Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Maisha yamenipiga, naomba ushauri

We kula 10% yako kimya kimya,SAsa chato airport ina msaada gani kwa Mlipa kodi,makao makuu Dodoma imeleta matokeo gani kwa kodi yako.
Maendeleo ya vitu bila kureflect maendeleo ya watu ni utakatishaji tu wa kodi zetu.

Mkuu no offence but maendeleo yamegawanyika na sio kila kitu kinachofanywa humu nchini lazima kilete impact direct kwako kuna mengine yataishia kuwapa faida kundi tu la watu fulani tu, mfano we huenda hutoona faida ya wizara zote kuhamia dodoma ila wananchi wanaopata tabu kufanya interview zaman walikua wanazunguka wazara tofauti leo hii wanazipata dodoma kirahisi pia wanadodoma wanazidi kuona jiji lao linavyokua kwa kupanda thamani ya viwanja na mahotel end etc ona SHILIKA LA NYUMBA linavyoipendezesha Dodoma kwa kujenga makazi ya staff na watu wakaida kwa nyumba nzuri na huko chato pia ni Tanzania na kunashughuli za kuingiza madawa kupitia njia ya anga na wanachato wao isingekua mtu wao kufariki wangefaidika zaidi maana ndo alikua na vision nzuri ya anachokijenga..

kimsingi dodoma ndo makao makuu ya nchi sasa kwanin shughuli za kiserikali sifanyike sehem ambapo isio husika ondoa chuki mkuu fikilia kwa ukiwa umefungua moyo!!!


Kwa mwenye thread samahani kwa kuandika mambo yalio nje ya topic but usikatetamaa maamuzi rahisi ndo hugungua njia usiamini sana kwenye maamuzi magumu maana hayapo.
 
Salaam,

Hii ni historia fupi ya maisha yangu, naomba ushauri wako wa nini nifanye kuyavuka haya.

Mimi ni kijana umri wangu miaka 30's. Historia yangu kielimu nimepitia mfumo huu wa elimu ya Tanzania (1+7+4+2+3). Baada ya kuhitimu masomo yangu ya chuo (Bachelor of art in sociology, 2015). nilirudi nyumbani kwa wazazi na kuanza kusaka ajira, nilipambana sana kusaka ajira kwa njia zote lakini juhudi zangu ziliishia kwenye hatua ya interview, na kigezo cha experience kikinikosesha ajira nilizokua naomba.

Baada ya kuchezea vichapo vya kutosha kwenye harakati za kusaka ajira, mwaka 2017 nilitoka kwa wazazi na kuanza kuishi geto kwa kuchangia garama za kodi na rafiki angu wa mtaani kwetu. Kwa kipindi hicho nilikua najishughulisha na biashara ya kuuza maji stendi ya mbezi (vibanda vya pembezoni mwa barabara). Hii kazi ilikua inanipa pesa ya kula na kuchangia kodi ya geto. Maisha yakaendelea nikiwa napambana kutafuta ajira rasmi lakini kila interview naambulia patupu.

Niliendelea na hii kazi ya kuuza maji stendi mtaji ukakua nikapanga room yangu mwenyewe na maisha yakasonga, 2018 nilipata mototo wangu wa kwanza, complication za ujauzito na garama za kujifungua kwa upasuaji ziliyumbisha sana biashara lakini nashukuru Mungu kamtaji kidogo kalibaki na mtoto alizaliwa salama

Kwa sababu ya mtaji kuyumba hata faida niliyokua naipata ilipungua + ushindani wa kibiashara ikabidi nitafute kazi ya ziada ili niweze kupata kipato cha kulea mama na mtoto na mimi mwenyewe. Nilichukua bodaboda ya mkataba nikawa nafanya kazi kuanzia saa 12 jioni hadi saa 6 usiku... Mchana nampa mtu deiwaka.

Tarehe 12/11/2018 saa 4 usiku, nikiwa bunju B ni siku nisiyokuja kuisahau katika maisha yangu niliponusurika kuuawa kwenye tukio la kuibiwa pikipiki niliyokua nafanya nayo kazi kwa mkataba. Jamaa walichukua pikipiki na kuniachia majeraha makubwa... Nashukuru Mungu sikuuawa. Nikatibiwa nikapona, balaa likaja namna ya kumalizana na mwenye pikipiki, tukakubaliana kulipana kidogo kidogo kwa miaka miwili.

Biashara yangu ya maji niliendelea nayo hadi mwaka jana pale nilipovunjiwa kibanda changu na mgambo wa jiji kwenye zoezi la kupanga wamachinga, walivunja usiku na sikuambulia chochote hata mbao za kuni nilikosa. Nimepambana sana kutafuta ajira rasmi bila mafanikio. Hata nimekata tamaa kuomba kazi. Maisha yamenipiga sana, uhakika wa kodi sina, uhakika wa kula sina, mwanamke amerudi kwao ili apate wa kumuachia mtoto na yeye akatafute.

Kwa msaada wa ndugu, mwaka jana niliesoma course ya PSV chuo cha NIT, na nina leseni hai class C1, lakini sijabahatika kupata ajira hata ya udereva. Kwa sasa nafanya kazi za saidia fundi, na vibarua mtaani, deni la kulipa pikipiki iliyoibiwa bado sijamaliza, kodi inakaribia kuisha, mtoto na mama nashindwa kutoa matunzo... Mbele naona kiza kinene na sijui nifanye nini kuvuka haya nayopitia.

Najua sipo pekeangu tunaopitia magumu ya kimaisha ya aina hii na wengine magumu zaidi ya haya. Ushauri wako ni muhimu sana.

Asante.
Mungu akufanyie wepesi...
 
Kwa sababu hali yangu ni ngumu ningekataa mimba? Maisha yakiwa tight huruhusiwi kuwa na mtoto? Hii ni kanuni ya wapi.... Si future zote za watoto zinakua determined na hali za kipato cha wazazi wake. Na hii hali niliyonayo sasa haitakua permanent, bado kuna chance ya kupambana kubadilisha mambo, mtoto wangu kwa umri wake wa sasa anapata mahitaji muhimu yote (yale ya lazima) na nahakikisha hilo kwa kidogo nachopata.
Pambana na Hali yako sasa usitupigie kelele hapa , unapewa ushauri we unaleta ujuaji WA kishamba hapa .
Wewe maisha ya kuunga unga halafu bado unaongeza wategemezi , we huwezi tumia common sense ? Hao watoto na huyo mke utawalisha nyasi ? Au elimu yako haijakukomboa ?
Acha ujinga ! , wewe ulitakiwa kuwa responsible kupambana na maisha Kwanza mpaka use fully stable hayo ya mke na watoto yapo Tu wanawake hawaishi na watoto hawaishi.

Na wewe inaonekana utarudia mistake ya kuongeza mtoto wakati life lako bado la kuunga unga Sana .
Mbadilike nyie watu , life la sasa si kama miaka ya 60 huko , kama hauko strategic life la sasa utateseka Sana na utapotea kabisa
 
Pambana na Hali yako sasa usitupigie kelele hapa , unapewa ushauri we unaleta ujuaji WA kishamba hapa .
Wewe maisha ya kuunga unga halafu bado unaongeza wategemezi , we huwezi tumia common sense ? Hao watoto na huyo mke utawalisha nyasi ? Au elimu yako haijakukomboa ?
Acha ujinga ! , wewe ulitakiwa kuwa responsible kupambana na maisha Kwanza mpaka use fully stable hayo ya mke na watoto yapo Tu wanawake hawaishi na watoto hawaishi.

Na wewe inaonekana utarudia mistake ya kuongeza mtoto wakati life lako bado la kuunga unga Sana .
Mbadilike nyie watu , life la sasa si kama miaka ya 60 huko , kama hauko strategic life la sasa utateseka Sana na utapotea kabisa
nimemshangaa sana kwa lile jbu lake. Hawa ndo wale wanaodanganywaga eti 'kila mtoto anakuja na sahan yake'
 
Hivi tukiamua kuchanga jero,buku,buku tano, kumi ishirini laki na kadharika.. Then atafutwe mtu anunue pikipiki mdau akabidhiwe c tutakua tumemuokoa mtz mmja kutoka kwenye msongo...
Ni maoni tu
 
Jamaa yetu anapatia magumu sana. Nafikiri kwanza arudi nyumbani kwao (kwa wazazi au walezi), apate utulivu wa akili, then aanze mchezo upya. Kujipanga kutokea nyumbani sio mbaya..
Hata mimi nilitaka kumshauri kama wewe. Nyumbani huwa tunapata utulivu wa kutosha na kuanza upya.
 
Hata mimi nilitaka kumshauri kama wewe. Nyumbani huwa tunapata utulivu wa kutosha na kuanza upya.
Kweli kabisa, ingawa wengine ukiwambii warudi makwao wanaona kama ume wadharau, ila ni sehemu nzuri sana ya kujipanga na kupata mwanzi mpya
 
Ivi mtu akiwa na ardhi ndo anatoboa vipi kwa hali kama yake yani kuuza ardhi au kilimo?

Nilijaribu kilimo mwaka jana mbona kuna gharama au kuna altanative ya bila kutumia pesa kufanya kilimo au mimi ndo nilikua napigwa
Inategemea ulifanya kilimo gani, halafu kilimo cha namna hii ya mshikaji siyo kikubwa cha kuhitaji mtaji mkubwa. Unaanza kidogo kidogo ili uweze kuishi.Kadri unavyozoea ndivyo unazidi kuongeza ukubwa wa kilimo, huku pembeni ukiwa na ufugaji.

Mfano watu wanaanza na ufugaji wa kuku 4,kilimo cha mihogo, viazi, maharage, mahindi hivi vyote vinawezekana kufanyika kidogo kidogo mpaka unapanuka.
 
maisha ya graduates wengi mtaani ni script yenye uwezo wa kutoa movie kali sana ikashinda hata tunzo ya Oscar
 
Back
Top Bottom