Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Kijijini ukitengeneza mashine manual ya kupanda mazao, kupukuchua mazao , kupiga mpunga, mtama, kupalilia, kumenya muhogo, kukamua mafuta, nk. Huwezi kufa njaa. Wakulima wanataka Sana huduma hizi.
Mashine upukuchukua gunia 20 kwa saa kila gunia ni sh elf 2 kupukuchua,
Mashine upanda mazao heka 5 kwa siku kupanda heka moja ni sh elf 20,
Wazo zuri sana hili mkuu. Tatizo mtaji, wa kupata mashine za aina hiyo
 
Barabaran tunapishana watu tukiwa na mambo magumu sana moyoni
Juzi nilipitia sehem nikamuuliza jamaa mmoja toilet wapi? Akanijibu kamtafute mama yako akuonyeshe
Jibu alilonipa na matatizo niliyo nayo kidogo nimuue ila nikampotezea nikajua tu na yeye ana majanga yake tu yameshamvuruga Kama mimi
Matatizo kila mtu anayo. Cha muhimu ni kuwa humble. Haina maana kujibu vibaya kwa sababu ya matatizo yako.
 
Wewe ni mjinga umetoka kabila la watu wavivu wasiowaza kesho zaidi ya kujaza tumbo

Unafikiri maendeleo yanakuja kwa kuwachekea wajinga kama wewe

Usa na ulaya unawaina wameendelea walipitia njia ya moto kufikia pale
We kula 10% yako kimya kimya,SAsa chato airport ina msaada gani kwa Mlipa kodi,makao makuu Dodoma imeleta matokeo gani kwa kodi yako.
Maendeleo ya vitu bila kureflect maendeleo ya watu ni utakatishaji tu wa kodi zetu.
 
Salaam,

Hii ni historia fupi ya maisha yangu, naomba ushauri wako wa nini nifanye kuyavuka haya.

Mimi ni kijana umri wangu miaka 30's. Historia yangu kielimu nimepitia mfumo huu wa elimu ya Tanzania (1+7+4+2+3). Baada ya kuhitimu masomo yangu ya chuo (Bachelor of art in sociology, 2015). nilirudi nyumbani kwa wazazi na kuanza kusaka ajira, nilipambana sana kusaka ajira kwa njia zote lakini juhudi zangu ziliishia kwenye hatua ya interview, na kigezo cha experience kikinikosesha ajira nilizokua naomba.

Baada ya kuchezea vichapo vya kutosha kwenye harakati za kusaka ajira, mwaka 2017 nilitoka kwa wazazi na kuanza kuishi geto kwa kuchangia garama za kodi na rafiki angu wa mtaani kwetu. Kwa kipindi hicho nilikua najishughulisha na biashara ya kuuza maji stendi ya mbezi (vibanda vya pembezoni mwa barabara). Hii kazi ilikua inanipa pesa ya kula na kuchangia kodi ya geto. Maisha yakaendelea nikiwa napambana kutafuta ajira rasmi lakini kila interview naambulia patupu.

Niliendelea na hii kazi ya kuuza maji stendi mtaji ukakua nikapanga room yangu mwenyewe na maisha yakasonga, 2018 nilipata mototo wangu wa kwanza, complication za ujauzito na garama za kujifungua kwa upasuaji ziliyumbisha sana biashara lakini nashukuru Mungu kamtaji kidogo kalibaki na mtoto alizaliwa salama

Kwa sababu ya mtaji kuyumba hata faida niliyokua naipata ilipungua + ushindani wa kibiashara ikabidi nitafute kazi ya ziada ili niweze kupata kipato cha kulea mama na mtoto na mimi mwenyewe. Nilichukua bodaboda ya mkataba nikawa nafanya kazi kuanzia saa 12 jioni hadi saa 6 usiku... Mchana nampa mtu deiwaka.

Tarehe 12/11/2018 saa 4 usiku, nikiwa bunju B ni siku nisiyokuja kuisahau katika maisha yangu niliponusurika kuuawa kwenye tukio la kuibiwa pikipiki niliyokua nafanya nayo kazi kwa mkataba. Jamaa walichukua pikipiki na kuniachia majeraha makubwa... Nashukuru Mungu sikuuawa. Nikatibiwa nikapona, balaa likaja namna ya kumalizana na mwenye pikipiki, tukakubaliana kulipana kidogo kidogo kwa miaka miwili.

Biashara yangu ya maji niliendelea nayo hadi mwaka jana pale nilipovunjiwa kibanda changu na mgambo wa jiji kwenye zoezi la kupanga wamachinga, walivunja usiku na sikuambulia chochote hata mbao za kuni nilikosa. Nimepambana sana kutafuta ajira rasmi bila mafanikio. Hata nimekata tamaa kuomba kazi. Maisha yamenipiga sana, uhakika wa kodi sina, uhakika wa kula sina, mwanamke amerudi kwao ili apate wa kumuachia mtoto na yeye akatafute.

Kwa msaada wa ndugu, mwaka jana niliesoma course ya PSV chuo cha NIT, na nina leseni hai class C1, lakini sijabahatika kupata ajira hata ya udereva. Kwa sasa nafanya kazi za saidia fundi, na vibarua mtaani, deni la kulipa pikipiki iliyoibiwa bado sijamaliza, kodi inakaribia kuisha, mtoto na mama nashindwa kutoa matunzo... Mbele naona kiza kinene na sijui nifanye nini kuvuka haya nayopitia.

Najua sipo pekeangu tunaopitia magumu ya kimaisha ya aina hii na wengine magumu zaidi ya haya. Ushauri wako ni muhimu sana.

Asante.
Mipango niliyonayo Kwa sasa

1. kuendelea kuomba kazi ya kuajiriwa kwa juhudi zote (mpango endelevu)
2. Kutafuta pikipiki na kufanya bolt
3. Kufungua kijiwe cha biashara ya kuuza utumbo wa ngombe.
 
Pole sana Mungu akafungue milango kwako, usikate tamaa kabisa Mungu akusaidie.
 
Mkuu ukisoma hii comment yangu,naomba unichek PM.
 
Una shahada ya kwanza ya sociology,una leseni class C na bado u kijana-hizo ni sifa zenye thamani kubwa. Kwa ushauri uliopewa naongeza huu: kwa maksudi jiunge na mtandao wa watu wenye ushawishi na uwezo.
 
Barabaran tunapishana watu tukiwa na mambo magumu sana moyoni
Juzi nilipitia sehem nikamuuliza jamaa mmoja toilet wapi? Akanijibu kamtafute mama yako akuonyeshe
Jibu alilonipa na matatizo niliyo nayo kidogo nimuue ila nikampotezea nikajua tu na yeye ana majanga yake tu yameshamvuruga Kama mimi
Teh teh teh!
 
Kwani hivyo vibarua na saidia fundi havikupi hela? Mbona watu wanaishi tu mtaan kwa hivyo vibarua...?
Nimewahi kuishi Dar Kwa kutegemea saidia fundi baada ya kupigika japo ni mateso makubwa ila huna namna..

Kiukweli nilirudisha mpira kwa kipa tena kwa kupata msaada wa nauli kutoka kwa jamaa ambae tuliwahi soma shule moja,nikaja kujipanga upya japo Nako mkoani nilikomaa na saidia fundi..

Connection ndio ilikuja kunipa unafuu..Usiombe yakukute 😁😁
 
Back
Top Bottom