Unaelezea nini sasa.? Mi naona huna cha maana unachoongea, unashindwa kuitetea field yako. Unaongelea kuhusu mtu wa Civil Engineering kuajiriwa serikalini hivi mara ya mwisho kwako kuona tangazo la ajira Serikalini linalotaka watu wa Civil Engineers ni lini.? Unaongelea kuhusu kilimo cha umwagiliaji, mtu wa Civil akafanye nini sasa akajenge mitaro au akachimbe bwawa.? Maana tuna wataalamu wa maji na mainjinia wa kilimo cha umwagiliaji. Upo kwenye field ya Civil ila huijui vizuri Civil wewe. Civil Engineering ni course ambayo ukisoma tegemea zaidi kujiajiri (kama kwenu familia safi na ukikidhi vigezo vya kupewa leseni), tegemea kufanya kazi za Project (kuna mradi wa kujenga jengo flani au kitu flani ukiisha basi), tegemea kufanya kazi katika makampuni binafsi ya ujenzi (ambayo hutoa ajira chache mno).