Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
Mwanakijiji umeanza kulewa sifa za wafuasi wako? Naona like a Patron/Godfather unaanza kuwalinda na kuwatetea. Haya we. Utakumbuka ushauri wangu. Yalimkuta Mwenzako Mwalimu Nyerere mpaka akawaandikia waraka wa 'Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania' wafuasi wake ambao walilewa sana 'zidumu fikra za Mwenyeketi wa Chama' mpaka wakawa viongozi waoga wa kutimiza wajibu wao wa Kikatiba wa kutetea hoja zao dhidi ya eti 'wabunge waliogeuka 'wakali kama mbogo' Bungeni. Endelea tu kulewa Amen za waumini wako. Majuto ni mjukuu. Alamsiki.
Je ni kupinge kwa sababu sitaki kukubaliana na wewe ili nionekane niwe huru kweli. Nikupinge hata kama najua unachosema ni kweli? Nikupinge alimradi tu nisije kuonekana mfuasi wako? Nikupinge ili tu na mimi niwe nakupinga? nikupinge ili niridhishe genge na kujionesha kuwa sisemi "amen" za bure tu? Au ni kupinge kwa sababu kweli sikubalini na wewe na wakati mwingine kama nakubaliana na wewe nisiogope kukuunga mkono?
Kwa sababu hadi sasa inaonekana tatizo lako haliko katika watu kunipinga ni kuwa wanakubaliana na mimi na hilo hulielewi. Ungependa watu wanaokubaliana na mimi wanipinge alimradi tu hata kama hawana sababu, unachopendekeza kufanya ni kuwa dhaifu.
Watu wengi wanaokubaliana na mimi nawaamini kwa uhuru wao wa mawazo kuliko wale wanaopingana na mimi. Ndiyo maana binafsi sioni kazi kukubaliana na watu kama kina FMES, Mtanzania, Rev. Kishoka Zakumi au mtu mwingine yoyote ambaye hoja yake ninaikubali. Jaribu kunishawishi uonie kama sitokubaliana na wewe.
Ukija kwa Mwalimu na hoja ambayo hujaijenga vizuri usishangae akakuonesha upuuzi wa hoja hiyo na ukabakia kulalamika "haambiliki". Leo hii ninaelewa sana kwanini ilikuwa vigumu kumshawishi Nyerere, maana watoa hoja wa wakati ule ndio hawa wanatoa hoja leo na tunavyozivunja vunja hapa wakati mwingine ni burudani tosha.