Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Katafute kazi viwandani ili uweze kujikimu huku akiangalia mambo ya ajira. Huko kwenu kijijini hakuna mashamba ukalime angalau upate mtaji?

Pole sana dogo one day yes.
Asante kwa wazo zuri mkuu. Nilijaribu kiwanda cha sabuni pale mbuyuni dsm. Sometimes hua naenda hapo sema nafasi pale ni chache na wahitaji ni wengi so kila siku wana limited number kulingana na kazi zilizopo siku hiyo. Kama una connection za viwanda vingine naomba maelekezo niende
 
KWA mjini unaweza ukaanza na Kazi ya hata ulinzi but wabongo awathamini walinzi, kampuni binafsi utalipwa elf 80 na tena baada ya siku 40,au KILA baada ya miezi 2,unakulaje unafikaje kazini haiwahusu wao. Hizi za nje hawazidi 280000.
So unaweza ukapiga ulinzi, then wife ana kaanga Mihogo asubui jioni anauza uji, ukiwa off unapambana kivingine. Then mtaji Ukikua mnaona cha kufanya. Japo ni ngumu kupambana ukiwa na familia,
 
Jamaa yetu anapatia magumu sana. Nafikiri kwanza arudi nyumbani kwao (kwa wazazi au walezi), apate utulivu wa akili, then aanze mchezo upya. Kujipanga kutokea nyumbani sio mbaya..
Kurudi nyumbani ni ngumu mkuu. Kwetu mimi ni mtoto wa kwanza wa kiume na wa pili kuzaliwa. Wadogo zangu wapo watano na wazee wangu kwa sasa kulingana na umri wao + maradhi hawana uwezo huo wa kuwahudumia wote, hata hao wadogo zangu wengine wapo kwa ndugu.
 
Unapopata changamoto za kimaisha, mara nyingi majibu yanakuwepo hapo hapo karibu yako...

Focus zaidi ma zaidi, na kamwe usikate tamaaa
 
Maisha yana mambo mengi sana, haupo peke yako katika hali hiyo ni wengi.

Mimi nakushauri Kama nyumbani Kuna ardhi rudi huko kajipange upya, jipe imani kwamba haijalishi umepitia mangapi lakini ipo nafasi ya kufanya comeback muda ujao, na hakika utaipata kesho iliyo bora zaidi.
Asante kwa kunitia moyo mkuu. I appreciate
 
Barabaran tunapishana watu tukiwa na mambo magumu sana moyoni
Juzi nilipitia sehem nikamuuliza jamaa mmoja toilet wapi? Akanijibu kamtafute mama yako akuonyeshe
Jibu alilonipa na matatizo niliyo nayo kidogo nimuue ila nikampotezea nikajua tu na yeye ana majanga yake tu yameshamvuruga Kama mimi
 
Mkuu sina cha kukusaidia zaidi hata mimi bado sijasimama ila what I can say kikubwa muweke Mungu mbele and its not over kitaeleweka tu ukiwa bado una pumzi.
Asante kwa kunitia moyo mkuu. Tuendelee kupambana na kumuomba sana Mungu.
 
Wewe ni mjinga umetoka kabila la watu wavivu wasiowaza kesho zaidi ya kujaza tumbo

Unafikiri maendeleo yanakuja kwa kuwachekea wajinga kama wewe

Usa na ulaya unawaina wameendelea walipitia njia ya moto kufikia pale
Magu alifanya kosa Sana mamiradi yake kwa pamoja yamewaletea watz umasikini Mkubwa. Angekewekeza miradi ya kuuinua vijana.
SAsa Ina maana gani kupoteza mda darasani miaka 14 tena ya kusota then unakuja anza SAwa na aliyemaliza la saba
 
Jikusanyeni muwe watano na rafki zako waaminifu, mkachukue mkopo halmashauri
Nikipata walio interested kuchukua mkopo halmashauri nitafanya hivyo. Changamoto za halmashauri ni kuwa hadi muwe kikundi na mkopo kua mdogo sana, yani hata kuwekeza uzalishe inakua mtihan kwel kweli.
 
Back
Top Bottom