Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,281
Huku kwetu sabuni ya kufulia unapimiwa kwenye kikombe cha chai kama huwezi kununua ndoo au box zima. Vile vitenge vitatu vinavyouzwa Karume na Mnazi Mmoja huku vinauzwa kipande kimoja. Ukiweza kununua vyote vitatu sawa, ukiweza viwili sawa ukishindwa kabisa unanunua kipande kimoja.
Kuku unanunua robo au nusu kutokana na pesa yako. Ukijiwa na wageni unanunua mchicha na robo kuku unapika na wali wa nazi, kuku ni wa mgeni huku jikoni mwenyewe unamalizia mchuzi kidogo wa kukombea sufuria na mchicha. Mgeni akiomba kuongezewa mboga anaharibu kabisa.
Tulichoshindwa na bado tunakifanyia utafiti ni jinsi ya kuuza tube ya dawa ya meno rejareja. Tukifanikiwa hili tutakua na PhD ya uchumi japo haitalingana na ya Dr Mwigulu Nchemba.