bwaiseekwetu
Senior Member
- May 29, 2022
- 172
- 471
Hii ni Kampuni ya Wachina ipo Veyula Dodoma na inazalisha Mafuta ya Kupikia.Hapa ni Jehanamu kwa kweli,yaani Wachina ni zaidi ya MAJAMBAZI wanatufanyisha kazi usiku kucha leo bila aibu wanatulazimisha kutusainisha Mkataba kwa malipo ya Laki Tatu kwa mwezi.Hivi Serikali ipo wapi??mbona hizi kero mnaambiwa kila siku??Kuna Wachina wanaishi hapa hawana hata Working Permit wanaishi kwa kujificha kama kunguru,maofisa Uhamiaji wakija wanaitwa chemba wanapewa kitu kidogo wanaondoka,maofisa kutoka OSHA na Idara ya Kazi nao wakija nao wanapewa kitu kidogo wanaondoka.Hii nchi imeoza rushwa mpaka matakoni