Hayo ni maisha ambayo ulishayaishi ama utakuja kuyaishi, baada ya kufa, mwili, unatupwa ( kuzikwa ) roho inaingia tena kwenye mzunguko mwingine kupitia mwili mwingine lakini kumbukumbu za nyuma ( maisha ya nyuma ) huwa zinajirudia kwa mtu huyu ambae ana roho ya zamani na mwili mpya.. hili hawataki tu kuliweka wazi lakini ndio kweli yenyewe, baada ya kufa utazaliwa, sehemu yoyote ile, kisha utakufa, utazaliwa na utakufa na ndio maana YESU aliwaahidi atarudi, ni kweli alirudi, akafa akarudi akafa na pengine hata muda huu yupo ila kwa mwili mwingine na mission nyingine kabisa..Mkuu ushaishi sana ( roho ) ndani ya miili tofauti tofauti miaka na mikaka, ushaishi kama Dino's, ushaishi kama samaki, ushaishi kidudu, utaishi kama binaadamu na baadae utaishi kama ghost, vyovyote itakavyokuwa , mwili wako utapotea lakini roho itavaa jumba lingine na itaishi milele.
Haya ni maono yangu..sikushawishi wala sikushauri uyatilie maanani.
Nitakupa link flani hivi ufuatilie Foundation moja ambayo inafuatilia mambo ambayo yakiwekwa wazi duniani hapa patakuwa pa moto ama foundation kama hizo zisingekuwepo sizani kama tungekaa na smartphone tukibonyeza kwa kujiachia namna hii, wapo watu wanakufa na baada ya masaa 72 wanazaliwa na kumbukumbu zao za zamani zote, na wanaa moja, wanaishi, wanakufa, wanazaliwa tena, tena wanazaliwa kwenye ile ile jamii yao.. wapo si porojo, wapo mkuu.