Maige: CCM itakufa

Maige: CCM itakufa

Anasema Ccm itakufa, anataka ife mara ngapi? Hajui kuwa CCM ni chama ambacho kinaongoza huku kikiwa marehemu?, washukuru sana wananchi wengi wa Tanzania kuwa mbumbumbu tofauti na hivyo sasa wangekuwa wanaongelea pumba zao kaburini.
.
"LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".
Anasahau tu kuwa yeye ni miongoni mwa waliochangia kuiua.
 
Mnafiki mkubwa Maige,unabwabwaja kama mwanamke wa uswahilini,kama unaona chama chako hakikufai basi ondoka si unakaa kulalama bila kuchukua hatua.

Ulichomwambia haitosho kbs!
Yeye anaona hali ilivyo anabaki kubwabwaja si aangushe zigo?
Wanyama wameuza si atoboe siri ilivyokuwa mpaka Twiga na wanyama wengine walivyofika Ughaibuni?

Movement For Change haimwachi hata mmoja kudadeki!
 
CHADEMA msimpe nafasi huyu kama atataka kuhamia kwa kuwa hana uzalendo na hawezi kukubali kuachia nafasi ili ufanisi upatikane, ni mng'ang'anizi wa madaraka, akafie mbali.
 
MBUNGE wa Jimbo la Msalala na Waziri wa zamani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amedai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitakufa kutokana na tabia ya viongozi wake kuendesha chama kwa kuegemea majungu na wivu wa madaraka.Kauli hiyo aliitoa jana katika ofisi za CCM wilaya ya Kahama, mbele ya mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja na viongozi wengine wa mkoa na wilaya.Maige alidai kuwa vitendo vya majungu na uongo uliokithiri vimechukua nafasi kubwa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali, hali ambayo itasababisha chama hicho kupoteza uwezo wa kuongoza na kuanguka.Alidai kuwa viongozi wachapakazi na wazalendo kwa nchi yao, wamekuwa wakipigwa vita kali na baadhi ya watendaji serikalini, bungeni na ndani ya chama hicho kwa maslahi binafsi.Maige alisema hasikitiki kuondolewa katika nafasi ya uwaziri, bali kinachomuuna ni kutimuliwa bila hata kupewa nafasi ya kujieleza katika ngazi zote husika ndani ya serikali na chama."Sikupewa nafasi yoyote, iwe ni katika kamati za Bunge au ndani ya chama kama zilivyo kanuni zetu. Hakuna aliyetaka kunisikiliza, na wengi waliosikia uzushi wa tuhuma zangu, waliamini na kuchukua maamuzi," alisema.Alidai kwa kipindi chote alichokuwa waziri, alipambana na mambo mengi mazito kwa kuzingatia kuwa wizara hiyo ni nzito na yenye utajiri mkubwa, lakini ameshangaa kuona kuwa mwisho wa uzalendo wake ni kuondolewa kwa aibu."Silalamiki kuondoka kwa vile hiyo ilikuwa ni dhamana, lakini sikufurahishwa kuondolewa kwa tuhuma ambazo kwanza sio za kweli, na pili sikupewa fursa ya kuzijibu kwa ufasaha na kwa uchambuzi makini wa kitaalamu. Hii ni hatari kwa sababu inaua chama kwa kupoteza watendaji wenye uchungu na taifa lao," alisema mbunge huyo.Alilaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM kushabikia kuondolewa kwake kwenye uwaziri ambapo walidhihirisha namna ambavyo si wakomavu wa kisiasa kwa kudhani kwamba wanamkomoa pasipo kuzama kwa kina na kubaini kuwa wao ndio watakaoathirika hasa kwa kuwa posho zao na mishahara zinatokana na jimbo hilo kuendelea kuwa mikononi mwa CCM na si vinginevyo.Alidai kuwa fitina na majungu aliyofanyiwa na viongozi wenzake ndani ya chama hicho, yamewakera wana CCM wengi, kiasi kwamba wazee zaidi ya 300 wa jimbo lake wamemfuata wakitaka awaeleze msimamo wake ikiwa atahama ama ataendelea kuwa ndani ya CCM."Wamekuja wazee hawa, wanawake kwa wanaume na vijana wengi, wakisikitika na kile kilichonitokea. Wanataka niwaambie kama nabaki CCM au naondoka, ili nao wanifuate," alisema.Aliongeza kuwa kwa kuwa yeye ni zao la wananchi wa Msalala, ni jukumu la wananchi kumuamlia hatima yake, na yeye atakuwa mtiifu kwao.Maige alidai inasikitisha kuona kuwa kuna nguvu kubwa za upinzani nchini, hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati wao CCM wamekalia majungu na fitina zisizo na maana.Hivyo, ametahadharisha kuwa wana CCM, wasishangae jimbo hilo likichukuliwa na wapinzani katika uchaguzi mkuu ujao, na wala hatakuwa na hasara.Aliongeza kuwa CCM yenye nyenzo zote za usafiri ikiwemo magari na pikipiki, imeshindwa kuhamasisha watu wilayani kote lakini CHADEMA wasiokuwa hata na baiskeli wamepita jimbo zima wakifanya mikutano yao na kugawa bendera zao kama njugu.Maige alimshambulia Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, akidai kuwa alipeleka taarifa ya uongo na iliyojaa unafiki kwa lengo la kumng'oa kwenye uwaziri na kwamba ndio maana baada ya lengo lao kutimia walitimkia Japan kujipongeza.Alimtaka Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama, kwa kuwa ametekeleza lengo lake la kumng'oa kwenye uwaziri sasa waketi meza ya mazungumzo kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama kwa kuwa kabla ya kupata wadhifa huo walikuwa marafiki na walitembea pamoja kwenye majimbo yote ya Kahama na Msalala kwenye mikutano yao.Naye Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Kahama, Hamad Masoud, alisema suala la ugomvi kati ya wabunge hao litafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya chama ili liweze kufanyiwa kazi.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja aliwapa pole wana Kahama kwa kile alichodai kumpoteza mpiganaji, na zawadi kwa wananchi wa eneo hilo, hivyo kuichezea bahati hiyo ni ujinga kwa wale wasiopenda maendeleo."Nafasi hizi hutolewa na Rais na haulizwi; ndivyo hivyo anapoamua kumpumzisha aliyemteua pia haulizwi. Inapotokea eneo kupata waziri ni fursa nzuri ya kupiga hatua katika maendeleo leo Kahama fursa hiyo haipo tena," alisema Mgeja.

