Maisha ya Hostel siku za Mwanzo Chuo kikuu

Preta siku hizi simuoni oni humu ndani. Naye keshaenda kuhiji nini? Mnasafiri kwenda wapi kama tayar uko Rombo? Au unaelekea moshi mjini?

Hujaona ile thread ya sisi wana JF tikiongozwa na mwenye nyumba wetu Maxence tunaelekea mbuga za wanyama tarehe 27?
 
Ebwana eeeeee huwenda siku tukikutana kwenye Party ya JF patakuwa hapatoshi. Huenda tumepishana sana tu kwenye makorido ya chuo bwana.

Ndugu yangu paulo hiyo Party kama itakuwepo mi naona itakuwa balaa maana Humu ndani mtu anajiita Rural Swagga unakuta ni baba yako mdogo,Kwa ufupi mimi sintakwenda kwanza nahisi kutakuwa na mashushu wakutosha 2
 
Hujaona ile thread ya sisi wana JF tikiongozwa na mwenye nyumba wetu Maxence tunaelekea mbuga za wanyama tarehe 27?

Cjaiona mkuu hebu nipe link yake. Leo nimekuwa busy kweli kazini hata JF sijaivinjari vzr leo.
 
Ndugu yangu paulo hiyo Party kama itakuwepo mi naona itakuwa balaa maana Humu ndani mtu anajiita Rural Swagga unakuta ni baba yako mdogo,Kwa ufupi mimi sintakwenda kwanza nahisi kutakuwa na mashushu wakutosha 2

Mashushu my foot mbona wa TZ tu waoga hivi hao mashushu watakufanya nini? kazi yao si kuilinda serikali iliyoko madarakani wewe watakusumbua kwa lipi? yaani nakerekaga na mashushu ma fufu arghhhhhhh
 
Ndugu yangu paulo hiyo Party kama itakuwepo mi naona itakuwa balaa maana Humu ndani mtu anajiita Rural Swagga unakuta ni baba yako mdogo,Kwa ufupi mimi sintakwenda kwanza nahisi kutakuwa na mashushu wakutosha 2

Acha tu Mkuu. Mi nadhani nitaomba udhuru nisihudhurie kwani inaelekea kati ya kipindi cha 2001/2002 hadi 2004/2005 tumekutana kwa sana tu kwenye mikorido ama hata darasa moja tukiwa chuo.
 
Cjaiona mkuu hebu nipe link yake. Leo nimekuwa busy kweli kazini hata JF sijaivinjari vzr leo.

quote_icon.png
Originally Posted by Paulo
Ebwana eeeeee huwenda siku tukikutana kwenye Party ya JF patakuwa hapatoshi. Huenda tumepishana sana tu kwenye makorido ya chuo bwana.

Mbona hapo uliandika hivyo nilidhani unajua......thread iliwekwa na Pakajimy search Wana JF wa Arusha mambo yako huku.....
 
Hiyo ya mbuga za wanyama sijaiona. Mi nime recall kutoka kwenye thread ya siku nyingi member mmoja alipendekeza kuwe na party ya JF. Sasa ulivyosema tena mambo ya mbuga za wanyama ikasound new kwangu so nikadhani labda imependekezwa leo na mi sijaiona. Anyway, it's ok, nimekusoma.
 
Unapokumbuka uzuri wa mabibo hostel, do not forget the other side of the coin...Usafiri kutoka na kuenda chuo ulikuwa ni wa msoto mno na mi namshukuru Mungu hilo lilinipita kushoto.
 
Ebwana mkuu nimeiona kupitia link ulonipa. Thanks a lot b'se I hadn't seen it before. It sounds so interesting and hopeful itabamba kinoma.
 
Ebwana mkuu nimeiona kupitia link ulonipa. Thanks a lot b'se I hadn't seen it before. It sounds so interesting and hopeful itabamba kinoma.

Poa mkuu, ngoja nitoke nikatafute Kivuo cha uvuguvugu.
 
Kwenye mikusanyiko yote lazima kuwe na mambo ya ajabu kama hayo. Mnasahau wale akina dada waliokuwa wanapitisha ndizi, karanga nk. Mlikuwa mnawalamba mkichoka kusoma!
 
Ha ha ha yalikukuta bwana weee..... Basi sisi mwaka wetu ndo tuliokuwa wa kwanza kupangiwa mabibo hostel mwaka 2001. Mi nikatupwa mabibo na marafiki zangu wakabaki main campus. Lakini nikawa bado natokea home (mbezi beach) naenda chuo kwa karibu kama miezi miwili hivi basi ndo maclass mate zangu wa mabibo wakawa wanaeleza mambo ya mabibo yalivyokuwa hot hot na mabinti kama kina kitimoto na wengine kama mtakumbuka. Basi mi nikaona nikienda mabibo basi nitachakachua uadilifu wangu, so nikaswitch na jamaa mmoja mshamba mshamba akaenda mabibo na kunipisha campus. Basi tangu mwaka huo hadi 2005 sikuwahi kukosa accomodation main campus.

Pia nakumbuka cc ndo tuliokuwa wa kwanza kufanya matriculations ili kujoin chuo.... Challenges zilikuwa kibao kwa wwale tulio ingia 2001
.

Matriculations ilianza 1999 ila 2000 nadhani hawakufanya.

[/B]

Matriculations ilianza 1999 ila 2000 nadhani hawakufanya.

Weeeeeeee, Ncha umepitiwa Mkuu, tuliingia 2001/2002 naku-graduate 2005. Ina maana tulifanya matriculation 2000. Sisi ndo wa KWANZA kufanya MATRICULATION na waKWANZA kutumia mabibo hostel ingawaje wengine tuling'ang'ania campus. Please revisit documents zako utaona ilivyo kaa.
 
Kweli mmenikumbusha mengi,
mimi nilikuwa member mzuri wa block G,pale utakuta watoto wa mbwa wamesahau shida zao wananyonya beer kwa kutumia straw ndeeeefu kama mita moja hivi,huku pembeni fred saganda(yule mzee wa rap za kichaga) anavunja mistari kwa ustadi wa hali ya juu.
Ukiangalia kwa mbali ndani ya cafeteria kuna wa2 lukuki wako kwenye foleni ya wali special(mifupa),isitoshe kuna kundi la walevi wa muhimbili wamezunguka counter wakiwa juu juu kila mmoja kakalia viti vitano(vile vya coca cola).
Ukiona umechoka basi waweza jisogeza kule uwanjani kusikiliza watu 'wakikemea' lakini uwe tayari kuona couples zikifanya mavituzzzzz wazi wazi au uwe na mapafu yanayovumilia moshi mzito wa bange.thats college life bana!
Kichekesho ni ile siku ya j2 asubuhi;wengine mwanukia perfume kuelekea church,wengine wanarudi kutoka bills au kili times na harufu ya fegi.
Old good memories!
 
Alaf Complex pale palikuwa kama ni sehemu ya kuuza sura mno, kila nikienda pale wauza sura wanajaa pale naona kama walijipangia ratiba ya kuzuru pale kila wanapopata nafasi!!

Kuna siku wakati naenda kuoga (ilikuwa block D),niliwakuta jamaa na demu wake wakipiga mswaki bafuni asbh, nilivoingia bafuni nao wakaingia bafuni kuoga, baadae nikasikia miguno ya mahaba aisee!!!

Mabibo pale pana mambo sana!
 
@ Mopao na Jack mmenichekesha na kunikumbusha mengi nyie watu tunafahamiana sio siri, mnakumbuka yule jamaa alieenda sijui block C akakuta kuku aliyemnunulia demu wake apike wale nakumbuka ilikuwa sku ya J2 jamaa kutoka church akakuta mafupa na jamaa kavaa taulo yake kajitandaza kitandani na nilibaunsa kumpiga hawezi kulia hawezi ikabidi achukue Maliboro aweke kichwani kwa vile jiko lilikuwa na moto bado likayeyusha mnailoni ikaanza kumchoma kichwa
 
Tehtehteh....nimeshindwa kujizuia kucheka aisee. Maana'ke ni kwamba jamaa alimegewa demu'ake...

Pole zake huyo jamaa...
 
Hahaha vile viwanja vya mabibo wkt wa ucku ilikua noma mana hapa watu wanasali pale watu wana ngonoka,kule wanavuta bangi block g watu wanalewa,yan dhambi na kusali vilikua vina blend in kma kawa,ila me nlikua nakaa block f so exile ilikua ya kiutu uzima
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom