Mpui Lyazumbi
JF-Expert Member
- Sep 1, 2010
- 1,910
- 445
Kwa kipato cha shs 542,000 hutakiwi kulalamika. Kuna watanzania kama 85% ambao wanapata 1/4 ya unachopata (135,000) na wanaishi na familia zao watoto wa3 and above na bado utakuta ana kibanda chake Charambe, Kongowe, Kitunda au Kipate.
Wewe una mke na mtoto mmoja na unatumia daladala unalalamika nini. Nakushauri kuwa na vipaumbele, acha makundi ya starehe kama ulevi. uzinzi then hicho kipato kinaweza kukutoa. Hebu tufanye mchanganuo hapa chini.
Tshs 542,000/=
1. Kodi ya nyumba shs 100,000
2. Chakula nyumbani shs 150,000
3. Chakula kazini shs 60,000
4. Nauli ya dala dala 30,000
5. Mengineyo shs 100,000
Jumla ya matumizi ni shs 440,000 hivyo unabaki na akiba ya 102,000. Ukitunza hii akiba kwa miezi sita unaweza ukampatie mke wake mtaji wa shs 612,000 baada ya miezi sita na mkaanza mkakati wa kununu ka plot Gongolamboto.
Chukua huo ushauri na usirudi kijijini utajuta.
wewe una maisha mazuri sana mpendwa ila hujitambui na ndio maana huridhiki. nimeona mahali unasema matumizi nyumbani kwa siku 8,000/-! mbona hapo unaishi kifalme kabisa? uliza wenzio kwa siku wanatenga kiasi gani kuacha nyumbani? utashangaa kuwa karibu nusu ya watanzania wote huacha si zaidi ya 3,000/- ya matumizi kwa siku na hiy ni kwa ajili ya unga, mafuta ya taa, ya kula, maharage, na viungo vyake, na on top of that wana vibanda vyao.
kwenye ofisi ninayofanya mimi (ya serikali) madereva na wahudumu wote wanavibanda vyao na walishajikomboa na nyumba za kupanga na wote hawa ni wa kima cha chini achilia mbali nyongeza za mishahaa za kila mwaka (JK akipenda), yaani hata pendekezo la TUCTA la 350,000/ wanalimezea mate. but wana furaha na courage ya kusonga mbele! sasa wewe una 840,000/ nyumbani kwako kila mwezi kisha unataka kuutupa na kurudi kijijini?
hebu muogope Mungu ndugu yangu, usitamani magari ya watu au kitu chochote usicho na uwezo nacho. mshukuru Mungu kwa kila alichokupa hata kama ni kidogo na usaidie wasio na uwezo kwa kadiri ya uwezo wako, hapo ndipo utakapoona furaha ya maisha na baraka za Mungu zikiongezeka maishani mwako.
kwa kweli mi sioni sababu ya kukata tamaa na maisha kiasi ulichofikia
pia ni vizuri ukajiendeleza kielimu, elimu ni njia ya mkato ya mambo mengi. ukistruggle kuongeza kipato chako mara kumi unaweza kustruggle hadi mwisho wa maisha yako bila kufikia lengo hilo, ila ukiamua kusoma, ni kiasi cha miaka mitatu au minne tu utafikia lengo hilo. tena hata wpte na mkeo mnaweza kwenda shuleni mkaomba mkopo HESLB kulipia masomo yenu na baada ya miaka mitatu/minne hivi, wote mnaona maisha katika mwanga bora! hebu wekeni akili kichwani hapo.
mbarikiwe
Wakati nasona hili bandiko lako, kichwani alinijia yule jasiri wa Tunisia-msomi aliyeamua kujitia kiberiti. Anaitwa Mohamed Bouazizi. Mcheki hapo chiniWakuu Maisha ya Mjini yamenishinda, yaani nikiangalia kipato changu na majukumu niliyonayo naona siwezi kabisa.
Maisha kama haya naona afadhali yale maisha niliishi kwa wazazi wangu enzi za mwalimu pamoja na kuwa babangu alikuwa mkulima lakini tulienda shule na tuliishi maisha mazuri.
Mimi sijui wenzangu mnaishije? mnapata haya machungu nayoyaona mimi? nasimama asubuhi kituoni kwenda kazini naona magari yanapita tu huku mmefunga vioo hivi kweli mna matatizo kama yangu kweli? Hivi nyie pesa mnazipata wapi? mbona najiona mpweke katika nchi yangu hii?
Wakuu siyo siri natafakari kama mambo yakizidi kuwa magumu basi nitafute nauli nirudi kwetu angalau huko nitakuwa na uhakika wa kusogeza siku.
Kipato changu wakuu ni Tshs 542,000/- Nina Mke na mtoto mmoja (5), nimepanga nyumba viwili na sebure - Mambo yamegoma kabisa.
Nipeni ushauri nateketea mtanzania mwenzenu.
Hapo kazini hakuna chance ya kuiba? :usa2:
Mtoto wa kike weye, Remember?Ha Tshs 542,000/- mbona nyingi sana mie napata 233,415/= na ninaishi dala dala kwa sana. Pole mwaya
nakauunga mkono mkuu, kwa mshahara wake anaonekana yuko juu kama ni take home basi huyu mshahara wake(nominal wage) ni kama 700,000. Akope hata mkopo benki ya posta anaweza kupata 6m na watamkata kama 180,000 kwa mwezi sii mbaya akanunue plot ya 1,500,000 zitakazobaki ajenge msingi utakamalika then kila mwezi atafute kama lakin na nusu anunue tofali na mchanga kidogo dogo apandishe vyumba wiwili taratibu.hakuna mtu anaeweza kuwa na cash ya kujengea labda awe fisadi.mambo ya harusi nk hakuna kuchangia,sasa ukilalamika ww na mwalimu au karani mdogo au mhudumu atasema nini? Pia kwani ofisi yako haina allowance ndogo ndogo labda vikao vya hapa na pale(real wage? Jitahidi ndugu kufanya hivo usilale.kama hapo mnapokaa kodi ni kubwa hamieni gongo la mboto huko huko nyumba ni cheap na utapata kiwanja au tafuta viwanja barabara ya bagamoyo ukishavuka tegeta kule vipo na ni rahisi zaidi. Sasa yawezekana unakaa sinza kila siku uko bar na kodi huko ni kubwa lazima maisha yawe magumu.kwa kipato cha shs 542,000 hutakiwi kulalamika. Kuna watanzania kama 85% ambao wanapata 1/4 ya unachopata (135,000) na wanaishi na familia zao watoto wa3 and above na bado utakuta ana kibanda chake charambe, kongowe, kitunda au kipate.
Wewe una mke na mtoto mmoja na unatumia daladala unalalamika nini. Nakushauri kuwa na vipaumbele, acha makundi ya starehe kama ulevi. Uzinzi then hicho kipato kinaweza kukutoa. Hebu tufanye mchanganuo hapa chini.
Tshs 542,000/=
1. Kodi ya nyumba shs 100,000
2. Chakula nyumbani shs 150,000
3. Chakula kazini shs 60,000
4. Nauli ya dala dala 30,000
5. Mengineyo shs 100,000
jumla ya matumizi ni shs 440,000 hivyo unabaki na akiba ya 102,000. Ukitunza hii akiba kwa miezi sita unaweza ukampatie mke wake mtaji wa shs 612,000 baada ya miezi sita na mkaanza mkakati wa kununu ka plot gongolamboto.
Chukua huo ushauri na usirudi kijijini utajuta.
Hapo kazini hakuna chance ya kuiba? :usa2: