Ifike mahali watu wa ustawi wa jamii waanze kutoa elimu kwa uma juu ya mahusiano ya ndoa, maana inapokuja kuachana licha ya dini za kila mmoja kabla ya kufika kuchukua talaka mahakamani lazima muanzie ofisi za ustawi wa jamii.
Tangu watoto waelimishwa kwanini uingie kwenye ndoa na ukiingia ujue hiki na hiki na hiki ukitarajie na hiki na hiki unaweza usikipate na hakuna kufanana na kadhalika na kadhalika. Yaani iwe suala la kujiandaa kisaikolojia zaidi ili wanaokataa ndoa waikatae tangu wadogo.
Sio waingie kichwa kichwa halafu baada ya miezi, mwaka au miaka kadhaa wanasema ndoa haina maana.Siwalaumu maana sijui wanayokutana nayo huko, sina uzoefu ila ni swali la kujiuliza, kwanini uingie kwenye ndoa? na uingie na nani?....
Walioko kwenye ndoa pia wana jukumu kubwa kuwaelimisha uzao wao kuhusu masuala haya haswa kipindi hiki cha utandawazi.