Maisha baada ya kifo

Umesema kweli.
 
Mkuu hiari ya kutenda ambapo ndio utashi unaousemea wewe; je mtu anawezaje kufanya bila kuwa na operating system (akili)?
 
Natamani watu hawa waelewe huu ukweli na waukubali,lakini kazi hii anaifanya mwenyewe Mola mlezi.

Kaka endelea kutupa faida.
 
2. Akili kwa binadamu inaumbwa na Mungu ambapo wewe umetumia neno utashi, hii akili ni operating system kwa binadamu yeyote yule asa kwanini Mungu asimuumbe kila mtu awe na operating system iliyokamilika?
Halafu ni nani aliyekuambia akili na Utashi ni kitu kimoja raia mwenzangu?


Akili ni uwezo wa kuelewa na kujifunza mambo au ni uwezo wa kufikiri na kuamua kwa busara, na busara ni uwezo wa kufikiria na kuamua jambo linalofaa. Utashi ni hiari ya kutenda na hiari tafsiri yake ni kufanya pasipo kulazimishwa.

Sasa pima mwenyewe kwenye mizani yako, kipi ni kipi na ni kipi kinakuja baada ya kipi?

Kwani ni nani asiyefahamu madhara ya ya kuvuta sigara? Lakini wapo wanaovuta na wengine ni madaktari, suala si kwamba hawana akili bali ni Utashi wao tu.
 
Swali je hayo unayoyafanya huwa unalazimishwa au huwa hifikirii ?

Ukinijibu hilo ujiandae kwa maswali mengine yatakayo tokana majibi yako.
 
hapa upo sawa kabisa kitu kingine mtu mpaka afe ni kwamba amepingana na law za nature
kama wanadamu tungeweza kufuata sheria za nature basi tungeishi milele assumption tu lkn
😀😀😀
Nacheka sana bro. Naomba unieleze hizo law za Nature ni nini hasa na zinafanyaje kazi ?

Nipo.......
 
hapa upo sawa kabisa kitu kingine mtu mpaka afe ni kwamba amepingana na law za nature
kama wanadamu tungeweza kufuata sheria za nature basi tungeishi milele assumption tu lkn
😀😀😀
Yaani hapo mtu anae kufa anakuwaje amepingana na law za Nature ?

Hizo law za Nature asili yake wapi ?

Pili unajua ni nini maana ya law ?

Tatu umejuaje kama hizo ni law ?

Kama hizo law umezijua kupitia binadamu ni upi ukweli wake halisi kutokana na ukamilifu ?

Naomba sana unijibu maswali haya kaka mkubwa ili nipate faida. Nasema hivi sababi huwa mnatabia ya kutokujibuwa maswalo ya msingi.

Nasubiri.............
 
😀 😀 😀 mkuu huu ulimwengu unatuchezesha kama midoli aise...
Kuchezeshwa kama mdoli unataka wewe bro. Ukimakinika na ukafikiri kwa usahihi utaelewa na utafaidika sana.


Ila kaa ukijua "Maisha ya duniani ni starehe za muda mfupi na ni upuuzi"

Akili tumepewa tuzitumie vizuri.
 


Kaka unauliza maswali mepesi sana. Umeshawahi kujiuliza kwanini Mola alileta mitume ?

Kwanini kwake yeye Mola kuna msamaha ?

Je kuna mtu ushawahi kumuuliza akajua yeye ni wa motoni au wa peponi ?

Tatizo lenu nyinyi huwa hamfikirii mambo kiundani.

Kaka leo kaa chini jiulize maswali haya,imekuwaje leo umejua kusoma na kuandika ?

Inakuwaje leo unatafuta hela na unapata ? Unafikiri ni kwa ujanja wako na maarifa yako ? Kama ni kwa ujanja wako na maarifa,kwa viwili hivyo mbona kuna wakati unatafuta na unakosa ?

Mola wetu ametupa neema kadha wa kadha,leo hii ona binadamu anavyo mkufuru na kumkana yeye lakini ana mpa rizki,na neema kadha wa kadha ?

Kaka kaa tenga muda ufikiri kinyume na unavyofikiri na yeye Mola anawapenda wale wenye kutumia akili.

Kauli hii huwa naitumia mara kadhaa kuwaambia wale wanaomkana Mola muumba,wajaribu kufikiria kinyume na wanavyofikiria bila shaka watambaukiwa na mengi wasiyoyajua.
 
"Roho yake hutoka, naye hurudi ardhini; siku hiyohiyo mawazo yake hupotea. Zaburi 146:4

"Walio hai wanajua kwamba watakufa, lakini waliokufa hawajui jambo lolote kamwe...jambo lolote unalofanya kwa mkono wako,lifanye kwa nguvu zako zote, kwa sababu hakuna kazi wala mipango wala ujuzi wala hekima kaburini, mahali unapokwenda. Mhubiri 9:5,10
 
Kuna tumaini gani kwa ajili ya wafu?
Yoh 5:28,29 matendo 24:15 "kutakuwa na ufufuo wa waadilifu na wasio waadilifu"majibu yote kutuhusu yapatikana kwenye biblia..Yehova anatueleza..
.
 

Kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba binadamu amewekea hali ya utashi. Hivi wakati Mungu anamuumba mtu si umesema kuwa Mungu anajua kuwa mtu X atakuwa ni wa motoni (ambapo kwa maelezo yako umesema kuwa anaenda kwa utashi wa huyo mtu mwenyewe), je inawezekana huyu mtu X akiwa duniani, akabadilika na akawa mtu wa peponi?
 
Swali je hayo unayoyafanya huwa unalazimishwa au huwa hifikirii ?

Ukinijibu hilo ujiandae kwa maswali mengine yatakayo tokana majibi yako.
Ikiwa Mungu anajua ya kuwa Zurri akizaliwa atakuwa ni mwizi ila kamuumba hivyo hivyo, je inawezekana Zurri akaja duniani na asiwe mwizi?
 
Mkuu umedandania comments bila kuangalia msingi wa hoja yangu. Nimeuliza hivi kipi tuamini kati ya hivi vitu viwili?


1)Mungu mwenyewe anaamua watu gani waende peponi na watu gani waende motoni. Kwavile yeye ndiye anayemuumba mtu na pia kabla hajamleta mtu duniani anajua mwanzo hadi mwisho wa huyo mtu utakuwaje. (Anajua alichokipanda na kitakachoota)

Au

2) Mungu hajui mwanzo(kabla ya mtu kuzaliwa)na mwisho wa mtu utakuaje hivyo jitihada au makosa yaweza kubadilisha hatima ya mtu (anajua alichokipanda ila kitachoota hajui)
 


Kaka nimekujibu vizuri sana nukta zako mbili tena kwa kuweka wazi kile kilichomo katika nukta hizo,soma tena utaelewa.
 
Juhudi zako unazotumia hapa duniani kuwa tajiri ni hizo utakazotumia kuingia mbinguni hata kwa kuhonga . Na uzembe wako wa kutokua tajiri utaenda motoni .
 
Kaka nimekujibu vizuri sana nukta zako mbili tena kwa kuweka wazi kile kilichomo katika nukta hizo,soma tena utaelewa.
Hilo jibu umeliona wewe, mimi sijaona ulipojibu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…