Maisha niliyoyapitia nikiwa na umri wa miaka 8-14

Jstar1

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
1,389
1,337
Huu umri sitakaa niusahau, kiukweli ni umri mdogo ila nimepitia mambo makubwa ambayo sitataka wanangu waje kuyapitia na naamini haitakuja kutokea.

Katika umri wa miaka hiyo ilikua kati ya 2006-2012, nmepitia mambo magumu, sitagusia upande wa wazazi wangu, ila kiukweli mzazi atabaki kua mzazi.

Nikiwa na umri wa miaka 8, nmechunga ng'ombe, nmevua samaki, nmelala majini mimi nmehama visiwa na kisiwa, nmefanya uvuv wa kila aina, ata ambao ni haramu, nmeuza maembe, machungwa, nmeuza karanga za mia mia, nmeuza mahindi ya kupasuka yale, nmeuza kuni.

Juzi nakuja kumuuliza mwanamke mmmja mtoto wako ana miaka mingapi akasema mtoto wangu bado mdogo, nkamuuliza mdog ana miaka mingapi, akajibu miaka 9 nilishtuka sana, hiyo miaka 9 mimi nilkua naenda shule na nkirudi napika.

Mungu si athmani sahivi nakula nachokitaka, sitachoka kushukuru, watu tunatembea ila mioyoni tuna siri nzito, nmehama wilaya baada ya kuchagukiwa form 1 wilaya nyingine, kupanda gari kwangu ilikua ndoto, mambo ni mengi, ila wazazi na watoto, maisha kila hatua ni magumu.

Naamini Mungu ndiye ajuaye hatina ya mtu, kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii bila kujali unapitia magumu gani, kama unavua vua haswa, kama unauza maembe uza kweli kweli, kama unasoma shika kalamu usiiachie, no one knows tomorrow.

Kama kuna mtu alipitia wakati mgumu akiwa na umri mdogo share na sisi tujue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Nimeanza kuvua samaki nikiwa na miaka 7, mnaenda na mtumbwi adi viswa vya mbali, kuna siku kimbunga kimetupiga tupo watu 7 kwenye mtumbwi,mtumbwi ukazama, kilichotusaidia ni vile vidumu vya maji(vya lita 5), tuliogelea umbali wa kama kilometer 4-5 kufika nchi kavu. Ila mimi nilikuwa nabebwa na wakubwa.
2. Shule (primary) nimetembea zaidi ya km 15 kwenda na kurudi, mlo ni adi urudi jioni,kuna siku bonge la nyoka(cobra) likaanguka toka juu ya paa kwa ndani, hiyo tupo darasa la tatu, yaani ndani ya dkk 5 tulishaliangamiza.
3.Wakati wa kilimo tunaamka saa 10 alfajiri kwenda kwanza shamba,ikifika saa 2 unapiga uji wa kutosha usio na sukari, alafu unaenda shule kusinzia. Wengine uji wenye sukari tumeunywa baada ya kufika sekondari, viatu nimevaa darasa la saba.
 
"Kuelezea hisia kwa njia ya maandishi si rahisi" binafsi nimekuelewa mkuu, pole sana kwa uliyo pitia pia usiwe mvivu wa kusaidia wale walio kwenye magum.
"Strongest people make time to help other even if they are struggling with their own problems".
 
Huo mtumbwi uliokuwa kilometa 5 kutoka nchi kavu huku ukiwa na watu 7 na vudumu vya lita tano vya kutosha kuokoa watu hao ulikuwa unajihusisha na uvuvi gani? Maana uvuvi wote naujua na matumizi ya hizo dumu moesy,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kiumbe aliyebeba maji kichwani kama mimi..Mpska sasa naweza beba ndoo kubwa kichwani bila kuweka kata kichaani na nikatembea bila kushika umbali wa 2km
Umenizi kuachia ndoo ikiwa kichwani. Mengine tunalingana. Kwa wenyeji wa mwanza wanaelewa umbali wa kutoka isamilo (paliitwa majengo mapya) hadi nera jirani na jengo la ccm mkoa. Nimebeba lita nyingi sana hapo nenda rudi.
 
Huo mtumbwi uliokuwa kilometa 5 kutoka nchi kavu huku ukiwa na watu 7 na vudumu vya lita tano vya kutosha kuokoa watu hao ulikuwa unajihusisha na uvuvi gani? Maana uvuvi wote naujua na matumizi ya hizo dumu

Sent using Jamii Forums mobile app
ulishawai vuka kisiwa kimoja adi kingine kwa mtumbwi? watu walikuwa saba , na vidumu (vya lita 5)vilikuwa vitatu, walikuwa wanapokezana adi tukafika nchi kavu. Kumbuka ni watu wanaojua kuogelea kwa sana, sema ile mtu akichoka anapewa kidumu ashikilie wakati anapumzika.
 
ulishawai vuka kisiwa kimoja adi kingine kwa mtumbwi? watu walikuwa saba , na vidumu (vya lita 5)viliukwa vitatu, walikuwa wanapokezana adi tukafika nchi kavu. Kumbuka ni watu wanaojua kuogelea kwa sana, sema ile mtu akichoka anapewa kidumu ashikilie wakata anapumzika.
hii kali mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom