Maisha halisi nguzo yake ni ukweli lakini je, kwanini watu hugeuza maisha kuwa ni maigizo?

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,417
11,068
Habari JF,

Niwashirikishe kwenye chagizo la fikra na fikirishi kiasi, palipo na ladha, raha na utamu unayoweza kuihisi, kuionja, kuitamani, kuusikiia, kuisikilizia, kuipenda au kivyovyote vile nyuma ya pazia kuna uchafu na madudu ambayo hatimae tunapata vitu kama ladha, raha na utamu.

Hivyo basi iwavyo vyovyote vile yatupasa kuwa na maarifa thabiti juu ya matumizi ya maneno yoyote yale katika maisha yetu. Kuishi maisha kwende sambamba na kutambua yaliyo ya kweli na kuipenda kweli kwa vitendo.

Tusiige pasi na akili ya viulizo kwanini? Ili iweje ? kwa ajili ya nini na nani ? wakati gani na kwa nani?

Ukweli ni nguzo ya uzima na maarifa kinyume na hapo maisha yataendelea kuwa ni maigizo yenye upofu mwingi ndani yake.

Tuendelee kuimarika zaidi kifikra kwa kuishi na kueneza iliyo kweli.

🙏🙏🙏

Wadiz a.k.a Baharia
 
Back
Top Bottom