Maisha Binafsi ya rais wa Irani: Wanasiasa wa Tanzania tujifunze

Usiende mali sana kwenye urais......angalia wabunge wetu.....siku ukizuka moto pale mjengoni wapo ambao hawataweza hata kupiga hatua tatu..... kisa Nyama na Bia...
 
Under his authority whenever he appoints any minister to his post he gets a signed
document from him with many points particularly highlighting that he shall remain poor
and that his personal and his relatives accounts will be watched and the day he leaves
the ministry shall be with dignity, and therefore it is not lawful for him or his relatives to
take any advantage of his office. First of all he declared himself for all the 'Big' wealth
and the property he owned was a Peugeot 504 car, Model 1977, an old small house
inherited from his father 40-years ago in one of the poorest zones in Tehran . His
accounts with a zero balance and the only money comes in to his a/c was from his
salary from the university as a lecturer with an amount of US$ 250 only.

Chukulia wewe ni waziri ,unapewa Mkataba wenye vipengele kama hapo juu,utakubaliana na mkataba ?...kama umejiuliza mara mbili moyoni...inaonyesha ni jinsi gani ilivyo tabu kupata viongozi waadilifu
 
Inafurahisha lakini nadhani muhimu ni uwajibikaji wa kiongozi kwa taifa lake ktk kuondoa umasikini,kuinua uchumi na wananchi kuishi kwa haki na amani.
 
Kwa maana hiyo mawaziri kama kina maige tungekuwa tumeshanyongelea mbali...
 
Huyu jamaa ni kiboko yao maana sidhani kama kuna Rais ambaye anaishi maisha kama yake.
JK akiweza mwezi mmoja tu kuishi kama huyu basi Tanzania si masikini tena.
 
Habari hii imenifanya nimkumbuke former president wa Burkina Faso, THOMAS SANKARA, alikuwa na mambo kama hayo!

ata khomen alishi hivyo kabla ajasababisha vifo vya watu milioni 2 kwa vita baina ya iran na iraq ,kadhalika huyu mtamjua ni kwanini anaishi maisha ya kujifunga kama yupo vitani wakati atakapo ruhusu mabomu ya nyuklia kutumika na kuua idadi kubwa ya raia wasio na hatia ,watu wa tabia hizi usababishwa na chukizo moyoni kutokana na maisha magumu kupindukia katika maisha udogoni mwake .
 
Ndio maana viongozi wa Bongo wanasema nchi yetu haina dini ili wanufaike na matanuzi.
 
ata khomen alishi hivyo kabla ajasababisha vifo vya watu milioni 2 kwa vita baina ya iran na iraq ,kadhalika huyu mtamjua ni kwanini anaishi maisha ya kujifunga kama yupo vitani wakati atakapo ruhusu mabomu ya nyuklia kutumika na kuua idadi kubwa ya raia wasio na hatia ,watu wa tabia hizi usababishwa na chukizo moyoni kutokana na maisha magumu kupindukia katika maisha udogoni mwake .

sitaki kupuuza mtazamo wako ila nauheshimu kwa kuwa yaweza kuwa hivyo unavyoamini, lakini na mimi naamini si lazima iwe hivyo, kwa kuwa watu wanaweza kushabihiana kwa matendo lakini wakatofautiana kwa malengo yatakayotokana na matendo hayo!
 
Tuweke hii kwenye katiba kabla ya rais na mawaziri kuapishwa, pia mafao ya wabunge na ma vx, v8, etc. yakatiliwe mbali.
Under his authority whenever he appoints any minister to his post he gets a signed
document from him with many points particularly highlighting that he shall remain poor
and that his personal and his relatives accounts will be watched and the day he leaves
the ministry shall be with dignity, and therefore it is not lawful for him or his relatives to
take any advantage of his office. First of all he declared himself for all the 'Big' wealth
and the property he owned was a Peugeot 504 car, Model 1977, an old small house
inherited from his father 40-years ago in one of the poorest zones in Tehran . His
accounts with a zero balance and the only money comes in to his a/c was from his
salary from the university as a lecturer with an amount of US$ 250 only.

Kwanza, nimeshanga....had mda huu nahangaika na kubofya keybord yangu si wajua tena mambo ya wenzetu haya......Ni ukweli usiopingika Mh.Rais wa Iran anastahili si tu sifa bali kuombewa dua maalum ya kumwongezea maisha mema na marefu ili wenye kupenda kujifunza tujifunze kupitia yeye....
Hilo la kuhusu katiba kwamba la kupunguza matumizi, mi sidhani kama hata linahitajika kuwa kwenye katiba, ni utashi tu wa viongozi...Ikiwa watu wanaweza mfano futa mtihani wa darasa la nne na kidato cha pili,kisa mtoto wa presida hakufaulu....na baadae kuirudisha baada ya kukamilisha mambo yao sitashangaa ikiwa..Watanzania tutaambiwa,rais wetu mtukutu sio mtukufu hawezi kuishi maisha haya kwani serikali inazo rasmali za kutosha,mbona marais wenzake wa nchi jirani wana,hivi na vile yaani yeye hiki imekuwa nongwa....Watu wameshatengeneza dili hapo..umesahau zile kauli za hata wananchi wale majani ndege ya rais lazima inunuliwe?
Mi binafsi nayapenda maisha hayo, natamani niyaisha daima si kwa sababu kwa sasa nipo hivi ila ndio maisha ninayoyapenda daima...MUNGU WABARIKI WOTE WENYE KUWAPENDA WENZAO DAIMA
 
maisha haya yanawezekana hata hapa kwetu ,tukianzia na waheshimiwa wote tatizo ni pale wanapoanza kujiwaza wao kwanza na familia zao na kusahau wananchi wao.kiongozi anayewaza utaifa wake kwanza ni kiongozi madhubuti ,fananisha na hawa wakwetu wanaona mwananchi wa kawaida hana maana anahitajika wakati wa kura tu .hawezi kujishusha msafara inatisha .magari mazito hata kule afghanistan kuna nafuu ,
 
viongozi wetu bado sana kufika hapo. Siku wakiwa hivyo tz tutauaga umasikini.
Wote wanapenda ukubwa na wanapenda mambo makubwa ya ufahari.
Hakika huo ni mfano wa kuigwa.
 
Uyu jamaa siku alipokuwa anaapishwa nilijua hana makuu
Ila Tz kutekeleza haya ni issue bongo watu wanapenda starehe
 
V8.jpg
 
Akifanya hivyo hapa Tanzania watamuona mshamba. Huyu jamaa huwa anasimamia anachoamini tofauti na wezi wetu wanaohubiri maji wakanywa mvinyo. Huyu jamaa si mnafiki hata kidogo. Amesoma vilivyo. Ana PhD yake halali lakini haimpi shida kama jamaa zetu wapendao za kupewa. Kwa Tanzania rais kama huyu alikuwapo in Edward Sokoine wakaamua kumuulia mbali kwa vile alipingana na ufisi na ufisadi wao.
 
Kumbe 'Rais Paul Kagame' hata nje ya bara la Afrika wapo??????????? Nampenda sana Rais Kagame kwa staili yake ya uongozi uliotukuka na uadilifu usio na mawaa!!!!!!!!!!!

Was actually thinkin the same..anazo mapungufu zake but maisha ya Kagemae quite simple..
 
Mh kwa hili namfagilia sana rais huyu wa Iran ,awali nilimchukulia tofauti kwa hili nampa big up .Hebu viongozi wa Tanzania igeni mfano huu.Kwani tumeona viongozi wengi wa Kiafrika wanapopata madaraka wao pamoja na wanaowazunguka hubadilika ghaflakwa kuishi maisha ya juu ,kujilimbikizia mali ili hali wakiacha wananchi wanaishi maisha duni.
 
Back
Top Bottom