Maige: CCM itakufa

Maige amesema kwamba fedha aliyotumia kununulia hilo jumba ni pesa YA MKOPO KUTOKA BENKI WALIYOKOPESHWA KWA DHAMANA YA SERIKALI. Hiyo ni kwa WABUNGE wote .Yeye pesa yake kanunulia nyumba na Wabunge wengine wamefungua BIASHARA ambazo hawalipii hata kodi. Gharama ya nyumba anadai haifiki hizo dola kati ya 400,000-700,000 na amewaambia TAKUKURU waende kwa wakala wa uuzaji nyumba watapata bei halisi ya nyumba hiyo!

Tunajua TAKUKURU wako kazini baada ya muda mfupi tutapata majibu nani anasema ukweli.

Mkuu ni TAKUKURU ipi ambayo ipo kazini?kama ni ya Hosea usipoteze muda wako hakuna jipya hapo.
 
Hii ndiyo demokirasia. Maneno ni yake na mdomo ni wake.
Ushauri kwa Rais; Jaribu kutuwekea watu makini na welevu katika wizara zetu. we can see now the true colour of Mr Ezekiel Maige. watch out Mr President
Ushauri kwa CCM; Chama kimejaa watu wenye majungu, fitina na wasio wana CCM hasa. Kauli kama hii ya Ezekiel Maige ni ishara tosha kama yuko CCM kwa maslahi binafsi na kama hata yapata, eti anatishia kama ana watu 300 wanamtaka ahame chama(CCM).
Ushauri kwa Ezekiel Maige; Kama kweli wewe ni Mwana CCM, kumbuka kuna kifungu kwenye msahafu wa CCM unaoitwa ahadi za mwana CCM. moja ya ahadi inasema
Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu; Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote; Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu; Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko; Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.
kwa ushauri zaidi, Kumbuka hii ahadi isemayo.
Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa. hii iwe ni fundisho katika maisha yako mbeleni kwa vile TAKURURU wako njiani

 
Huyu hana jipya mbona alipokuwa waziri hajaongea upuuzi huu? anataka kuhama chama abaki kwenye gamba lao tu
 
pole maige, hamia kwenye basi kubwa cdm usibanane kwenye hako kabito ambacho kila m2 anataka kua dereva au akae siti ya mbele

Heko Lembeli kumwadabisha nitakupa jina la kajamaa kengine ni kawaziri ukaadhibu
 
sikatai lakini riziki hailazimishwi...si ana yale malori mawili yanayomwingizia dola elfu sijui nne kwa mwezi?? si ni msomi mzuri tu?? si ni mbunge??
Mkirua si kwamba ni msomi tuu bali ni "Qualified Accountant"
 
Last edited by a moderator:
duh, vijana hao, kaanza kuongea mapema sana......ni kumdharirisha aliykutea kwamba anasiliza majungu.. nadnani wapo wengine waliotakiwa kutoka lakini rais hakufanya hivyo.....ushari wa bule kwa Mh maige ni kukaa kimya basi
 
Maige ni Mbunge wangu ni mchapa kazi kweli,
ila NAMUUNGA MKONO na tunakaaahame chama kwenda CHADEMA NA BADO TUNAMPENDA[






QUOTE=Pharaoh;3954360]Kwa nini hajaleta utalii wa bahari ya Tanzania bara isiokuwa mahoteli, tungewapunguzia watalii wa beach zanzibar manake ndio wanaowapa jeuri
[/QUOTE]

Hata mim namkubali sana huyo mhe.Ni mbunge wangu,safi sana,hana makuu wala chuki binafsi na mtu.Ni mtu wa watu.MAIGE=IMAGE.Taka usitake
 
Tunaweza kuanzisha utalii wa watu kuja kuona 'FISI' kijijini kwako baada ya Twiga kuisha. Tunza vizuri hao fisi mheshimiwa, uwaziri wako wa maliasili waweza endelea kijijini kwako
 
hahaaa...labda angejiuliza yeye ni waziri wangapi kumwagika na ccm ikaendelea kusimama...akiona vipi abanduke aende cdm wanakopokea matapishi ya ccm......
 
Wee maige si ungenyamaza kwanza upepo upite ndo uanze kuropoka huo upuuzi wako.
 
Huyu MAIGE anelisema AKIWA ndani ya serikali au WAKATI AKITOKA KWA KUKERWA NA MATATIZO YA MCHAGUZI WAKE=HESHIMA,

Asemayo sasa NI KELELE ZA LOOSER Jimboni kwake wakigundua upuuzi wake heri wamwambie mapema AWAJIBIKE JIMBONI NA KUONESHA MCHANGO WAKE KABLA YA 2015
 
(Alidai kuwa fitina na majungu aliyofanyiwa na viongozi wenzake ndani ya chama hicho, yamewakera wana CCM wengi, kiasi kwamba wazee zaidi ya 300 wa jimbo lake wamemfuata wakitaka awaeleze msimamo wake ikiwa atahama ama ataendelea kuwa ndani ya CCM.“Wamekuja wazee hawa, wanawake kwa wanaume na vijana wengi, wakisikitika na kile kilichonitokea. Wanataka niwaambie kama nabaki CCM au naondoka, ili nao wanifuate,”)

Hivi nyie huwa mnajionaga ni kama watu gani vile? wewe hao watu wasubiri uamuzi wa utashi wako ndio na wao wakufwate huko? wao ni misukule wako? tatizo mmezoea kuongoza mawoter mellon na ndio maana mnabaki na mawazo haya, kama hao watu hawana utashi wa kuona mazuri na mabaya na kutegemea eti wewe utachofanya nao wanasubiria baki nao hukohuko hawana faida, kwani kabla ya wewe kua mbunge hao watu nani alikua anawasaidia kufikiria na kuamua cha kufwata? au ndio wanaofaidika kibinafsi na uwepo wako
 
pole maige, hamia kwenye basi kubwa cdm usibanane kwenye hako kabito ambacho kila m2 anataka kua dereva au akae siti ya mbele

Hakuna kuhamia CDM wala nini abakie huko huko kwa wanafiki wenzie.....angeteuliwa kwenye baraza jipya angeyasema hayo aliyoyasema?.....hayo ni maneno ya mkosaji......CCM huwa wanajifanya kucharuka na kusema hovyo wakitemwa kwenye nafasi zao za uongozi......hawawatendei haki watanzania manake wakiwa huko wanakuwa mstari wa mbele kutetea hata visivyofaa mbele ya jamii......wezi wakubwa hawa......aendelee kubaki kwenye lichama lake lenye amani na utulivu.....Hatumtaki CDM manake atatujazia nafasi za watanzania masikini na wenye uzalendo na nchi yao.......Chadema ni chama cha wananchi sio cha viongozi waliostaafishwa kwa kufuja mali ya umma!
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja aliwapa pole wana Kahama kwa kile alichodai kumpoteza mpiganaji, na zawadi kwa wananchi wa eneo hilo, hivyo kuichezea bahati hiyo ni ujinga kwa wale wasiopenda maendeleo.“Nafasi hizi hutolewa na Rais na haulizwi; ndivyo hivyo anapoamua kumpumzisha aliyemteua pia haulizwi. Inapotokea eneo kupata waziri ni fursa nzuri ya kupiga hatua katika maendeleo leo Kahama fursa hiyo haipo tena,” alisema Mgeja.

Kumbe uwaziri ni nafasi ya kupora mali ya umma na kupeleka jimboni haya ni matumizi mabaya ya madaraka na ndiyo maana tunapambana mawaziri wasiwe wabunge ili huu ujambazi ukome kabisa.............
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom