vipi as long as ninaongea point na nimewazidi hoja nawaondoa ujinga Basi liwalo na liwe, I don't care!!! Kama nilivyofanyiwa JF nami niliwafanyia wao!

Nikaenda advance, aisee huko ndio balaa! Jamiiforums ilinijengea kujiamini Sana! Nilikuwa vizuri darasani! Ila kitu kikubwa Jamiiforums ilinijengea ni uvumilivu pindi ninapofanya argument na mtu! Sijisikii vibaya mtu akinizidi hoja, nakubali kushindwa ila wenzangu hawana uvumilivu wanasusa na wakiniona wanaamua kutochangia kitu! Ilifikia muda natangaza darasani mtu yeyote aanzishe maada yoyote achague upande anaoumudu halafu tupambane kwa hoja!

Nilikuwa najua nisiposhinda kwa hoja Basi nitamshinda kwa kumkera Hadi asuse! Nilikuwa nina yale majibu sio matusi ila mtu hawezi kuvumilia! Yote hayo nimefundishwa Jamiiforums. Yaani nikicharuka siku hiyo nasema Mungu hayupo! Hapo nitashuka na hoja za Kiranga watu wanakaa mbali futi 100. Siku nyingine nasema Mungu yupo halafu nashuka na hoja za Eiyer! Watu wananiona Kama Socrates wa karne hii! Uchawi nauzungumzia kwa vifungu vya Mshana! Jamaa wakaanza kuniita philosopher, jina nikalipenda nikalichukua!

Kufika chuo niliendelea na undava wangu! Undisputed. Hakuna siku nitakosa cha kuchangia darasani nilikuwa najiamini tu! Nikapata girlfriend ila siku zote Jamiiforums ilikuwa imenifundisha "Don't put feelings in front of common Sense" hii Imani iliathiri Sana mahusiano yangu! Sikudumu na yule dada tukaachana kwa kiburi changu na ujuaji! Sijali mapenzi, nataka mpenzi wangu awe na akili. Niliamini ninachowaza Mimi ndio chenye akili ukienda tofauti Basi uje na hoja nzito na uwe mvumilivu wa kuitwa Mbulumundu! Vinginevyo achana na Mimi!

Wakaja wengine Hali ikawa the same mapenzi si muhimu kivile nawekeza zaidi kwenye ufilosofa wangu!

Nilikuja kumpata rafiki anaitwa Anna! Anna nahisi alijua shida yangu, akawa ananiambia nimekuwa Kama sanamu au mashine. Sina hisia! Akawa anasema Mimi ni mfu ninayetembea, mbinafsi, najijali Mimi tu! Alinielekeza mengi Sana! Akawa ananichukua ananipeleka kanisani kwao tukajadili kuhusu Mungu na uwepo wake!

Anna alinifanya nitazame maisha katika angle nyingine! Nikajifunza kuheshimu tofauti baina zetu wanadamu na kuziheshimu pia! Nikajifunza kujishusha, kujali hisia za watu! Kuacha ujuaji! Nikaanza kujenga urafiki na watu! Nikawa msikivu, hata kwenye mijadala nikawa situmii kauli ngumu! Hadi leo hii najali Sana hisia za watu natafuta namna Bora ya kukabiliana nao bila kuwafanya wajisikie vibaya! Maisha mafupi haya nahitaji kuwa na ustawi mzuri na watu.

Jamiiforums imenifundisha mengi sana! Imenitoa ujinga, imenifunza umakini, kufikiri, kusoma ili kuelewa, utulivu! Nawashukuru wote kwa kiasi kikubwa mmefanya niwe Mimi!

Hadi Sasa nina miaka zaidi ya sita Jamiiforums, nimeikumbuka safari yangu hapa nikatamani kushea nanyi!

Mungu awabariki
 
Tumpe nini Anna wa watu kwa kukomboa sanamu la watu..😅

Jf kwangu nilikuta naijua tu!.. ilikuwa nikisearch Google kitu fulani naona wananidirect huku jf.. mwishowe nikanogewa nikajiunga nikawa member nilianza kama mpole ila sahivi sasa..😎

Jf ni kisima Cha maarifa na ujinga pia na jokes hizo zote ni sifa tulizonazo wanadam,so ni vile tu utaamua uchote kipi uache kipi..
 
Tumpe nini Anna wa watu kwa kukomboa sanamu la watu..😅

Jf kwangu nilikuta naijua tu!.. ilikuwa nikisearch Google kitu fulani naona wananidirect huku jf.. mwishowe nikanogewa nikajiunga nikawa member nilianza kama mpole ila sahivi sasa..😎
Jf ni kisima Cha maarifa na ujinga pia na jokes hizo zote ni sifa tulizonazo wanadam,so ni vile tu utaamua uchote kipi uache kipi..

JF njoo ulivyo, akili utazikuta humu.
 
Tumpe nini Anna wa watu kwa kukomboa sanamu la watu..😅

Jf kwangu nilikuta naijua tu!.. ilikuwa nikisearch Google kitu fulani naona wananidirect huku jf.. mwishowe nikanogewa nikajiunga nikawa member nilianza kama mpole ila sahivi sasa..😎
Jf ni kisima Cha maarifa na ujinga pia na jokes hizo zote ni sifa tulizonazo wanadam,so ni vile tu utaamua uchote kipi uache kipi..
Hahahahaha... Kikubwa zaidi kwa JF inakufanya uwe makini. Usiwe mjinga mjinga vinginevyo utafanywa mjinga kwelikweli
 
Jf ni taasisi yenye wafanyakazi na wafanyiwa kazi km jamii nyingine tu.
Ukiishi Jf km ni house boy basi Utakuwa hivyo na ukiishi km Kiduku Lilo utakuwa hivyo pia

Ishi kwa uhalisia wako ufurahi.
 
Kw maelezo yako ya kutufokea nimejifunza kitu kimoja kuwa humu wapo wakina Hannah tu kwahiyo wanahitajika wakina Anna ili kuwasaidia hawa jamaa waliokufundisha hizi tabia na wao wabadilike
 
Kw maelezo yako ya kutufokea nimejifunza kitu kimoja kuwa humu wapo wakina Hannah tu kwahiyo wanahitajika wakina Anna ili kuwasaidia hawa jamaa waliokufundisha hizi tabia na wao wabadilike
Jamaa hawawezi kubadilika, ni sikio la kufa! Ukiondoa makandokando hayo jamaa Wana akili sana
 
Back
Top Bottom