Maisha yangu na baada ya miaka hamsini: Simulizi ya maisha ya Shaaban Robert

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,220
12,725
Hii ni simulizi ya maisha ya Shaaban Robert kama ilivyoandikwa na yeye mwenyewe. Fuatana nami uisome hapa, pia unaweza kuisoma bure ndani ya maktaba app (by pictuss) inayopatikana playstore.

DIBAJI



Ni fahari kubwa kwangu kukaribishwa kuandika maneno machache kuhusu kazi na sifa za marehemu Shaaban Robert kuhusu ufanisi wa lugha ya Kiswahili. Jina la marehemu Shaaban Robert limeota mwamba usiobomoka mioyoni mwa Waafrika wengi wa Afrika ya Mashariki katika karne yetu ya leo. Sifa za marehemu huyu zimeenea pote duniani kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kalamu yake kuihuisha lugha ya Kiswahili na kuieneza makini yake.

Alikuwa mshairi maarufu wa zamani zake na kila aliyewahi kusoma tungo zake katika gazeti la Mambo Leo hakukosa kupata fundisho fulani kwa tungo hizo. Kazi alizokwisha kuziandika na kusomwa na watu zastahili kusomwa mara kwa mara na tena kwani mbinu ya kalamu yake mpaka dakika ya kufa kwake ilikuwa ya hekima tupu (au kwa kileo tusemavyo ya Filosofia).

Napenda kuchukua fursa hii kuwashawishi wasomaji kuzidi kusoma kazi za marehemu huyu ili wapate hekima za maandishi yake. Kadhahka na kuwaomba nao wafuate nyayo zake katika kuiendeleza na kuikuza lugha hii ya Kiswahili -iliyo ya Taifa la Tanzania huu ni kwa Waziri wa Elirnu Sina budi kutoa shukrani nyingi kwa kazi hizi za Shaaban Robert kwani zinatufaa sana kwa ufundishaji katika vyuo vya Tanzania. Mafundisho yake ni makubwa kwa mawazo yake na kwa lugha yake vilevile.

S. N. Eliufoo
Waziri wa elimu
Dar es Salaam
Juni, 1966





MAISHA YANGU



UTANGULIZI


M IAKA kumi imepita tangu mwandishi wa kitabu hiki alipoandika
insha juu ya maisha yake mwenyewe iliyosimulia kwa muhtasari
utoto, michezo, vyuo, kumbi, utu uzima, kazi na arusi. Insha yake
ilifaulu ikapata tuzo ya kwanza katika shindano la kuandika insha
lililofanywa Afrika Mashariki katika mwaka wa 1936. Tangu wakati
huo mambo mengine mengi yaliyohusu maisha yake yalitokea
kwa maendeleo ya umri au yalibadilika kwa kufuata hali mpya.

Mambo hayo mengine yalipasa kusimuliwa vilevile ili kuhitimisha
hadithi ya maisha yake. Kwa hivi kitabu hiki hakikariri matokeo
yaliyokwisha kuhadithiwa ila mambo ambayo kwanza hayakuelezwa.
Kwa sababu hii mwandishi huyu ameacha kando mambo yote
yaliyotokea katika miaka ishirini na sita ya maisha yake.

Shaaban Robert
Tanga
Tanganyika Territory
Septemba 1, 1946



UMRI

NILIKUWA na umri wa miaka ishirini na saba. Maisha yalikuwa bado mapya na matumaini yake yalikuwa mengi sana. Katika afya nilikuwa nimejaa utomvu wa uzima na katika moyo furaha.

Kichwa kilikuwa bado kuota mvi na ugonjwa ulikuwa mbali na mwili. Uchovu ulikuwa kitu kigeni kukiona mwilini. Nilikuwa katika mwanzo tu wa maisha; bado sijafika katikati wala mwisho wake. Kurasa za maisha yangu yaliyopita zilikuwa chache na matendo haba yaliyoandikwa juu yake katika wakati wa nyuma yalikuwa hayawezi kuwatamanisha wengine kuyanakili wala kuniridhisha mimi mwenyewe.

Wakati mmoja nilifikiri kuwa yote yaliyo azizi au bora kwa mtu ni matendo yake aliyotenda zamani; na kwa kuwa mimi sikupata kutenda tendo lolote la maana nilijiona sawa kabisa na maskini. Wazo hili lilibatilishwa na fikira kuwa pengine ubora wa mtu huwezekana kuwa katika wakati ujao. Kwa kujifariji hivi nilijiandaa kusaburi kwa uangalifu sana nishike bahati yangu wakati wowote itokeapo. Kwa desturi bahati ina miujiza mingi sana. Haina ahadi na mtu yeyote na mara nyingi huchelewa kwenda kwa mtu. Kwa hivi wakati mwingi ulipita katika kungoja.

Baadaye bahati ilitokea lakini mara kwa mara niliposimama wima kuiendea niliteleza nikaanguka chini. Nilipotaka kunyosha mkono
kuishika yalitokea mazuio ambayo sikuyatazamia au nilifungiwa
milango ya mbele nisionane nayo.
Milango ya nyuma ya kuifikia bahati ilikuwapo mingi lakini
haikunishawishi hata kidogo. Nilitaka ikiwezekana niweze
kuwajihiana na bahati uso kwa uso mbele ya hadhara siyo
mafichoni. Yamkini mtauliza. Ulingoja bahati gani? Bahati
niliyokuwa nikingoja ilikuwa ni ya kutenda jambo lisilo aibu
mbele ya macho ya watu katika maisha yangu yote. Ikiwa kabla
ya umri wangu wa sasa nilipata kutenda aibu ambayo mimi
mwenyewe sifahamu lakini inayokumbukwa na wengine nilitaka nisitende tena aibu hiyo katika wakati wangu ujao.

Labda utashangaa sababu mimi nilitaka sana bahati ya namna
hii badala ya bahati ya vitu kama vile utajiri au mamlaka juu ya
watu vinavyotafutwa na wengi kwa sababu ya fahari yake. Nasadiki
kuwa utajiri ni kitu cha tamaa na mamlaka yana fahari lakini
nilivihofu vitu hivi sababu pengine wenye vitu hivi kwa wingi na
kufurika aibu iliwatia alama mbaya sana. Niliona mamia ya watu
waliouza roho zao kwa vitu hivi lakini pato lao lote lilikuwa ni
uharibifu wa majina yao. Ukosefu wa jina zuri ni ukiwa mkubwa
duniani. Jambo hili sikulipenda. Nilitaka niwe na jina lililo mbali
na madoa katika umaskini na unyonge wakati wote wa maisha
yangu. Maisha ya mtu ni msingi wa maendeleo ya nchi. Doa lolote
liwezekanalo kuzuiwa kuyaaibisha ni wajibu kushindwa kabisa.

Jambo hili likiwa jepesi au gumu, kumpa moyo mtu au uchovu,
mimi nilikusudia kulipata kwa hali yoyote. Kama nikishindwa
kufaulu kupata lote nilitaka nipate nusu au robo yake. Kidogo
bora kuliko kukosa kabisa; na jaribu dogo la wema bora kuliko kubwa la ubaya. Kurasa za mbele zitaeleza matendo.
 
MAISHA YA NYUMBANI

JAMBO moja kubwa katika mambo ya huzuni kwa watu wote sasa lilitokea. Mke wangu mpenzi alishikwa na maradhi na baada ya muda kidogo wa udhaifu na maumivu akafariki dunia.

Matengano haya kati yetu yalitokea baada ya miaka kumi ya kuishi pamoia kwa mapenzi, amani, raha na buraha. Tokeo hili lilikuwa
pigo kubwa sana kwangu na msiba katika nyumba nzima Marehemu huyu alikuwa johari ya maisha yangu, tegemeo na mshauri mwema. Alinisaidia katika mambo mengi wakati wa maisha yetu pamoja ambayo yangalinishinda kuyatenda mimi peke yangu.



Sura yake ilikuwa jamali kwa kimo cha kadiri. Uso ulikuwa mviringo wa yai, nywele nyeusi za kushuka, paji pana, nyusi za upindi, macho mazuri yaliyokuwa na tazamo juu ya kila kitu, kope za kitana, masikio ya kindo yasiyopitwa na sauti ndogo,
meno yenye mwanya yaliyojipanga vizuri mithili ya lulu katika chaza, ulimi wa fasaha na maneno ya kiada yaliyotawaliwa kila wakati, midomo ya imara isiyokwisha tabasamu, sauti pole na tamko kama wimbo, kidevu cha mfuto katikati yake palikuwa na kidimbwi kidogo, Shingo kama mnara arnbayo juu yake paliota kichwa cha mawazo mengi, chini ya shingo mabega yalikuwa kama matawi ya maua, kifua cha madaha, mikono ya mbinu, tumbo jembamba, miundi ya kunyooka na miguu ya mvungu.

Uzuri wake ulikuwa kamili. Kwa tabia alikuwa mwaminifu na mfano wa kuiga katika nyumba. Wanawake ni wengi kama walivyo wanaume lakini wenye sura kama iliyoelezwa ni adimu sana kukutana nao katika dunia.

Kabla ya kuoa nilitafuta umbo namna yake muda wa miaka kumi.
Kwa maisha mafupi kama tuliyo nayo sasa miaka kumi si muda mdogo; basi kutafuta kwangu kulikuwa si rahisi. Kitu nilichokuwa
nikitafuta kwa muda huo wote nilikipata mwisho lakini baada ya
miaka kumi tu mingine kilikwenda safari watu wasiyorudi na wito usikofika. Mauti yake ya mapema yalikuwa ni msiba na hasara kubwa sana kwangu. Nilishindwa kujizuia kama nilivyotaka
kulia kama hivi:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom