Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Ina wezekana

Member
Sep 2, 2017
72
162
Salaam,

Hii ni historia fupi ya maisha yangu, naomba ushauri wako wa nini nifanye kuyavuka haya.

Mimi ni kijana umri wangu miaka 30's. Historia yangu kielimu nimepitia mfumo huu wa elimu ya Tanzania (1+7+4+2+3). Baada ya kuhitimu masomo yangu ya chuo (Bachelor of art in sociology, 2015). nilirudi nyumbani kwa wazazi na kuanza kusaka ajira, nilipambana sana kusaka ajira kwa njia zote lakini juhudi zangu ziliishia kwenye hatua ya interview, na kigezo cha experience kikinikosesha ajira nilizokua naomba.

Baada ya kuchezea vichapo vya kutosha kwenye harakati za kusaka ajira, mwaka 2017 nilitoka kwa wazazi na kuanza kuishi geto kwa kuchangia garama za kodi na rafiki angu wa mtaani kwetu. Kwa kipindi hicho nilikua najishughulisha na biashara ya kuuza maji stendi ya mbezi (vibanda vya pembezoni mwa barabara). Hii kazi ilikua inanipa pesa ya kula na kuchangia kodi ya geto. Maisha yakaendelea nikiwa napambana kutafuta ajira rasmi lakini kila interview naambulia patupu.

Niliendelea na hii kazi ya kuuza maji stendi mtaji ukakua nikapanga room yangu mwenyewe na maisha yakasonga, 2018 nilipata mototo wangu wa kwanza, complication za ujauzito na garama za kujifungua kwa upasuaji ziliyumbisha sana biashara lakini nashukuru Mungu kamtaji kidogo kalibaki na mtoto alizaliwa salama

Kwa sababu ya mtaji kuyumba hata faida niliyokua naipata ilipungua + ushindani wa kibiashara ikabidi nitafute kazi ya ziada ili niweze kupata kipato cha kulea mama na mtoto na mimi mwenyewe. Nilichukua bodaboda ya mkataba nikawa nafanya kazi kuanzia saa 12 jioni hadi saa 6 usiku... Mchana nampa mtu deiwaka.

Tarehe 12/11/2018 saa 4 usiku, nikiwa bunju B ni siku nisiyokuja kuisahau katika maisha yangu niliponusurika kuuawa kwenye tukio la kuibiwa pikipiki niliyokua nafanya nayo kazi kwa mkataba. Jamaa walichukua pikipiki na kuniachia majeraha makubwa... Nashukuru Mungu sikuuawa. Nikatibiwa nikapona, balaa likaja namna ya kumalizana na mwenye pikipiki, tukakubaliana kulipana kidogo kidogo kwa miaka miwili.

Biashara yangu ya maji niliendelea nayo hadi mwaka jana pale nilipovunjiwa kibanda changu na mgambo wa jiji kwenye zoezi la kupanga wamachinga, walivunja usiku na sikuambulia chochote hata mbao za kuni nilikosa. Nimepambana sana kutafuta ajira rasmi bila mafanikio. Hata nimekata tamaa kuomba kazi. Maisha yamenipiga sana, uhakika wa kodi sina, uhakika wa kula sina, mwanamke amerudi kwao ili apate wa kumuachia mtoto na yeye akatafute.

Kwa msaada wa ndugu, mwaka jana niliesoma course ya PSV chuo cha NIT, na nina leseni hai class C1, lakini sijabahatika kupata ajira hata ya udereva. Kwa sasa nafanya kazi za saidia fundi, na vibarua mtaani, deni la kulipa pikipiki iliyoibiwa bado sijamaliza, kodi inakaribia kuisha, mtoto na mama nashindwa kutoa matunzo... Mbele naona kiza kinene na sijui nifanye nini kuvuka haya nayopitia.

Najua sipo pekeangu tunaopitia magumu ya kimaisha ya aina hii na wengine magumu zaidi ya haya. Ushauri wako ni muhimu sana.

Asante.
 
Jaribu na huku
IMG-20220913-WA0002.jpg
 
National Anthem mwananetu tumshauri vipi hapa? Maana kwa kweli amepitia misuko suko.

Au tumpatie boxer awe analeta buku saba kila leo na bby mama wake tumpe mtaji wa kuuza uji wa ulezi usubuhi
Jamaa yetu anapatia magumu sana. Nafikiri kwanza arudi nyumbani kwao (kwa wazazi au walezi), apate utulivu wa akili, then aanze mchezo upya. Kujipanga kutokea nyumbani sio mbaya..
 
Back
Top Bottom