Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Maisha yamenipiga, naomba ushauri

Salaam...

Hii ni historia fupi ya maisha yangu, naomba ushauri wako wa nini nifanye kuyavuka haya...

Mimi ni kijana umri wangu miaka 30's. Historia yangu kielimu nimepitia mfumo huu wa elimu ya Tanzania (1+7+4+2+3)... Baada ya kuhitimu masomo yangu ya chuo (Bachelor of art in sociology, 2015). nilirudi nyumbani kwa wazazi na kuanza kusaka ajira, nilipambana sana kusaka ajira kwa njia zote lakini juhudi zangu ziliishia kwenye hatua ya interview, na kigezo cha experience kikinikosesha ajira nilizokua naomba,

Baada ya kuchezea vichapo vya kutosha kwenye harakati za kusaka ajira, mwaka 2017 nilitoka kwa wazazi na kuanza kuishi geto kwa kuchangia garama za kodi na rafiki angu wa mtaani kwetu... Kwa kipindi hicho nilikua najishughulisha na biashara ya kuuza maji stendi ya mbezi (vibanda vya pembezoni mwa barabara). Hii kazi ilikua inanipa pesa ya kula na kuchangia kodi ya geto. Maisha yakaendelea nikiwa napambana kutafuta ajira rasmi lakini kila interview naambulia patupu.

Niliendelea na hii kazi ya kuuza maji stendi mtaji ukakua nikapanga room yangu mwenyewe na maisha yakasonga, 2018 nilipata mototo wangu wa kwanza, complication za ujauzito na garama za kujifungua kwa upasuaji ziliyumbisha sana biashara lakini nashukuru Mungu kamtaji kidogo kalibaki na mtoto alizaliwa salama

Kwa sababu ya mtaji kuyumba hata faida niliyokua naipata ilipungua + ushindani wa kibiashara ikabidi nitafute kazi ya ziada ili niweze kupata kipato cha kulea mama na mtoto na mimi mwenyewe. Nilichukua bodaboda ya mkataba nikawa nafanya kazi kuanzia saa 12 jioni hadi saa 6 usiku... Mchana nampa mtu deiwaka.

Tarehe 12/11/2018 saa 4 usiku, nikiwa bunju B ni siku nisiyokuja kuisahau katika maisha yangu niliponusurika kuuawa kwenye tukio la kuibiwa pikipiki niliyokua nafanya nayo kazi kwa mkataba. Jamaa walichukua pikipiki na kuniachia majeraha makubwa... Nashukuru Mungu sikuuawa. Nikatibiwa nikapona, balaa likaja namna ya kumalizana na mwenye pikipiki, tukakubaliana kulipana kidogo kidogo kwa miaka miwili.

Biashara yangu ya maji niliendelea nayo hadi mwaka jana pale nilipovunjiwa kibanda changu na mgambo wa jiji kwenye zoezi la kupanga wamachinga, walivunja usiku na sikuambulia chochote hata mbao za kuni nilikosa. Nimepambana sana kutafuta ajira rasmi bila mafanikio... Hata nimekata tamaa kuomba kazi. Maisha yamenipiga sana, uhakika wa kodi sina, uhakika wa kula sina, mwanamke amerudi kwao ili apate wa kumuachia mtoto na yeye akatafute.

Kwa msaada wa ndugu, mwaka jana niliesoma course ya PSV chuo cha NIT, na nina leseni hai class C1, lakini sijabahatika kupata ajira hata ya udereva. Kwa sasa nafanya kazi za saidia fundi, na vibarua mtaani, deni la kulipa pikipiki iliyoibiwa bado sijamaliza, kodi inakaribia kuisha, mtoto na mama nashindwa kutoa matunzo... Mbele naona kiza kinene na sijui nifanye nini kuvuka haya nayopitia.

Najua sipo pekeangu tunaopitia magumu ya kimaisha ya aina hii na wengine magumu zaidi ya haya. Ushauri wako ni muhimu sana

Asante.
Usipagawe, usichachawe,nenda mdogo mdogo kapanga manani,usipagawe usichachawe matatizo yapo,yako ni mitihani.

Bro pole sana ila tambua kuna mwisho wa matatizo,utakuja pata nuru angavu.

Juhudi+nia=utafanikiwa.

Omba sana mungu akupitishe kipindi hiki kigumu
 
Chagua moja ya wazo hapa kwa mtaji kidogo unaweza.
IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO


1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.utengenezaji wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71.Utengenezaji mifagio
72.utengenezaji crips za Mihogo,ndizi,viazi,nk
73.Utengenezaji tambi,ubuyu
74.panda mlonge,au nyonyo,au mibono au muarobaini Ili uje uuze mafuta,au utengeneze sabuni.
75.Kutengeneza siagi ya karanga
76.Home delivery hapa ni kupita KILA nyumba na kuchukua oda za mahitaji yao then unaenda kununua unawaletea
77.Utengezaji wa vifungashio vya karatasi
78.utengenezaji mitungi,vyungu,majiko ya udongo
79.Kilimo cha mboga mboga.
 
Kwani hivyo vibarua na saidia fundi havikupi hela? Mbona watu wanaishi tu mtaan kwa hivyo vibarua...?
Hao mafundi wenyewe wanarudi Bush. Kuna kit maisha yanataka wengi hatuambiw. Pia watu tunashindwa kuendan na Kas ya mabadiliko y maisha. Kwa dunia ya sasa saidia fundi wengi nafuu yao ni kugeuka bodaboda
 
Hii mistari uliyoiandika ni bonge moja ya hit Song mkuu ila usichoke kupambana ukianguka nyanyuka kuna watu wako karibu nawe watakunyanyua jikung'ute vumbi kisha songa mbele haupo peke yako katika msoto wa maisha kikubwa ni kutokukata tamaa amini kuna kesho yenye mafanikio ipo kwa ajili yako
 
Kijijini ukitengeneza mashine manual ya kupanda mazao, kupukuchua mazao , kupiga mpunga, mtama, kupalilia, kumenya muhogo, kukamua mafuta, nk. Huwezi kufa njaa. Wakulima wanataka Sana huduma hizi.
Mashine upukuchukua gunia 20 kwa saa kila gunia ni sh elf 2 kupukuchua,
Mashine upanda mazao heka 5 kwa siku kupanda heka moja ni sh elf 20,
 
Kwani hivyo vibarua na saidia fundi havikupi hela? Mbona watu wanaishi tu mtaan kwa hivyo vibarua...?
Havikupi uhakika wa kazi kila siku ndiyo changamoto yake. vingekuwa vnakupa uhakika wa kazi kila siku isingekuwa shida.
 
Magu alifanya kosa Sana mamiradi yake kwa pamoja yamewaletea watz umasikini Mkubwa. Angekewekeza miradi ya kuuinua vijana.
SAsa Ina maana gani kupoteza mda darasani miaka 14 tena ya kusota then unakuja anza SAwa na aliyemaliza la saba
 
Mwamba hapo rudi tu home kijijini kale ugali wa bure uanze upya popote penye watu pana fursa ni kujifunza nini uanze nacho.
Still kilimo cha mazao yasiyohitaji mvua nyingi ndio solution ya starting point.
 
Back
Top Bottom