Maisha ya ujana ya akina Ulimwengu, Shivji.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya ujana ya akina Ulimwengu, Shivji..

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Sumaku, May 19, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  May 19, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maisha ya ujana ya Jenerali Ulimwengu, Shivji, Museveni, Sitta na wengineo UDSM

  16 May 2009

  Na Born Again Pagan

  Makala haya kwanza yaliandikwa kwenye “Kijiji” chetu (mjengwablogspot.com) mwezi Mei, 2007, chini ya kichwa cha habari, “BAP Anavyomwelezea Yoweri Museveni”. Madhumuni yake yalikidhi ombi la “Mwenyekiti wa Kijiji” kunitaka nitoe maelezo kidogo juu ya wanafunzi wenzangu Darasa la 1970 hapo Mlimani: Yoweri Kaguta Museveni na Hirji.
  Nilianza kwa kutoa hoja kwamba haiwezekani kabisa kuweza kusimulia ya Yoweri Kaguta Museveni na Hirji bila kutoa, pengine, “background” ya miaka kumi ya kuanzia 1960 na jinsi matukio hayo yalivyojenga mikitadha iliyozalisha wanafunzi wenye msimamo mkali, kama akina Yoweri Kaguta Museveni na Hirji.

  Katika makala haya yaliyohaririwa na kuongezea maelezo zaidi (pamoja na kubadili kichwa chake), ninagusia baadhi ya matukio ya miaka hiyo, na jinsi yaliyochangia katika kuivisha maisha ya ujana wa akina Yoweri Kaguta Museveni (Uganda), Hirji, Issa Shivji (Tanzania) pamoja na wengineo wengi waliomaliza hapo Mlimani mwaka 1970, kwa mfano:

  Souma (Guinea), Archibord Kapote Mwakasungura (Malawi), John Garang (marehemu) wa Sudani, Salim Msoma, Issa Shivji, Nimrod Mkono, Moses Maira (marehemu), Ali Mchumo, James Kateka, Augustine Mahiga, Adamu Marwa, Pius Ngw’andu, Crispin Hauli, (marehemu), Abdallah Ngororo (marehemu), Patrick Qorro, Jenerali Ulimwengu, na wengine wengi sana, kama mimi.

  Vile vile, makala haya yanachangia juu ya hali hapo Mlimani miaka yetu ya 1966-1970; mkwaruzano baina ya vyama vya wanafunzi vya USARF/TYL na USU kuhusu suala la “Rag Day”; umoja wa USARF na TYL; makala yanamtoa Hirji kando kidogo na kuzingatia tu ya Yoweri Kaguta Museveni (kwa makusudi); na mwisho, mgomo wa Jumamosi, 22 Oktoba, 1966.

  Sisemi kuwa hao waliomaliza mwaka 1970 hapo Mlimani ndio tu maisha yao ya ujana yaliiva na kuwa na msimamo mkali. La hasha! Wengine walikuwa hawana msimamo huo! Na walikuwepo wengine nyuma yetu wenye msimamo mkali, pia, ikiwa ni pamoja na hao waliotutangulia. Ila nawataja hao wa mwaka 1970 kwa sababu ndio lilikuwa darasa letu.

  Matukio ya Miaka Kumi Kuanzia 1960
  Tumetoka mbali; tunakwenda mbali, pia. Kati yetu (wewe na mimi) huko tuendako hakuna aliyewahi kupafikia, ingawa tunapanga kuwasili huko. Miaka kumi ya kuanzia 1960 ilikuwa ya matukio mengi na mikakati mingi, ki-ulimwengu na ki-taifa (Tanzania). Ufuatao ni mtiririko wa matukio na mikakati hiyo; lakini si ki-miaka (chronology).

  Moja, misukosuko ya ki-mataifa ya miaka ya kuanzia 1960 ilikuwa ni kupanuka kwa itikadi eti ya u-Komunisti. Kudhibiti kupanuka kwa u-Komunisti duniani kuliongozwa na Amerika ikisaidiana na Nchi za Magharibi, mithili ya hadithi ya kuweka kifuniko jini lisitoke kabisa ndani ya chupa!

  Nchi hizi ziliuona u-Komunisti kuwa ni utamaduni uliowania kuua ule wa ki-Bepari. Michakato hiyo ikazua, eti, Vita Baridi! Amerika ilikania kudhibiti (to contain) kupanuka kwa u-Komunisti huko Asia ya Mashariki ya Mbali, Amerika ikawania kuishambulia Vietnam.

  Mbili, kutamalaki kwa udugu baina ya Afrika na U-Rusi na kufungua Chuo Kikuuu cha Lumumba Friendship kilichochukua wanafunzi wengi wa-Afrika. Sambamba na hilo, kupanuka kwa Vita Baridi kuliingilia mstakabali wa Bara la Afrika. Ugomvi wa Ulaya ukaletwa kwetu Afrika.

  Tatu, kuuawa kwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo Emergy Patrice Lumumba kutokana na njama za serikali ya Amerika kupitia Shirika la Ujasusi la CIA na serikali ya Ubelgiji zikishirikiana na vibaraka wa ndani chini ya Joseph Désire Mobutu na Moisé Kapenda Tshombe wa Jimbo la Katanga lililotaka kujitenga! Amerika na Ubelgiji hawakupenda kuiona Kongo inakuwa ya ki-Komunisti, na, pengine, kuambukiza sehemu nyinginezo za Afrika, hasa Afrika Kusini.

  Nne, mchakato wa Afrika kutaka kujitawala ulijikita katika ndoto ya Umajumuhi (Pan-Africanism) ya wasomi waliobobea wakishirikiana na wenzao wa Amerika na Karibe au niseme wenzao wa Diaspora. Hawa waliweza kuunda mtandao wao vizuri kuliko kuunda mtandao na walalahoi wa chini (grassroots). Pengine hapa ndipo kuna kitovu cha kuyumba kwa uongozi katika nchi zetu za ki-Afrika!

  Umajumuhi (Pan-Africanism) ukabaki ni ndoto tu hadi leo kutokana na wa-Koloni kuweka vikwazo kuwa kwa waasisi wetu kuwa na u-haki wa kudai uhuru, iliwabidi kuthibitisha kuwa walikuwa ni wasemaji wa walalahoi. Hii iliuleta mchakato wa kupigania uhuru kwa uwanja wa nyumbani, k-taifa na sio ki-Bara la Afrika.

  Nchi nyingi zilianza “kuruka juu na kujulikana”, kama majimbi kutoka majivu-moto (popcorns)! Na sisi tukawamo katika mchakato huo.

  Tano, ingawa Umajumuhi (Pan-Africanism) ulishindwa kulikomboa Bara la Afrika kwa mkupuo (wholesale), waasisi wetu hawakukata tama ya Umajimuhi. Wengine walionelea kuwa Afrika ingeweza kukidhi lengo hilo kwa kuungana rejareja (piecemeal): wakaunda, kwa mfano, Umajumuhi-kipande, Pan-African Movement for East and Central Africa (PAFMECA).

  Kiongozi wetu aliahidi kuchelewesha uhuru wa nchi yetu kwa kuzingoja nchi nyingine tatu za ujirani mwema (Kenya, Uganda na Zanzibar). Lakini wapi! Ilibidi nchi za Afrika zijitawale, reja reja. Leo zinalilia kuunda Afrika moja!
  Sita, kwa Tanzania Bara, chini ya siku kama 1000 hivi, Waziri Mkuu Julius Nyerere alitangaza kujiuzulu. Sababu: Kuimarisha TANU. Ilimbidi aende kwa wananchi tena kupata kibali cha kuongoza mstakabali wa taifa la Tanganyika changa.

  Lakini kuna pia ukweli kwamba Waziri Mkuu Nyerere alifanya hivyo ili kuepusha kura ya maoni ya wa-Bunge machachari, ambayo karibu ilikuwa impe “a vote of no confidence” kutokana na kupingwa kwa baadhi ya sera (za Chama Tawala na Serikali yake) kuhusu suala la uraia katika mikitadha ya Umajimuhi (Pan-Africanism), kwa ujumla, na Tanganyika, hasa. Nyerere alionekana ‘a statesman” kwa kunusuru maafa yaliyokining’inia usoni mwa nchi yetu changa!

  Mtafaruki wa namna hiyo ulikikumba chama cha TANU kwenye mkutano wake wa Tabora kutoka Januari 25-28, 1958 na kuzalisha chama cha upinzani cha African National Congress, chini ya Zuberi A. Mtemvu.

  Wa-Bunge machachari wa wakati huo, kwa mfano, Mheshimiwa M-Bunge Richard Wambura (East Lake Province - leo Mkoa wa Mara) alidiriki hata kutamka kauli kama hii: Endapo umeshindwa kuongoza, tuachie sisi tuongoze/waachie wengine waongoze. (Rejea Hansard ya mwezi huo ambao Nyerere alipojiuzulu).

  Wa-Bunge machachari walihoji, kwa jina la Umajimuhi: Kwa nini ilikuwa ni rahisi kwa wa-Ulaya (hasa wa-Uingereza) na wa-Asia waliokuwa na uraia wa Uingereza) kuweza kuwa raia wa Tanganyika kuliko wa-Nigeria au wa-Ghana, kwa kifupi wa-Afrika wa kutoka nchi nyingine za Afrika?
  Zaidi, wa-Bunge walilileta nyumbani suala la uraia na kuuliza kwa nini spidi ya Afrikanaizesheni (kutoa hatamu za uongozi wa ngazi mbalimbali kwa wazalendo wa-Matumbi) zilikuwa za mwendo wa “mzee kobe”?

  Saba, suala la Afrikanizesheni lilijikita ki-jeshi: Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi (Tanganyika Rifles). Hatimaye, likachukua mkakati mwingine na kusababisha uasi wa Jeshi la Ulinzi uliozimwa kwa msaada wa aliyekuwa m-Koloni wetu (Jeshi la Uingereza), baada ya Rais na Makamu wake kujificha kwa siku kama tatu hivi.

  Nane, baada ya kuzimwa uasi huo na Rais kutoka majifichoni, yalifuatia mambo kadhaa, ki-Katiba. Kwa mfano, Katiba ilibadilishwa; kufutwa kwa Vyama vya Wafanyakazi na kuundwa kwa NUTA; migomo kupigwa marufuku; sheria ya Kuweka Watu Kizuizini Preventive Detention Act); na matayarisho ya chini chini ya Tanzania kuwa ni ya chama kimoja. Mabadiliko hayo yalimpa Rais madaraka mengi kiasi cha Rais Nyerere kutamka kwamba angeweza kuwa dikteta, kama angependa!

  Tisa, mtazamo mpya wa Amerika kuhusu hali ya ki-siasa Zanzibar, ambako kulikuwa na kituo chake cha mambo ya anga za juu (satellite surveillance station). Yasemekana baadhi ya wa-Zanzibari walikuwa na msimamo wa mkono wa kushoto uliotishia, eti, maslahi ya Amerika.

  Hii ilitokana hao kuhusiana ki-ukaribu sana na Kwame Nkrumah (Ghana), Abdel Gamal Nasser (Misri), u-Rusi, u-China na Kuba.

  Kumi, Muungano wa Tanzania. Kuna wenye kuamini kuwa Nchi za Magharibi ziliogopa kuiona Zanzibar ikiselea kuelekea eti, u-Komunisti, hasa kufuatia mapinduzi yaliyong’oa utawala wa ki-Sultani. Hawakutaka kuona Zanzibar inakuwa “Kuba” ya Afrika.

  Tanzania Bara (Tanganyika) ilikuwa chini ya Julius Nyerere. Na Nchi za Magharibi zilimfikiria kuwa ni mpinga u-Komunisti (our man in Dear es Salaam). Hata yeye Julius Nyerere (m-Katoliki) aliwahi kutamka kuwa si m-Komunisti kwa sababu ma-Komunisti hawamwamini Mungu!

  Nyerere alikuwa m-Majimuhi (Pan-Africanist). Kwahiyo, eti, Nchi za Magharibi zilimtumia Mwalimu Nyerere (m-Majimuhi) kuinasua Zanzibar na kuunda Muungano, kulingana na lengo la mikitadha ya Umajimuhi.

  Na kwamba hata Sultani wa Zanzibar alipopinduliwa, aliishi katika meli yake kwa muda wa karibu siku tatu nje ya Dar es Salaam kabla ya kukimbilia Uingereza.

  Kumi na moja, kutamalaki kwa udugu baina ya Afrika na Nchi za Asia (Afro-Asian Solidality) na pia kukua kwa uhusiano baina ya nchi huru za ki-Afrika na nchi za Mashariki ya Kati (Pan-Arabism, chini ya Abdel Gamal Nasser).

  Kumi na mbili, Kumi na mbili, kuzaliwa wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), chini ya katibu Mkuu Diallo Teli wa Guinea.

  Kumi na tatu, kutamalaki kwa umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote wa Vita Baridi. Lakini nchi zetu zikajikuta zinavutana kati ya itikadi ya Nchi za Magharib, kwa upande mmoja, na u-Rusi/u-China, kwa upande mwingine.

  Afrika ikajigawa katika makundi mawili:
  Casablanca Group - nchi zenye msimamo mkali wa kukataa misaada na kutegemea wengine: Algeria, Misri, Ghana, Guinea, Libya, Mali na Moroko.
  Brazzaville Group (zenye kupenda ujamaa wa ki-Afrika pamoja na zisizo na msimamo mkali): Ethiopia, Liberia, Nigeria, Sierra Leone, Somalia, Togo, Tunisia na Congo (Kinshasa, kwa upande wa pili. Kundi hili lisilo na msiamamo mkali lilibadilika kutoka Brazzavuile Group na kuwa Monrovia Group.

  Kugawanyika kwa vyama vya wafanyakazi kati vile vyenye msimamo mkali: All-African Trade Union Federation (AATUF) kilichobadilika na kuwa Organisation of African Trade Union Unity (OATUU), kwa upande mmoja, na All Africa Free Trade Unions (AAFTU), kwa upande mwingine.

  Itaendelea wiki ijayo:

  Barua pepe: romuinja@yahoo.com

  Chanzo: kwanzajamii.com
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Inataka muda wa kutosha kusoma...Ukiisoma kwa kulipia kwenye `cafe` ndo imekula kwako.

  Lete hiyo dozi iliyobaki...!
   
 3. S

  Sumaku Member

  #3
  May 26, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Born Again Pagan

  KATIKA makala yaliyopita, tuliendelea na matukio mengine yaliyochangia kikamilifu katika kujenga muktadha wa msimamo mkali wa baadhi ya vijana waliokuwa wakisoma hapo Mlimani mwaka 1966 hadi 1970, kama akina Issa Shivji na Yoweri Kaguta Museveni, na wengineo.

  Tumeishaona matukio kumi na tatu yaliyochangia kidogo kidogo katika kujenga muktadha wa msimamo mkali wa baadhi ya vijana waliokisoma hapo Mlimani miaka ya 1966 – 1970. Hili ni kundi ninalolifahamu vizuri – wanafunzi wa mwaka wangu. Kwa kutamka hivyo, ningependa kumweka kando kidogo Samwel Sitta, ambaye alimaliza hapo Mlimani mwaka 1967 – kundi langu tukiwa mwaka wa kwanza.

  Wanafunzi wa mwaka wangu wa kwanza walikuwa ni wengi, karibu mara mbili. Ukubwa huo ulitokana na kufukuzwa na kurudishwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza (1966).

  Makala yaliwatambua baadhi tu ya hao vijana, kwa mfano, Souma (Guinea), Yoweri Kaguta Museveni (Uganda), Archibord Kapote Mwakasungura (Malawi), na John Garang (marehemu) wa Sudani. Vijana wa-Tanzania walikuwa, kwa mfano, Salim Msoma, Issa Shivji, Henry Mapolu, Brendire Moronda (marehemu), Andrew Shija, Ali Mchumo, Adamu Marwa, Pius Ngw’andu, Saida Yahya, Crispin Hauli, (marehemu), Abdallah Ngororo (marehemu), Patrick Qorro, Jenerali Ulimwengu, na wengine wengi sana, kama mimi.

  Ishirini na nne, wakati ya ujamaa yalipotamalaki, Mlimani kikawapokea wageni wengi kutoka serikali za Tanzania na vyama vyao vya TANU/Afro-Shirazi,. Kwa mfano, Rais Abed Karume alikuja kuimarisha umoja wa vijana wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa mwaliko rasmi kwa wana-TYLtawi la Mlimani kuitembelea Zanzibar.

  Wengine walikuwa ni akina ma-Bwana Benjamin William Mkapa, Kingunge Ngombale-Mwiru na G. Mapunda (marehemu) na walimu wengine kutoka Chuo cha TANU cha Kivukoni wakawa “ma-Profesa” wetu wa Ujamaa. “Ma-Profesa” wetu hao walisaidiana na ma-Profesa wa Idara ya Mafunzo ya Maendeleo (Department of Development Studies) kutupanua mawazo yetu (kutupiga msasa) tuachane na tabia za u-Koloni mkongwe na u-Koloni Mamboleo (neo-Colonialism) na kutuhimiza tuwe wazalendo kwa Tanzania, Afrika na nchi nyinginezo zilizokiendelea.

  Namkumbuka Bwana Benjamin W. Mkapa alivyotueleza kwa ufasaha juu ya “juche” (siasa ya kujitegemea) ya Korea Kasikazini. Tulimsikiliza kwa makini; tuliyatafukari namna ya kuyatekeleza hayo ya “juche” nchini Tanzania katika muktadha wa Ujamaa. Pengine, hakuna nchi masikini isiyotembeza bakuli duniani, kama nchi ya Korea Kasikazini!

  Wengine sisi tulimfahamu Bwana Benjamin Mkapa kabla ya kuja Mlimani. Tulimfahamu kama Mhariri wa gazeti la ki-Uingereza la Chama The Nationalist, pamoja na msimamo mkali wa gazeti hilo katika ukombozi wa Afrika. Kwahiyo, kumwona akija hapo Mlimani kulitufanya tutege masikio yetu kumsikiliza akiongea kwa ki-Uingereza, lugha aliyoimudu!

  Kutoka kwa ma-Bwana Benjamin William Mkapa, Kingunge Ngombale-Mwiru na G. Mapunda (marehemu), tulizidi kuufahamu u-Bepari ukifananishwa mithili ya unyonyaji wa kupe au mithili ya u-nyama!

  Leo hii, tukimsikia mstaafu Rais wetu Bwana Benjamin Mkapa akishutumia kwamba alifanya biashara akiwa Ikulu, na kwamba awamu yake iliuza vya Tanzania alivyopigania kuvitaifisha, tunashangaa sana!

  Leo hii unyonyaji na u-nyama huo kwa ma-Bwana Benjamin William Mkapa na Kingunge Ngombale-Mwiru vinaonekana kuwa ni nyenzo mbadala ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo badala ya watu, aridhi, siasa safi na uongozi mwema!

  Tunaaswa na mbobeaji Profesa Ali Al’Amin Mazrui kuwa Mwalimu Nyerere, na Ujamaa wake, alilisahau hili la wajibu wa u-binafsi katika kuzalisha maendeleo! Na kwa kulisahau, Rais wetu mstaafu Hassan Mwinyi (Mzee Ruksa) anatuasa kuwa Ujamaa, pamoja na uzuri wake, ni “ndoto” tu!

  Ma-Bwana Benjamin Mkapa na Kingunge Ngombale-Mwiru wameungana na ma-Bepari! Wanakula sahani moja na hao hao ma-nyang’au! Je, tuwaelewaje? Je, walikuwa wakitudanganya! Je, wanaona soni? Je, huu si unafiki wa bendera fuata upepo? Je, ni ubeuzi tu? Je, wameona mwanga wowote?

  ishirini na tano, uongozi na udamisi (joviality) wa Mwalimu Nyerere: Mwalimu Nyerere naye alikipenda Chuo Kikuu Mlimani! Alikuwa “a regular visitor”, kulingana na maneno ya Mkuu wa Chuo Dr. Wilbert Kumalija Chagula. Kuna wakati alitumia kama juma moja hivi hapo Mlimani tukifundishana ya Ujamaa (A Teach-in Week on Socialism). Lakini akina Mwinyi-Mkapa-Kikwete wanawasaga tu bila kuwafundisha wananchi ya u-Bepari wauelewe!

  Akina Mwinyi-Mkapa-Kikwete wanawaambia wananchi ni lazima wafuate utadawazi wa soko huria kwa sababu kila nchi inuafuata, mithili ya ngoma ya mdundiko! Hii si kweli. Utandawazi ni sera za vyama tawala na serikali zao za mkono wa kulia, hasa wakati wa Reaganomics-Thatcherism na mabaki yake.

  Kuyumba kwa uchumi wa dunia leo hii kumeyafanya hayo ya Reaganomics-Thatcherism kupitwa na wakati, penda, tusipende! Kuyumba kwa uchumi kunarudisha pole pole ya vyama na serikali za mkono wa kushoto,panda, tusipende!

  Wakati mwingine Mwalimu Nyerere alipendelea kuwaleta wageni wa taifa hapo Mlimani kukutana na jamii ya Chuo Kikuu na kubadilishana mawazo, kwa mfano, Rais Josip Tito wa Yugoslavia na Indira Gandhi wa India.

  Mwalimu alivutwa na wanafunzi wa Mlimani. Lakini alivutwa zaidi na wana-TYL, Tawi la Mlimani. Alipokuwa na nafasi, hakusita kuwakaribisha alasiri Jumapili wana-TYL nyumbani kwake Msasani kwa vinywaji (bia na soda) na korosho za kukaangwa ili kubadilishana mawazo.

  Nakumbuka siku moja alitukaribisha kwa mazungumzo. Walikuwepo wasaidizi wake: Paul Sozigwa, Joseph Butiku, Philemon Mgaya na wengineo. Mkutano ulianza kwa ukimya. Mara Mwalimu aliamuru tuletewe vinywaji kwa kuamuru, “Waleteeni vijana wangu vinywaji. Najua wakinywa bia moja au mbili wataanza kuzungumza. Wewe unakunywa nini? Na wewe?”

  Vijana walioulizwa walikuwa wameketi karibu naye. Lakini sijui kwa kuogopa, waliomba soda. Mwalimu alishangaa na kuendelea, “Mwenye kutaka kunywa bia asiogope, ‘feel at home’.

  Mwalimu alikoshwa sana na baadhi ya michango kutoka kwa kundi letu. Akiwa amejawa na furaha, huku naye ameshikilia glasi kubwa ya bia na kutafuna korosho, Mwalimu alitamka maneno yafuatayo (si neno kwa neno – verbatim - ila maneno haya yapo karibu karibu sana na yale aliyotamka):

  Vijana, nimesikia sifa zenu! Wakati mwingine mnaacha kumalizia “homework” zenu alasiri za Jumatano zisizo na madarasa mkisaidia wananchi katika kisomo cha watu wazima na kuokota korosho hapo Mlimani kutunisha mfuko wa Tawi lenu. Na wakati mwingine nasikia kwamba mnaacha raha za wikiendi. Mnakwenda huko Ruvu kuvuna mpunga na kutoa misaada mingineyo kwa wanavijiji huko Bagamoyo! Mnawakumbuka wanyonge!

  Mwalimu Nyerere alisita kidogo kabla ya kuongezea:

  Vijana, mnafanya kazi hizi za kujitolea hata kuwashinda viongozi wangu. Lau kama viongozi wangu wanaonisaidia wangekuwa na nia na moyo, kama ninyi, nchi yetu ingekuwa mbali katika maendeleo yake!

  Huku tukipiga makofi, tuliguswa sana na tamko hilo la Mwalimu. Lakini kusoma furaha zetu na makofi tuliyopiga, mara Mwalimu alitoa changamoto kali:

  Ninyi vijana ni ‘progressive’. Lakini cha kunishangaza ni kwamba mnapomaliza miaka ya ujana wenu na masomo yenu, mnabadilika; mnakuwa ma-‘reactionary, per excellence!”

  Hakuna hata mmoja wetu aliyediriki kutoa mchango mchango kujibu hiyo hoja na changamoto ya Mwalimu Nyerere!

  Labda, hiyo kauli ya Mwalimu Nyerere ilikuwa na utabiri unaoweza kujibu kidogo baadhi ya kero za msomaji Rugeiyamu Kahwa, kuhusu vijana akina Yoweri Kaguta Museveni na Issa Shivji wa zamani na sasa.

  Ishirini na sita, matembezi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Chou-en-Lai wa u-China katika baadhi ya nchi za Afrika: Ziara hiyo ilileta mafua na kukuna vichwa kwa wivu kwa Nchi za Magharibi, kufuatia kauli yake, “Africa is Ready for Revolution” (Afrika Imeiva Tayari kwa Mapinduzi). Nchi hizo zilijiami kwa mbinu za kulinda eti maslahi yao katika Bara la Afrika.

  Ishirini na saba, zikiongozwa na Amerika, Ufaransa na Uingereza katika kulinda maslahi yao, serikali za Nchi za Magharibi zilianza zilizidisha mikakati yake ya kuzisetri tawala za kibaguzi za wa-Ulaya walowezi wachache na wabaguzi huko kusini mwa Afrika Kusini (Rhodesia, Msumbiji, Afrika Kusini, South West Africa/Namibia na Angola).

  Ishirini na nane, nchi moja kati ya tawala za kibaguzi za wa-Ulaya walowezi wachache na wabaguzi huko kusini mwa Afrika, Rhodesia, ikawa ni “mtoto mbaya”, kwa Uingereza na muasi kwa Afrika. Utawala wake, chini ya kiongozi wao, haini Ian Smith, ulijitangazia uhuru wa mabavu (Unilateral Decralation of Independence - UDI) na kuendelea kuwatesa ndugu zetu zaidi.

  Uingereza iliendelea na msimamo wake wa NIBMAR (No Independence Before Majority African Rule). Lakini wananchi vibaraka wa humo nchini na chama chao cha United African National Council (UANC) cha Bishop Abel Tendekayi Muzorewa, kwa kushirikiana na mhaini Ian Smith, waliunda serikali ya muda Rhodesia/Zimbabwe, chini ya Waziri Mkuu Bishop Abel Muzorewa. Serikali hiyo ililaani vita ya ukombozi.

  Afrika ilikataa kuitambua serikali hiyo na ilizingatia kuwa Rhodesia lilikuwa bado ni koloni la m-Uingereza. Kwahiyo, jukumu la kuikomboa lilikuwa chini ya uwezo wa Uingereza. Ma-Profesa wengine wa Rhodesia, wenye asili ya Ulaya, walikimbia na kujisetri nchini kwetu wakifundisha hapo Mlimani: Terrence Ranger, John Illife na John Mcracken (Historia) na Roger Woods (Sosiolojia).

  Ishirini na tisa, mtafaruki baina ya Ma-Rais Kwame Nkrumah na Julius Nyerere: Wote wawili walikuwa na malengo sawa ya ukombozi na umoja wa Afrika. Lakini kidogo walihitilafiana katika mbinu za kufikia ukombozi na umoja huo.

  Rais Kwame Nkrumah alipendelea Afrika ijikomboe kwa mkupuo ili kuleta umoja huo mara moja. Zaidi, alitaka Ghana iongoze katika ukombozi wa kumaliza u-Koloni, kama ilivyoongoza katika kuanza kuutoa na kuleta uhuru.

  Rais Julius Nyerere alipendelea Afrika ifikie umoja wake kwa rejareja, au ki-makundi. Zaidi, alitaka mojawapo ya nchi huru zilizokuwa karibu ya kusini mwa Afrika ndio ishike hatamu za ukombozi.

  Dar es Salaam ilishinda hilo la wapi yawe makao makuu ya African Liberation Committee (Kamati ya Ukombozi).

  Makala yajayo yatamalizia matukio haya.
  Barua pepe romuinja@yahoo.com

  CHANZO: kwanzajamii.com
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,814
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 180
  Kwi kwi kwi. Yaani rais anakwenda University kufundishana ujamaa (utopia) na wanafunzi.

  Ndio maana tume-lost.
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  May 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zateni kumbe umejificha huku! Kama kawaida yako where Mwalimu is mentioned there u shall be. Rais alikuwa anaenda kujadiliana nao vichwa vyenzake - kama Obama alivyoenda University of Notre Dame majuzi!
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Companero,
  Hivi viongozi wa leo wakienda chuo kikuu wataenda kusema nini?
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  May 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wa Afrika au Tanzania? Wa Afrika washaenda - mf. Mbeki na Museveni. Wa Tanzania yupo mmoja aliwabeba wanafunzi kwenye mabasi kutoka Chuo wakaenda kuwahutubiwa naye kwenye mkutano wa Chama! Nadhani huko waliongelea namna ya kujiunga na kukijenga Chama ili kidumu daima!
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 26, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Oh yeah....ujamaa?
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  May 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ujamaa what au unasubiri Mwanakijiji aje kuungelea uitikie Amen?
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,814
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 180
  Hizo zilikuwa classic primitive nonsense za viongozi wa Africa. Mnakwenda kufundishana ujamaa.

  Niambie ni nani waliokuwemo kwenye hiyo mijadala ambaye ameweza kuinvest hata kwenye shamba la mchicha.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  May 26, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Yeah..kwani kaenda wapi? sijamwona hapa muda mrefu
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  May 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  komredi, you are better than this! grrrrrr
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  ndio maana mkuu mie sipendi paste za BAK awe aanchukua main points tu.......mtu anakopi mapage yoote na kuyabwaga......800 nusu saa jamani cafe
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  May 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  All this is because you don't rebuke/denounce your followers. Tell them categorically to think and argue for themselves. Here is an interesting thread, we can't afford to mess it up with rhetorical questions aimed at provoking debates that will reinfornce hero worshipping. Tell your clones to be real and engage the text in hand from BAP without resorting to your aid! Let the debate continue.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  May 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  that is beyond ridiculous! in all three allegations;
  still ridiculous! according to you if they(whatever that means) don't agree with me that means they are thinking for themselves but when they do agree then they don't? still a massively flawed reasoning. If I were to agree with you to "rebuke" the so called "followers" what does that say about my relationship with you, especially by agreeing with you. According to your reasoning, if I were to oppose your assertion then I'm independent but if I agree I become your follower? Doesn't that very act negate whatever argument you are holding against those who agree with me?

  you can never have a candid debate with someone who calls you names, reduce you to rubbish and try so hard to injure your character. In any debate you will have people who agree with you, and have reached such an agreement because you convinced them. That does not make them 'clones' or whatever else you have in your mind.

  Only arguments, properly formed and clearly made can convince people. Calling people names as you are doing now does not help in the exchange of ideas in a public square.

  If you believe by going against me or opposing me qualifies a person of being independent then you are totally mistaken. But if that makes you feel independent because you don't agree with me then independent you are! but are you?

  On the other hand however, what if I'm the one agreeing with them more than they agree with me? am I then the follower of many!?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  May 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Ahem...ahem...ahem! You rock dude!
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  May 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Preach on brother..preach on...
   
 18. Companero

  Companero Platinum Member

  #18
  May 27, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji umeanza kulewa sifa za wafuasi wako? Naona like a Patron/Godfather unaanza kuwalinda na kuwatetea. Haya we. Utakumbuka ushauri wangu. Yalimkuta Mwenzako Mwalimu Nyerere mpaka akawaandikia waraka wa 'Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania' wafuasi wake ambao walilewa sana 'zidumu fikra za Mwenyeketi wa Chama' mpaka wakawa viongozi waoga wa kutimiza wajibu wao wa Kikatiba wa kutetea hoja zao dhidi ya eti 'wabunge waliogeuka 'wakali kama mbogo' Bungeni. Endelea tu kulewa Amen za waumini wako. Majuto ni mjukuu. Alamsiki.
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  May 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Wewe bana huna hoja hapa. Ni wangapi wanakubaliana na wewe hapa? Je hao ni wafuasi wako? Na ni wangapi wewe unakubaliana nao hapa na kwingineko? Ina maana wewe ni mfuasi wao? Hebu acha vioja bana la sivyo una come across kama vile una ajenda nyingine. Inaniwia vigumu kuamini kama kweli wewe unaamini hata hayo unayoyasema mwenyewe. Nasukumwa kuamini unasema tu just for the hell of it...
   
 20. Companero

  Companero Platinum Member

  #20
  May 27, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  You've got a point. Nimekubali hoja YENU (Au ni YAKO?). Sina la ziada. Usiku mwema.
   
Loading...