Maisha ya Ubachelor sometime yanachosha

Maisha ya Ubachelor sometime yanachosha

Nilipika uji wa ulezi usiku, asubuhi nikaenda gym narudi nataka tena nipike uji.

Akili inaniambia, sasa hii sufuria jana si umepikia uji? Na sasa hivi si utapikia uji? Sasa uioshe ya kazi gani?

Kilichofuatia ITV .......
Kazi zote nitafanya lakini kuosha vyombo tu, hapo ndio ugonjwa ulipo.
Ikitokea nimepata mgeni alafu niko na mood ya kupika, natoa tahadhari kabisa kwamba baada ya msosi kila moja aoshe vyombo alivyotumia
 
Daah kuna siku nimerudi geto sa kumi na moja jioni nimechoka kinoma halafu vyombo vichafu nikasema ngoja nijilaze kidogo walau kanusu saa. Kilichotokea nimeshtuka saa sita usiku mvua inanyesha sasa hapo ndio naisikia njaa yenyewe na usingizi sina.

Nilichukua sufuria la kuchemshia maji nikachemsha chai nikala na parachichi. Maana usiku kuanza kuhangaika na mavyombo jau sana. Hapo ndio nikatambua umuhimu wa mke aseeh
 
Back
Top Bottom