Tanzania Daima

Maige anaanza kujifunza sanaa ukubwani!! Kama ndani ya chama chake cha "NyinyiEM" walimnyima nafasi ya kujieleza read KUJITETEA; kwa nini asitumie fursa hii ya kurejea kwake jimboni kuwaeleza wapiga kura wake ukweli kuhusu sakata zima? awaeleze dola laki 7 (410 according to him) nini siri yake badala ya kumlaumu Lembeli; ajifunze kutoka CDM ambayo alitumia fursa hiyo kuisifia sana organisational capabiolity yake; tukitendewa ndivyo sivyo na kuzomewa viongozi wetu hupeleka kesi kwa wananchi, kwa nini yeye asifanye hivyo kwenye hadhara hiyo. msanii tu. sasa asubiri kupandishwa kizimbani mpaka kieleweke. umma ujue kijana mdogo kama yeye na uwaziri wa miaka 3 kapata wapi dola laki 4?!
 
mbona ulikuwa haujatueleza,yaani ukikoswa uwaziri hapohapo na ccm inakufa.....................
 
pole maige, hamia kwenye basi kubwa cdm usibanane kwenye hako kabito ambacho kila m2 anataka kua dereva au akae siti ya mbele

naamin IPO SIKU ATAPIGA CHAFYA,,,,,kuntaja alotorosha wanyama pale KIA
 
Kwa hili Maige amenishangaza sana, yaani baada ya kutoswa uwaziri unasema CCM itakufa. Kwani CCM inategemea wizara ya Maliasili kujiendesha..au vile vitalu na twiga waliopanda ndege ilikuwa kwa ajili ya CCM.
Mawaziri kama hawa hawafai coz hawajui maana ya uwajibikaji, ninaamini uwajibikaji ni nyenzo muhimu sana katika siasa unapoona mambo hayaendi kama ulivyokuwa unataka unaachia ngazi hapo tutakuona shujaa na siyo mpaka utoswe then useme wewe bado ni shujaa. Ungeyaongea haya baada ya kujiuzulu mwenyewe ingekuwa na maana lakini coz umepigwa chini then unaona chama kitakufa hapa hufai hata kuwepo kwenye siasa.
 
Wakati anapewa uwaziri akakenea mene 32 nje hakujua chama kinakufa shwain

Sizitaki mbichi hizi
 
Kwa nini hajaleta utalii wa bahari ya Tanzania bara isiokuwa mahoteli, tungewapunguzia watalii wa beach zanzibar manake ndio wanaowapa jeuri
 
Pwani ya bara ni tupu na ni pottencial kubwa ambayo hatujaitumia
 
pole maige, hamia kwenye basi kubwa cdm usibanane kwenye hako kabito ambacho kila m2 anataka kua dereva au akae siti ya mbele

teh!teh!....ya nini kubanana wakati mungu katupa maccopolo tunashindwa kuitumia tu.....maigeeee wakati ndio huu baadae hutapata nafasi
 
Mzee wagobe upooo au mkuki kwa nguruwe mtam kwa binadam mchungu?.
 
Maige ni Mbunge wangu ni mchapa kazi kweli,
ila NAMUUNGA MKONO na tunakaaahame chama kwenda CHADEMA NA BADO TUNAMPENDA[

QUOTE=Pharaoh;3954360]Kwa nini hajaleta utalii wa bahari ya Tanzania bara isiokuwa mahoteli, tungewapunguzia watalii wa beach zanzibar manake ndio wanaowapa jeuri[/QUOTE]
 
MBUNGE wa Jimbo la Msalala na Waziri wa zamani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amedai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitakufa kutokana na tabia ya viongozi wake kuendesha chama kwa kuegemea majungu na wivu wa madaraka.Kauli hiyo aliitoa jana katika ofisi za CCM wilaya ya Kahama, mbele ya mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja na viongozi wengine wa mkoa na wilaya.Maige alidai kuwa vitendo vya majungu na uongo uliokithiri vimechukua nafasi kubwa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali, hali ambayo itasababisha chama hicho kupoteza uwezo wa kuongoza na kuanguka.Alidai kuwa viongozi wachapakazi na wazalendo kwa nchi yao, wamekuwa wakipigwa vita kali na baadhi ya watendaji serikalini, bungeni na ndani ya chama hicho kwa maslahi binafsi.Maige alisema hasikitiki kuondolewa katika nafasi ya uwaziri, bali kinachomuuna ni kutimuliwa bila hata kupewa nafasi ya kujieleza katika ngazi zote husika ndani ya serikali na chama."Sikupewa nafasi yoyote, iwe ni katika kamati za Bunge au ndani ya chama kama zilivyo kanuni zetu. Hakuna aliyetaka kunisikiliza, na wengi waliosikia uzushi wa tuhuma zangu, waliamini na kuchukua maamuzi," alisema.Alidai kwa kipindi chote alichokuwa waziri, alipambana na mambo mengi mazito kwa kuzingatia kuwa wizara hiyo ni nzito na yenye utajiri mkubwa, lakini ameshangaa kuona kuwa mwisho wa uzalendo wake ni kuondolewa kwa aibu."Silalamiki kuondoka kwa vile hiyo ilikuwa ni dhamana, lakini sikufurahishwa kuondolewa kwa tuhuma ambazo kwanza sio za kweli, na pili sikupewa fursa ya kuzijibu kwa ufasaha na kwa uchambuzi makini wa kitaalamu. Hii ni hatari kwa sababu inaua chama kwa kupoteza watendaji wenye uchungu na taifa lao," alisema mbunge huyo.Alilaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM kushabikia kuondolewa kwake kwenye uwaziri ambapo walidhihirisha namna ambavyo si wakomavu wa kisiasa kwa kudhani kwamba wanamkomoa pasipo kuzama kwa kina na kubaini kuwa wao ndio watakaoathirika hasa kwa kuwa posho zao na mishahara zinatokana na jimbo hilo kuendelea kuwa mikononi mwa CCM na si vinginevyo.Alidai kuwa fitina na majungu aliyofanyiwa na viongozi wenzake ndani ya chama hicho, yamewakera wana CCM wengi, kiasi kwamba wazee zaidi ya 300 wa jimbo lake wamemfuata wakitaka awaeleze msimamo wake ikiwa atahama ama ataendelea kuwa ndani ya CCM."Wamekuja wazee hawa, wanawake kwa wanaume na vijana wengi, wakisikitika na kile kilichonitokea. Wanataka niwaambie kama nabaki CCM au naondoka, ili nao wanifuate," alisema.Aliongeza kuwa kwa kuwa yeye ni zao la wananchi wa Msalala, ni jukumu la wananchi kumuamlia hatima yake, na yeye atakuwa mtiifu kwao.Maige alidai inasikitisha kuona kuwa kuna nguvu kubwa za upinzani nchini, hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati wao CCM wamekalia majungu na fitina zisizo na maana.Hivyo, ametahadharisha kuwa wana CCM, wasishangae jimbo hilo likichukuliwa na wapinzani katika uchaguzi mkuu ujao, na wala hatakuwa na hasara.Aliongeza kuwa CCM yenye nyenzo zote za usafiri ikiwemo magari na pikipiki, imeshindwa kuhamasisha watu wilayani kote lakini CHADEMA wasiokuwa hata na baiskeli wamepita jimbo zima wakifanya mikutano yao na kugawa bendera zao kama njugu.Maige alimshambulia Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, akidai kuwa alipeleka taarifa ya uongo na iliyojaa unafiki kwa lengo la kumng'oa kwenye uwaziri na kwamba ndio maana baada ya lengo lao kutimia walitimkia Japan kujipongeza.Alimtaka Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama, kwa kuwa ametekeleza lengo lake la kumng'oa kwenye uwaziri sasa waketi meza ya mazungumzo kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama kwa kuwa kabla ya kupata wadhifa huo walikuwa marafiki na walitembea pamoja kwenye majimbo yote ya Kahama na Msalala kwenye mikutano yao.Naye Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Kahama, Hamad Masoud, alisema suala la ugomvi kati ya wabunge hao litafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya chama ili liweze kufanyiwa kazi.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja aliwapa pole wana Kahama kwa kile alichodai kumpoteza mpiganaji, na zawadi kwa wananchi wa eneo hilo, hivyo kuichezea bahati hiyo ni ujinga kwa wale wasiopenda maendeleo."Nafasi hizi hutolewa na Rais na haulizwi; ndivyo hivyo anapoamua kumpumzisha aliyemteua pia haulizwi. Inapotokea eneo kupata waziri ni fursa nzuri ya kupiga hatua katika maendeleo leo Kahama fursa hiyo haipo tena," alisema Mgeja.

Tanzania Daima

Hawa ndiyo viongozi wenye uroho wa Madaraka wasiyotakiwa. Ina maana katika Mawaziri walioachwa yeye ndo amefanyiwa majungu? na Mbona hakusema ni majungu kabla hajawajibishwa?
 
Maige ni Mbunge wangu ni mchapa kazi kweli,
ila NAMUUNGA MKONO na tunakaaahame chama kwenda CHADEMA NA BADO TUNAMPENDA[

QUOTE=Pharaoh;3954360]Kwa nini hajaleta utalii wa bahari ya Tanzania bara isiokuwa mahoteli, tungewapunguzia watalii wa beach zanzibar manake ndio wanaowapa jeuri
[/QUOTE]
Mbunge wako baada ya kutemwa siyo, na mbona wewe ulikuwa wa kwanza hapa JF achukuliwe hatua. Mdanganyeni huyo fisadi kwa maneno ya kukkejeli, tuone mwisho wake. Hivi anafikiri kulalama wananchi wake watamsamehe? Labda aende kule wanakopokelewa walioshindikana manake kule hakuna sisa tena bali ulaghai mtupu.
 
Back
Top Bottom