Maisha yamenichapa haswa

Maisha yamenichapa haswa

Wakuu, nahisi naongea peke yangu au nacheka peke yangu ila sijapata mtu tu wa kuniambia kwa jinsi life lilivonichapa.

Kazi niliyokuwa nayo sina tena, marafiki niliyokuwa na kunywa nao hawapo tena, simu yangu siku nzima saa 24 hakuna hata missed call.

Nashindwa kupita mtaani, natoka ghetto asubuhi saa 12 narudi usiku sana naogopa vidole mtaani.

Bili ya umeme na maji nimekuwa mdaiwa sugu, bado Kodi ya nyumba.

Yaani mpaka nimesema, mpenzi wangu yule nilikuwa nawaletea visa vyake nae kaniacha kikatili sana.

Mungu atusaidie vijana tunapitia magumu sana!
Yaani wewe simu yako haiiti 24 hours Mimi simu yangu. Kwa mwaka huu haijawahi kupigwa hata Mara. Moja tangu mwaka huu uanze acha hizo bana Kila mtu maisha yampiga hatusemi tu just move on and never give up bro
 
maisha hayajawahi kua fair brother! hebu angalia hii

uko hai mzima wa afya kuna mwengine anapigania uhai wake icu

una pa kulala walau utadaiwa kodi kuna mwenzio hajui usiku ukiingia atalala wapi

una sim umeweza kutype jf kuna mwenzio anaitaman awe nayo hata aspopigiwa yeye awe na simu

unajua nn jifunze kushukuru kwa kidogo ulichonacho usiache kupambana hujui muda wala siku ya kutusua
Haya mawazo Kama yametoka Kwa
My wife to be
 
Wakuu, nahisi naongea peke yangu au nacheka peke yangu ila sijapata mtu tu wa kuniambia kwa jinsi life lilivonichapa.

Kazi niliyokuwa nayo sina tena, marafiki niliyokuwa na kunywa nao hawapo tena, simu yangu siku nzima saa 24 hakuna hata missed call.

Nashindwa kupita mtaani, natoka ghetto asubuhi saa 12 narudi usiku sana naogopa vidole mtaani.

Bili ya umeme na maji nimekuwa mdaiwa sugu, bado Kodi ya nyumba.

Yaani mpaka nimesema, mpenzi wangu yule nilikuwa nawaletea visa vyake nae kaniacha kikatili sana.

Mungu atusaidie vijana tunapitia magumu sana!
Mkuu, pole.

Lakini bora wewe una miguu unatoka geto, kuna wengine hawana hata miguu.
 
Mpe muongozo hajui
Anatafuta kijiwe anatengeneza meza kama zile wanazouzia vipande vya kuku au matunda.
Unaanza kupika kachori na pweza zingatia eneo la movement yenye watu wengi, ndugu zako wanaopafahamu maeneo ya mazizini pale kisinia watu awalali mpaka alafajiri panakucha!

Au biashara ya matunda.

Au unatengeneza mishkaki ya 200 kwa 500 pembeni unachoma na ndizi zingatia eneo lenye movement kubwa.

Hiyo laki3 inatosha kabisa kuanzia kila kitu.
Utayari tu mkuu.
 
Kuhusu hiyo simu ya laki 3 una mshauri afanye nini?
Dah.... tenga moja la nyanya ni elfu 60 pale mabibo.... na lina nyanya 600.... akigawa mafungu ya nyanya 4 atapata mafungu 150...akauza buku kila fungu atatengeneza laki na nusu...yaani faida ya elfu 90 kila tenga.....na kama akifanikiwa kuuza matenga yote 5 kwa siku hapo unaongelea faida ya laki 4 kwa siku....na ukumbuke kesho atarudi mabibo akiwa na laki 7 mfukoni....akiamua hiyo laki ajipongeze halafu anunue matenga 10....Dah 🤣 🤣
 
Dah.... tenga moja la nyanya ni elfu 60 pale mabibo.... na lina nyanya 600.... akigawa mafungu ya nyanya 4 atapata mafungu 150...akauza buku kila fungu atatengeneza laki na nusu...yaani faida ya elfu 90 kila tenga.....na kama akifanikiwa kuuza matenga yote 5 kwa siku hapo unaongelea faida ya laki 4 kwa siku....na ukumbuke kesho atarudi mabibo akiwa na laki 7 mfukoni....akiamua hiyo laki ajipongeze halafu anunue matenga 10....Dah
Mkuu

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Hao waliokukimbia hawakuwa marafiki zako wa ukweli na kazi za watu ni ishu za kupita kwaio visikuumize kichwa. Reset akili yako anza upya, na achana na kuwafikiria watu wanakuonaje we ndo mwamuzi wa maisha yako.Watu hawana pa kula, pa kulala na hawana simu kama hiyo yako lakini wanapambana kubadilisha maisha na wanafanikiwa. Kikubwa akili mkuu matirio na pesa huja yenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom