Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Sisi sote ni masikini KOSA KUBWA ni kuzaa ukiwa huna maisha yakueleweka na kipato.

Unampa tabu kiumbe ukiyemleta duniani.

Hii tabia ya kuzaa kuzaa huku ukiwa huna uchumi wa kueleweka Mimi naipiga vita sana mnawapa watoto wenu tabu na shida zenu.

Umezaliwa kwenye umasikini unammleta kiumbe kisicho na hatia kwenye umasikini wenu hii sio fair kabisa.

Watoto ni muhimu sana LAKINI tunahitaji subira kuwaandalia maisha yenye unafuu.

Vijana wa siku hizi mnazingua sana na tatizo kubwa mmendekeza ngono zembe.

Unaweza dhani umelaaniwa au huna bahati kumbe maisha yako yanajiendea tu bila mkakati Wala mpango.

Kazi ya kuuza maji nilikuwa safari ya mwanzo kabisa kukutoa kwenye lindi umasikini ingeweza kufanya ukapata mtaji zaidi ukafungua biashara kubwa ambayo ingekutoa maisha.

Kama kuuza maji kumekuwezesha kupanga geto na kulipa Kodi mbona ungefanikiwa tu

Tatizo lako mindset Yako inawaza ajira tu na hukipendi unachokifanya hili ni tatizo la graduates wengi.

Ukampa mtu na mimba kwa maisha ya kubaingaiza ukajididimiza down wewe mwenyewe kwa mikono na akili Yako.

Anyway achana na hizo ajira inawaza maana hio sociology kama sio uafisa wa ustawi wa jamii au dawati la jinsia hakuna kazi.

So option ulio nayo kukomaa na hizo mbishe za mtaani.

Nakuombea ufanikiwe ila funga zipi mzee kama utafungua fungua akili na mahesabu.
 
nimemshangaa sana kwa lile jbu lake. Hawa ndo wale wanaodanganywaga eti 'kila mtoto anakuja na sahan yake'
Mtoa mada ni naive sana. Hajui namna cycle of poverty ilivyo na jinsi hali ya wazazi inavyo determine future ya watoto wao kwa asilimia karibia 100.
Aendelee kujidanganya ikiwezekana aongeze watoto wafike hata sita.
 
Salaam,

Hii ni historia fupi ya maisha yangu, naomba ushauri wako wa nini nifanye kuyavuka haya.

Mimi ni kijana umri wangu miaka 30's. Historia yangu kielimu nimepitia mfumo huu wa elimu ya Tanzania (1+7+4+2+3). Baada ya kuhitimu masomo yangu ya chuo (Bachelor of art in sociology, 2015). nilirudi nyumbani kwa wazazi na kuanza kusaka ajira, nilipambana sana kusaka ajira kwa njia zote lakini juhudi zangu ziliishia kwenye hatua ya interview, na kigezo cha experience kikinikosesha ajira nilizokua naomba.

Baada ya kuchezea vichapo vya kutosha kwenye harakati za kusaka ajira, mwaka 2017 nilitoka kwa wazazi na kuanza kuishi geto kwa kuchangia garama za kodi na rafiki angu wa mtaani kwetu. Kwa kipindi hicho nilikua najishughulisha na biashara ya kuuza maji stendi ya mbezi (vibanda vya pembezoni mwa barabara). Hii kazi ilikua inanipa pesa ya kula na kuchangia kodi ya geto. Maisha yakaendelea nikiwa napambana kutafuta ajira rasmi lakini kila interview naambulia patupu.

Niliendelea na hii kazi ya kuuza maji stendi mtaji ukakua nikapanga room yangu mwenyewe na maisha yakasonga, 2018 nilipata mototo wangu wa kwanza, complication za ujauzito na garama za kujifungua kwa upasuaji ziliyumbisha sana biashara lakini nashukuru Mungu kamtaji kidogo kalibaki na mtoto alizaliwa salama

Kwa sababu ya mtaji kuyumba hata faida niliyokua naipata ilipungua + ushindani wa kibiashara ikabidi nitafute kazi ya ziada ili niweze kupata kipato cha kulea mama na mtoto na mimi mwenyewe. Nilichukua bodaboda ya mkataba nikawa nafanya kazi kuanzia saa 12 jioni hadi saa 6 usiku... Mchana nampa mtu deiwaka.

Tarehe 12/11/2018 saa 4 usiku, nikiwa bunju B ni siku nisiyokuja kuisahau katika maisha yangu niliponusurika kuuawa kwenye tukio la kuibiwa pikipiki niliyokua nafanya nayo kazi kwa mkataba. Jamaa walichukua pikipiki na kuniachia majeraha makubwa... Nashukuru Mungu sikuuawa. Nikatibiwa nikapona, balaa likaja namna ya kumalizana na mwenye pikipiki, tukakubaliana kulipana kidogo kidogo kwa miaka miwili.

Biashara yangu ya maji niliendelea nayo hadi mwaka jana pale nilipovunjiwa kibanda changu na mgambo wa jiji kwenye zoezi la kupanga wamachinga, walivunja usiku na sikuambulia chochote hata mbao za kuni nilikosa. Nimepambana sana kutafuta ajira rasmi bila mafanikio. Hata nimekata tamaa kuomba kazi. Maisha yamenipiga sana, uhakika wa kodi sina, uhakika wa kula sina, mwanamke amerudi kwao ili apate wa kumuachia mtoto na yeye akatafute.

Kwa msaada wa ndugu, mwaka jana niliesoma course ya PSV chuo cha NIT, na nina leseni hai class C1, lakini sijabahatika kupata ajira hata ya udereva. Kwa sasa nafanya kazi za saidia fundi, na vibarua mtaani, deni la kulipa pikipiki iliyoibiwa bado sijamaliza, kodi inakaribia kuisha, mtoto na mama nashindwa kutoa matunzo... Mbele naona kiza kinene na sijui nifanye nini kuvuka haya nayopitia.

Najua sipo pekeangu tunaopitia magumu ya kimaisha ya aina hii na wengine magumu zaidi ya haya. Ushauri wako ni muhimu sana.

Asante.
Nikupongeze Kwa uandishi mzur....
Nimepitia maoni ya wadau mbali mbali..
Kuna jamaa kasema atachangia laki Moja...
Story yako imenitouch sana nimesisimka pia nimelengwa na machozi....
Sikujui hunijui ila Leo ningefanya arrangements Kuna nafasi za kazi sehemu kwenye kampuni Kuna maslah mazur tu ninge ku connect ila Kwa Sasa nimesitisha kusaidia watu maana Kuna madogo wamefanya upigaji mkubwa...so nime be dis appointed kuwabeba watu.....najua sitakiwi ku generalized ila ngoja nipumzike.

Mama mzazi aliwai kunambia am 4 real mwanangu siku yako ipo....
Nili ingoja sana mixer kukata Tamaa ila ilifika japo niliona imechelewa...nikutie moyo Never give up.
Wadau Issues hapa ni connection...tumsaidie kumpa connection.
Kuna jamaa wanaitwa WATU unaweza ku google wanakopesha piki piki...kinacho takiwa ni KADI ya nida na mdhamini wapo maeneo mengi kianzio ni kama laki 3....

Kuna mdau humu kama atakua serious kasema atachangia laki..
Mimi ntamchangia elfu 50.... Wadau wengine wajipige pige tupate laki 3... Akachukue japo loan ya piki piki japo HUNTER Marejesho atafanya mwenyew weekly
Pia naomba wadau kama mtapitisha hii hoja...
Humu Kuna watu wengi waaminifu achaguliwe mmoja mwenye muda na nafasi awe kama mwenyekiti tumsimamie mwenzetu najua waitaji ni wengi ila tufanye kitu Kwa mwenzetu...Nimpe Rai ndugu yetu 'Ina wezekana' asituangushe.
Naomba kuwasilisha.
 
Duuh kumbe kuna watu wana changamoto kuliko mm daaah ngoja niendelee ku hustler tu pole sana mkuuu
 
Mkuu ulitekeleza hii ahadi?
 
Pole sana ndugu yangu kwa ushauri wangu mimi naona kama kuna uwezekano wa kupata mkataba chukua tu mkataba kaka
 
Maisha hayajawahi kuwa raisi, ondoka apo mjini tafuta kijiji au rudi kijijini kwenu, maisha ya kijijini hayana pressure, anza kufuga kuku, lima kwa kiasi uwezacho jitaidi kila mwaka unaongeza kilimo na ufugaji baaada ya muda mfupi utanirudia kwa mafanikio.....mjini matumizi makubwa, pesa ngumu kupatikana alafu pressure ya maisha ni kubwa sana
 
Back
Top Bottom