Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Magu alifanya kosa Sana mamiradi yake kwa pamoja yamewaletea watz umasikini Mkubwa. Angekewekeza miradi ya kuuinua vijana.
SAsa Ina maana gani kupoteza mda darasani miaka 14 tena ya kusota then unakuja anza SAwa na aliyemaliza la saba
Of course,aliingia na GIA mbaya ya kuharibu biashara na uchumi na kuleta mamiradi ya ajabu ajabu..

Nilikuwa mhanga mwaka 2016 ,ilibidi nirudishe mpira kwa kipa na nilikuwa Dar kipindi hicho..

Kiukweli sitaki tena kuukumbuka huo Mji maana nikipata shuruba sio mchezo baada ya kampuni niliyokuwa nafanya Kazi kufilisika..
 
Vinanipa pesa ya kula na vinanisaidia. Changamoto ni kua havipo kila siku na mahitaji yapo pale pale...
Hiyo ndio changamoto ya vibarua,aitha urudi home au utafute day worker ya Bajaji au pikipiki na utafute hela ya nauli..

Sometime unakuta fundi anakudhulumu nk vinginevyo unaweza kuhisiwa panyaroad ukala chuma 😃😃
 
Wewe ni mjinga huwezi kujua faida za miradi mikubwa
Akili yako iishie kujadili simba na yanga tu
We kula 10% yako kimya kimya,SAsa chato airport ina msaada gani kwa Mlipa kodi,makao makuu Dodoma imeleta matokeo gani kwa kodi yako.
Maendeleo ya vitu bila kureflect maendeleo ya watu ni utakatishaji tu wa kodi zetu.
 
Barabaran tunapishana watu tukiwa na mambo magumu sana moyoni
Juzi nilipitia sehem nikamuuliza jamaa mmoja toilet wapi? Akanijibu kamtafute mama yako akuonyeshe
Jibu alilonipa na matatizo niliyo nayo kidogo nimuue ila nikampotezea nikajua tu na yeye ana majanga yake tu yameshamvuruga Kama mimi
Watu mitaani wamevurugwa na maisha sana,yaani mtu mwenyewe tu kula yake tu nanga inapaa sembuse kuna familia,ndio ukijitokeza kumuongelesha kama ivyo hasira zake lazima akumalizie wewe
 
Salaam,

Hii ni historia fupi ya maisha yangu, naomba ushauri wako wa nini nifanye kuyavuka haya.

Mimi ni kijana umri wangu miaka 30's. Historia yangu kielimu nimepitia mfumo huu wa elimu ya Tanzania (1+7+4+2+3). Baada ya kuhitimu masomo yangu ya chuo (Bachelor of art in sociology, 2015). nilirudi nyumbani kwa wazazi na kuanza kusaka ajira, nilipambana sana kusaka ajira kwa njia zote lakini juhudi zangu ziliishia kwenye hatua ya interview, na kigezo cha experience kikinikosesha ajira nilizokua naomba.

Baada ya kuchezea vichapo vya kutosha kwenye harakati za kusaka ajira, mwaka 2017 nilitoka kwa wazazi na kuanza kuishi geto kwa kuchangia garama za kodi na rafiki angu wa mtaani kwetu. Kwa kipindi hicho nilikua najishughulisha na biashara ya kuuza maji stendi ya mbezi (vibanda vya pembezoni mwa barabara). Hii kazi ilikua inanipa pesa ya kula na kuchangia kodi ya geto. Maisha yakaendelea nikiwa napambana kutafuta ajira rasmi lakini kila interview naambulia patupu.

Niliendelea na hii kazi ya kuuza maji stendi mtaji ukakua nikapanga room yangu mwenyewe na maisha yakasonga, 2018 nilipata mototo wangu wa kwanza, complication za ujauzito na garama za kujifungua kwa upasuaji ziliyumbisha sana biashara lakini nashukuru Mungu kamtaji kidogo kalibaki na mtoto alizaliwa salama

Kwa sababu ya mtaji kuyumba hata faida niliyokua naipata ilipungua + ushindani wa kibiashara ikabidi nitafute kazi ya ziada ili niweze kupata kipato cha kulea mama na mtoto na mimi mwenyewe. Nilichukua bodaboda ya mkataba nikawa nafanya kazi kuanzia saa 12 jioni hadi saa 6 usiku... Mchana nampa mtu deiwaka.

Tarehe 12/11/2018 saa 4 usiku, nikiwa bunju B ni siku nisiyokuja kuisahau katika maisha yangu niliponusurika kuuawa kwenye tukio la kuibiwa pikipiki niliyokua nafanya nayo kazi kwa mkataba. Jamaa walichukua pikipiki na kuniachia majeraha makubwa... Nashukuru Mungu sikuuawa. Nikatibiwa nikapona, balaa likaja namna ya kumalizana na mwenye pikipiki, tukakubaliana kulipana kidogo kidogo kwa miaka miwili.

Biashara yangu ya maji niliendelea nayo hadi mwaka jana pale nilipovunjiwa kibanda changu na mgambo wa jiji kwenye zoezi la kupanga wamachinga, walivunja usiku na sikuambulia chochote hata mbao za kuni nilikosa. Nimepambana sana kutafuta ajira rasmi bila mafanikio. Hata nimekata tamaa kuomba kazi. Maisha yamenipiga sana, uhakika wa kodi sina, uhakika wa kula sina, mwanamke amerudi kwao ili apate wa kumuachia mtoto na yeye akatafute.

Kwa msaada wa ndugu, mwaka jana niliesoma course ya PSV chuo cha NIT, na nina leseni hai class C1, lakini sijabahatika kupata ajira hata ya udereva. Kwa sasa nafanya kazi za saidia fundi, na vibarua mtaani, deni la kulipa pikipiki iliyoibiwa bado sijamaliza, kodi inakaribia kuisha, mtoto na mama nashindwa kutoa matunzo... Mbele naona kiza kinene na sijui nifanye nini kuvuka haya nayopitia.

Najua sipo pekeangu tunaopitia magumu ya kimaisha ya aina hii na wengine magumu zaidi ya haya. Ushauri wako ni muhimu sana.

Asante.
Pole sana kijana mwenzangu,lau ningekuwa na connection sehemu yoyote ile ningekuvutia uzi,changamoto unazopitia nazielewa sana,kwa mtu ambae hajapitia ivyo anaweza ona kama unaigiza ama wewe ni mvivu tu wa kufanya kazi,Pole sana
 
Nimeumia sana,vp kk nyumbani uliondoka salama?namaanisha wazaz walibaririki uondoke?
 
Nchi ngumu Sana hii , yaani maisha ya mwananchi wa kawaida ni unbearable , income inequality , unequal distribution of resources + mismanagement na poor leadership ya serikali ni ticking time bomb ,
Soon tutakuwa kama wasomali na Ethiopians wanaokamatwa kwenye malori wanakimbiia nchi yao
 
Barabaran tunapishana watu tukiwa na mambo magumu sana moyoni
Juzi nilipitia sehem nikamuuliza jamaa mmoja toilet wapi? Akanijibu kamtafute mama yako akuonyeshe
Jibu alilonipa na matatizo niliyo nayo kidogo nimuue ila nikampotezea nikajua tu na yeye ana majanga yake tu yameshamvuruga Kama mimi
hizi Zama watu wanatembea wanaongea peke Yao kama wendawazimu mwigulu mjaaa laana weeee twafaaaaa
 
Barabaran tunapishana watu tukiwa na mambo magumu sana moyoni
Juzi nilipitia sehem nikamuuliza jamaa mmoja toilet wapi? Akanijibu kamtafute mama yako akuonyeshe
Jibu alilonipa na matatizo niliyo nayo kidogo nimuue ila nikampotezea nikajua tu na yeye ana majanga yake tu yameshamvuruga Kama mimi
Nimecheka kama mazuri vile Mungu atusaidie Kwa kweli Hali sio kabisa kitaa
 
Pole kaka mkubwa Changamoto za maisha ni sehemu salama sana Kwa maisha ya mafanikio iwapo utakua mvumilivu so usikate tamaa amini kilakitu kitakaa kwenye mstari
 
Pole sana kijana mwenzangu,lau ningekuwa na connection sehemu yoyote ile ningekuvutia uzi,changamoto unazopitia nazielewa sana,kwa mtu ambae hajapitia ivyo anaweza ona kama unaigiza ama wewe ni mvivu tu wa kufanya kazi,Pole sana
Asante mkuu... Haya ni maisha halisi ya vijana wengi tulio mtaani kwa kukosa ajira. Tuendelee kupambana na kumuomba sana Mungu...
 
Halafu unazaa bado unajua Hali yako yenyewe tete , huyo mtoto unafikiri future yake itakuwaje ?
Nawalaumu Sana watu wanaofanya hivi ,future ya mtu iko determined Sana na mzazi .
Kwa sababu hali yangu ni ngumu ningekataa mimba? Maisha yakiwa tight huruhusiwi kuwa na mtoto? Hii ni kanuni ya wapi.... Si future zote za watoto zinakua determined na hali za kipato cha wazazi wake. Na hii hali niliyonayo sasa haitakua permanent, bado kuna chance ya kupambana kubadilisha mambo, mtoto wangu kwa umri wake wa sasa anapata mahitaji muhimu yote (yale ya lazima) na nahakikisha hilo kwa kidogo nachopata.
 
Pole kaka mkubwa Changamoto za maisha ni sehemu salama sana Kwa maisha ya mafanikio iwapo utakua mvumilivu so usikate tamaa amini kilakitu kitakaa kwenye mstari
Asante kwa kunitia moyo, mkuu. Jah bless
 
Back
Top Bottom