Maisha Binafsi ya rais wa Irani: Wanasiasa wa Tanzania tujifunze

Kwa Tanzania!! Ambako mtu anachukua pesa ya kujenga daraja anajenga kwake, pesa ya kujenga hospitali anajengea kimada, mradi anaukimbizia kusikostahili kwa sababu ana maslahi huko... ndio tupate mzalendo wa aina hiyo!?
hapana haitatokea kwa sababu wengi wetu HATUWAZI KITANZANIA... TUNAWAZA KINYUME NA TANZANIA!
Bado TUKO KWENYE ALINACHA!

Niliweka Avatar kama kumuenzi, na kumaanisha Watanzania tunahitaji kiongozi aina hiyo, Mkweli na Mzalendo kwa Nchi yake.
 
Na...pato la mwaka la Iran ni zaidi ya mara 300 ya pato la Bongo. Sisi tuna laana!
 
Hajaingia kaikopa chadema kujenga jumba la nanihii.

Kufikiri kuwa Slaa anaweza ishi au Ikulu kuwa Ofisi yake kama Rais ni ndoto za mchana.
milembe kumbe wagonjwa wanaruhusiwa kutoka hospitali siku hizi?
 
Dr.Slaa alitaka kupiga picha tu watu wamuone.Hayo maisha ya Rais wa Iran alianza kuyaishi kabla ya urais.Slaa anaishi maisha ya kifahari nyumbani mtaani anatuongopea ndo maana analipwa posho kuuubwa.Usilinganishe kichuguu na mlima bwana
Hujui maisha ya kifahari wewe
 
Wafanya biashara wa Iringa si ndivyo wanavyoishi?. Tena wanaambiwa hayo ni masharti ya waganga!
 
Mengine yote sawa, lakini kulala chini na kuishi kama maskini wakati CASH unazo?! Ngoja nikaulize Tunduma uchawi wa kuku na punje za mahindi!
 
Unaisapoti ccm kwa kuona mtu wa dini yako, akiondoka unarudi FUC!.

weng watakimbia ccm kwao ni makazi ya mpito makazi ya kudumu kwao ni CUF HATA MIKUTANO MINGI WANAOJAA CUF NI WALEWALE WA CCM.
 
Hapa kabla hatujaanza kwa viongozi wetu tujitazame na sisi mmoja mmoja,sisi hapa mtu akipata kichance kidogo sehem anayofanyia kazi tu mtaani watu tutakoma,tena akiishanunua kivista kuanzia wake zetu mpaka dada zetu watamtabua,nlichojifunza kwa huyu ahmednajad haya maisha anayoishi ni nature yanatoka toka moyoni wala hacopy na kupaste,kifupi anajitambua kama yeye ni binadamu ambae sio chochote,na anafaham kuwa mungu kamuweka hapo kwenye urais ili kusimamia haki za watu na sio kwenda kuwaibia au kuwadhulumu haki zao,

Viongozi wetu pamoja na sisi dini zetu tumezipa migongo sana lakini ukweli kama tungefata yale dini zetu zinatufundisha wote tungeishi maisha hayo maana ukitazama ndio mafundisho ya dini zote,
 

Ahmedinejad, the Iranian President, who astonished many when he first reached the
office of the Presidency by donating all the high valued Iranian carpets to one of the
mosques in Tehran by replacing them with the low cost ordinary carpets. He observed
that there was a huge extravagant lounge for receiving and welcoming the VIPs and
he ordered it to be closed and asked the protocol office to arrange for an ordinary
room only with wooden chairs.




Baada ya hizi impressive drama..mjiulize kwanini alitoa msikitini na si katika sinagogue au kanisa?Mungu hakupi thawabu kwa kuwapenda wakupendao,ila kwa maadui wazo.Kwani hata waovu hupenda wazovu wenzao na hakuna cha ziada ili upewe thawabu...wengi hamjaangalia hili.Wel crafted but poorly edited.
 
Huyu jamaa hata mimi namzimia sana,achilia mbali propaganda za uadui wao na west,huyu jamaa ni a true leader,down to earth,mwenye kujali maslahi ya taifa na wananchi wake,na pia very smart.Akiwa anaongea unatamani kusikiliza tu.Pia hapendi makuu na ni very simple.Ni kama alivyokuwa Nyerere hapa kwetu kwa kiasi flani.
 
Huyu jamaa hata mimi namzimia sana,achilia mbali propaganda za uadui wao na west,huyu jamaa ni a true leader,down to earth,mwenye kujali maslahi ya taifa na wananchi wake,na pia very smart.Akiwa anaongea unatamani kusikiliza tu.Pia hapendi makuu na ni very simple.Ni kama alivyokuwa Nyerere hapa kwetu kwa kiasi flani.

Nyerere aliagiza Mercedes Benz za kifahari enzi hizo 77 kwa ajili ya kupokea wageni 77 akawajengea na hoteli mpya inaitwa 77 yenye vyumba 77. kwa ajili ya mkutano wa siku tatu tu.

Unafananisha mbingu na ardhi?
 
Mwalimu Nyerere aliishi maisha simple pia ukilinganisha na viongozi wa enzi zake ambao walitawala wanachi wakiwa hawajaamka na wachache wakiwa na elimu angejilimbikizia pesa na utajiri kama wao na wakati anaondoka angehakikisha mwanae anakuwa Rais, pia Patrice Lumumba wa Congo Zaire, Marian Nguabi wa Congo Brazaville, Mutallah Muhammed wa Nigeria na Thomas Sankara waliishi maisha simple sana ,wakati wa mapinduzi ya kumuondoa Sankara yaliyofanywa na Blassier Compaore aliitangazia jumuiya ya kimataifa kuwa Sankara alikuwa kajilimbikizia mali baada ya uchunguzi kufanyika akakutwa alikuwa anamiliki pegout 504, gitaa moja na dollar za kimarekani 700 na hana nyumba wakati alikuwa katawala kwa miaka 5

Kuona vile wananchi wakaandamana katika mji mkuu wa Burkinafaso wakitaka Compaore aondolewe na kuuawa Compaore akiambia France International kuwa yeye hakupanga kuumua Sankara isipokuwa aliuawa kwa bahati mbaya tu ila yeye alitaka kumstafiisha kwa nguvu baada ya kuona sera zake za ujamaa zimeshindwa, Compaore kuona wananchi wamemlilia Sankara kwa nguvu akampa mjane wa Sankara Mariam dollar milioni moja na kumhamishia uhamishoni Ufaransa huku akiahidi familia yake kulipwa dollar 10,000 kila mwezi kama matumizi ya familia yake.

Kwahiyo zamani viongozi halisi walikuwepo wengine waliokuja ni wezi kwa ajili ya matumbo yao na familia zao
 
Nyerere aliagiza Mercedes Benz za kifahari enzi hizo 77 kwa ajili ya kupokea wageni 77 akawajengea na hoteli mpya inaitwa 77 yenye vyumba 77. kwa ajili ya mkutano wa siku tatu tu.

Unafananisha mbingu na ardhi?

Pamoja na maelezo yako Nyerere alikuwa kiongozi bora kuliko kiongozi yeyeto katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati hakujilimbikizia mali wala kutajirisha familia yake anaweza kuwa alifanya vile kukarimu wageni lakini sio kwa ajili yake huwezi kulinganisha na Mwinyi, Mkapa wala Kikwete wala Kenyatta, Mobutu, Museven, Kagame, Karume na wengine mwandishi mmoja mzungu aliandika kuwa pamoja na Nyerere kushindwa katika sera zake viongozi wa nchi za magharibi walimuona ni "saint" maana hakushindwa kwa dhamira mbaya bali alifanya kutoka moyoni akiamini kusaidia watu wake.
 
Back
Top Bottom