Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,350
Uswahilini maisha ya kila mtu, ni mume/mke wa nani? Anafanya kazi gani? Ana watoto wangapi? Ni kabila gani?
Nani ni mpenzi wa nani?
Huwa siyo siri.
Watataka wajue maisha yako, kama maisha yako ni ya kuunga unga. Ukipata shida hawatakuacha. Kama hawatakuwa na pesa ya kukusaidia watamtafuta Gea Habib awasaidie kuitangaza ili upate msaada.
Kama maisha yako yametulia pesa ya mboga si shida basi ishi kwa heshima. Ukienda kwenye msiba kula hata kama umewekewa sinia ushirikiane na wenzako. Usipogusa chakula inakuwa noted hiyo.
Huku kwetu kuvaliana nguo ni kitu cha kawaida. Unaweza kununua khanga na kuwapa mashost wakutolee upya.
Huku tunashirikiana kwa shida na raha. Kama huna chakula cha kuwapa watoto usishangae habari zitaenea na sahani za chakula zitaingia.