Je, ni kweli tunauishi upendo halisi ama ulio kizuizini?

Nov 2, 2023
60
50
Kila mtu anaweza kuwa na neno ukimuliza kuhusu upendo. Toka muda watu wamesha tafafuta maana nyingi za neno upendo lakini bado hakuna anayeweza kuongelea upendo kwa maneno na akaumaliza kama jinsi ulivyo. Kila mtu ataongelea matokeo yake kwa jinsi alivyo ishi na uzoefu wake katika mazingira yake.

Kwa tunavyoishi tumesha sikia na kuzoe kuwa upendo ni matendo fulani kumuonyesha mtu kwa kumjali na kumfanyia zaidi ya wengine kwa kujihisi una hitajika kufanya hivyo kwa jina la upendo. Kwa hili tunaona upendo ni matendo mema kwa kuwafanyia wengine.

Tujiulize, kwanini watu tunao wa penda ni rahisi sana kuwa adui zetu wakubwa? Kwani upendo unazalisha chuki ndani yake au kuna tatizo gani ndani yake linalo tupelekea kufanya haya mabaya mengi kwa jina la upendo. Au hatuelewi maana ya upendo tumeshika baadhi ya vitu vya kufanya tu na tukaishia hapo.

Kwanini upendo unakuwa wivu, una leta chuki, una kufanya uwe mtumwa wa mtu, kwa ufupi kwanini upendo uwe chanzo cha kukukosesha raha badala ya kukupa mwangaza wa kukushangaza jinsi unavyokuchukua na kupotea kwenye mshangao wake.

Kitu cha msingi kujua ni upendo hauna kikomo wala ubaya wowote ila sisi ndio tunautengeneza ufuti kwenye mifumo yetu ya kijinga tuliyojiwekea kwa kutojitambua kwetu na kuufanya upendo uwe kuzuizini na ufanye kama mifumo yetu ya akili ilivyojiwekea kujipa usalama. Kwa hili tunashindwa kupata upendo halisi na tunaishia kutumia kwa ajili ya kufurahisha akili zetu tu kwa jinsi mfumo wetu wa akili unavyopata faraja.

Mfumo wako wa akili una wezaje kuwa kizuizi cha upendo. Ni hivi, tumeshindwa kujifahamu undani wetu na thamani zetu. Akili yetu imekuwa ikituendesha bila sisi kuijua nafasi ya kikomo chake katika ufahamu wetu. Ufahamu wetu ukizidiwa na akili iliyojijenga kutafuta usalama uliojiwekea kutokana na mazingira yake, basi upendo nao hautakuwa na ufahamu bali kukidhi haja za akili tu.

Usipokuwa mwathirika wa akili yako kutaka kutumia nguvu kulinda upendo wako uuone muda wote, ukimtumia mtu meseji ajibu hapo hapo bila hivyo unawaza mengine, kutotaka kumuona na ushirikiano na mtu mwingine yoyote, hiyo yote ni akili kuwa bugudha kwenye upendo ila ukiweza kuuacha upendo utanue kama uhalisia wake ulivyo basi itapelekea mtu atajikuta analazimika kukupenda na kujilinda mwenyewe kwakuwa hatotaka kupoteza ladha halisi ya upendo usio na kizuizi cha akili.

Na huu upendo ulio chini ya akili ndio unaoleta msuguano kwenye maisha yetu, kwakuwa hatu ufungui kuona upendo unatushangaza nini bali unaziba pengo gani katika akili yetu na tunapoteza maana halisi ya upendo.

NB: Usijaribu kutafuta maana ya upendo iliyo kamilika hakuna. Cha muhimu ni kuishi kwenye ufahamu zaidi kwa kuelewa akili zetu na mifumo yetu ya kuishi tuliyojiwekea, na isiwe kizuizi cha kuona uhalisia wa maisha na upendo jinsi ulivyo bila kuweka ubinafsi wetu kati.
 
Back
Top Bottom