... Akiambatanisha picha za viongozi wa Simba, Mangungu na Try again, Ahmed Ally amesema LEO WAMEZOMEWA !
"Leo tumezomewa kutoka Mtwara hadi Dar, hali ambayo inawaumiza zaidi Wachezaji, hakuna mchezaji anayetaka kufungwa makusudi ili azOmewe. Kuzomewa ni kitendo cha aibu sana"
"Katika nyakati hizi ni vema kila mmoja akaheshimu maumivu ya mwenzie kwani hakuna anayejua mwenzie anaumia kiasi gani"
"Tufane yote lakini tuwaache viongozi wamalize kuugulia baada ya hapo waje watutengenezee timu madhubuti kwa ajili ya msimu ujao"
"Hakuna anayekubali kuharibikiwa katika kazi yake, viongozi wetu wanapambana usiku na mchana kuhakikisha sisi mashabiki tunapata furaha"
"Tuwaunge mkono kwenye kipindi hiki kigumu kwao kwani na wao wanaumia kama sisi na hawana mahala pa kupeleka lawama zao"
Ahmed Ally