Maisha yamenichapa haswa

Kama hauna aibu kama mimi au sio bishoo. Uza simu hiyo ingia sokoni asubuhi ununue tenga la nyanya utembeze na baiskeli hapo mjini daslam lazima utapata hata 5000 ya kula kila siku.

Regret haitakutatulia matatizo. Tushapitia hizo shida na sisi. Nilianza kuuza simu ili nipate hela ya kula, nikanunua kitochi. Hela ilivyokata nikauza jiko la gesi. Ahahahhahaaa

Jamani maisha magumu yasikieni kwa watu tu mkihadithiwa... maana unaishi kwa stress hatari, ukiwa na buku kumi mfukoni unaogopa hata kuichenchi maana unakuwa unawaza ikiisha sijui ndo utakufa...

Ila itabidi upambane mkuu hamna namna, ukishindwa kabisa rudi kijijini ukaanza moja kabisa, maana haina maana upo mjini halafu unaishi maisha ya digidigi... ikiwa ngumu sana usifosi, rudi kijijini hata ukalime.
 
Dah.... tenga moja la nyanya ni elfu 60 pale mabibo.... na lina nyanya 600.... akigawa mafungu ya nyanya 4 atapata mafungu 150...akauza buku kila fungu atatengeneza laki na nusu...yaani faida ya elfu 90 kila tenga.....na kama akifanikiwa kuuza matenga yote 5 kwa siku hapo unaongelea faida ya laki 4 kwa siku....na ukumbuke kesho atarudi mabibo akiwa na laki 7 mfukoni....akiamua hiyo laki ajipongeze halafu anunue matenga 10....Dah
Sio rahisi kihivyo hasa kwa mtu ambae Hana uzoefu na biashara, ninachomshauri ajiripue tu aondoe aibu afamye anachoweza kufanya atatoboa kwa uwezo wa Allah
 
Kama hauna aibu kama mimi au sio bishoo. Uza simu hiyo ingia sokoni asubuhi ununue tenga la nyanya utembeze na baiskeli hapo mjini daslam lazima utapata hata 5000 ya kula kila siku.

Regret haitakutatulia matatizo. Tushapitia hizo shida na sisi. Nilianza kuuza simu ili nipate hela ya kula, nikanunua kitochi. Hela ilivyokata nikauza jiko la gesi. Ahahahhahaaa

Jamani maisha magumu yasikieni kwa watu tu mkihadithiwa... maana unaishi kwa stress hatari, ukiwa na buku kumi mfukoni unaogopa hata kuichenchi maana unakuwa unawaza ikiisha sijui ndo utakufa...

Ila itabidi upambane mkuu hamna namna, ukishindwa kabisa rudi kijijini ukaanza moja kabisa, maana haina maana upo mjini halafu unaishi maisha ya digidigi... ikiwa ngumu sana usifosi, rudi kijijini hata ukalime.
Wewe ni tapeli
 
Pole sana hauko peke yako ndugu yangu unajua nini cha kufanya............Fungia vyeti vyote ulivyokua navyo halafu ingia mtaani ki ukali, usichague kazi, hakikisha unatumia kidogo kuliko unachokipata nitafute baada ya miezi 6 ni matumaini utakuja kunishukuru ndugu pole sana uchaguzi ni wako!!!!!
 
Wakuu, nahisi naongea peke yangu au nacheka peke yangu ila sijapata mtu tu wa kuniambia kwa jinsi life lilivonichapa.

Kazi niliyokuwa nayo sina tena, marafiki niliyokuwa na kunywa nao hawapo tena, simu yangu siku nzima saa 24 hakuna hata missed call.

Nashindwa kupita mtaani, natoka ghetto asubuhi saa 12 narudi usiku sana naogopa vidole mtaani.

Bili ya umeme na maji nimekuwa mdaiwa sugu, bado Kodi ya nyumba.

Yaani mpaka nimesema, mpenzi wangu yule nilikuwa nawaletea visa vyake nae kaniacha kikatili sana.

Mungu atusaidie vijana tunapitia magumu sana!
Yatapita tu, usikate tamaa
 
maisha hayajawahi kua fair brother! hebu angalia hii

uko hai mzima wa afya kuna mwengine anapigania uhai wake icu

una pa kulala walau utadaiwa kodi kuna mwenzio hajui usiku ukiingia atalala wapi

una sim umeweza kutype jf kuna mwenzio anaitaman awe nayo hata aspopigiwa yeye awe na simu

unajua nn jifunze kushukuru kwa kidogo ulichonacho usiache kupambana hujui muda wala siku ya kutusua

NAKAZIA
 
Wakuu, nahisi naongea peke yangu au nacheka peke yangu ila sijapata mtu tu wa kuniambia kwa jinsi life lilivonichapa.

Kazi niliyokuwa nayo sina tena, marafiki niliyokuwa na kunywa nao hawapo tena, simu yangu siku nzima saa 24 hakuna hata missed call.

Nashindwa kupita mtaani, natoka ghetto asubuhi saa 12 narudi usiku sana naogopa vidole mtaani.

Bili ya umeme na maji nimekuwa mdaiwa sugu, bado Kodi ya nyumba.

Yaani mpaka nimesema, mpenzi wangu yule nilikuwa nawaletea visa vyake nae kaniacha kikatili sana.

Mungu atusaidie vijana tunapitia magumu sana!
Siku zote kwenye maisha, wekeza hela kwenye mali ambayo hata ukiyumba itakusaidia wewe ila usiwekeze kwa wanawake na marafiki.
Mwanamke akikuomba 50,000 mpe 10,000 nyingine bora ununue pazia mlangoni maana hutokea pazia likawa linathamani sana kuliko mpenzi
 
Back
Top Bottom