Maisha hata hayanogi tena,jamiiforum hainogi tena imepoa tuliwaambia nchi inahitaji kiongozi wakuchilimua kama JPM.

Maisha hata hayanogi tena,jamiiforum hainogi tena imepoa tuliwaambia nchi inahitaji kiongozi wakuchilimua kama JPM.

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,574
Reaction score
56,795
Enzi za awamu ya tano mambo yalikuwa mchakamchaka kila siku unapata sababu ya kuishi ila siku hizi kumepoa sana hakuna wa kuchangamsha maisha, hakuna ziara za kushtukiza wala kutumbua majipu ni kama tunajilazimisha kuishi tu siku ziende.Mpaka topic za kuanzisha thread mtu unakosa.

Nikiingia mtandaoni nakosa cha kufanya x zinaboa,udaku unaboa,bongo fleva inaboa,wanasiasa wanaka,viongozi wa dini wanaboa...najikuta namaliza bando langu kaangalie Netflix movies na wildlife photographer,bambo na Mtanga,interview za zamani za kina noorah,old music ndo kidogo inanipotezea muda.
 
Kuna nini kipya bwashee..yaani mood yangu iko down sana siku hizi au ndo dalili za utu uzima na pressure..mbona hata sina madeni sina stress niko abroad kwenye standard life ila bado namiss kitu flani cha swahili na sikipati.
Tatizo una kaza fuvu sana , na hawa machawa wamevuruga majadiliano ya akili na utulivu kwa mustakabadhi wa maendeleo ya taifa
 
Back
Top Bottom