Maige: CCM itakufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maige: CCM itakufa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, May 29, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa Jimbo la Msalala na Waziri wa zamani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amedai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitakufa kutokana na tabia ya viongozi wake kuendesha chama kwa kuegemea majungu na wivu wa madaraka.Kauli hiyo aliitoa jana katika ofisi za CCM wilaya ya Kahama, mbele ya mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja na viongozi wengine wa mkoa na wilaya.Maige alidai kuwa vitendo vya majungu na uongo uliokithiri vimechukua nafasi kubwa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali, hali ambayo itasababisha chama hicho kupoteza uwezo wa kuongoza na kuanguka.Alidai kuwa viongozi wachapakazi na wazalendo kwa nchi yao, wamekuwa wakipigwa vita kali na baadhi ya watendaji serikalini, bungeni na ndani ya chama hicho kwa maslahi binafsi.Maige alisema hasikitiki kuondolewa katika nafasi ya uwaziri, bali kinachomuuna ni kutimuliwa bila hata kupewa nafasi ya kujieleza katika ngazi zote husika ndani ya serikali na chama."Sikupewa nafasi yoyote, iwe ni katika kamati za Bunge au ndani ya chama kama zilivyo kanuni zetu. Hakuna aliyetaka kunisikiliza, na wengi waliosikia uzushi wa tuhuma zangu, waliamini na kuchukua maamuzi," alisema.Alidai kwa kipindi chote alichokuwa waziri, alipambana na mambo mengi mazito kwa kuzingatia kuwa wizara hiyo ni nzito na yenye utajiri mkubwa, lakini ameshangaa kuona kuwa mwisho wa uzalendo wake ni kuondolewa kwa aibu."Silalamiki kuondoka kwa vile hiyo ilikuwa ni dhamana, lakini sikufurahishwa kuondolewa kwa tuhuma ambazo kwanza sio za kweli, na pili sikupewa fursa ya kuzijibu kwa ufasaha na kwa uchambuzi makini wa kitaalamu. Hii ni hatari kwa sababu inaua chama kwa kupoteza watendaji wenye uchungu na taifa lao," alisema mbunge huyo.Alilaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM kushabikia kuondolewa kwake kwenye uwaziri ambapo walidhihirisha namna ambavyo si wakomavu wa kisiasa kwa kudhani kwamba wanamkomoa pasipo kuzama kwa kina na kubaini kuwa wao ndio watakaoathirika hasa kwa kuwa posho zao na mishahara zinatokana na jimbo hilo kuendelea kuwa mikononi mwa CCM na si vinginevyo.Alidai kuwa fitina na majungu aliyofanyiwa na viongozi wenzake ndani ya chama hicho, yamewakera wana CCM wengi, kiasi kwamba wazee zaidi ya 300 wa jimbo lake wamemfuata wakitaka awaeleze msimamo wake ikiwa atahama ama ataendelea kuwa ndani ya CCM."Wamekuja wazee hawa, wanawake kwa wanaume na vijana wengi, wakisikitika na kile kilichonitokea. Wanataka niwaambie kama nabaki CCM au naondoka, ili nao wanifuate," alisema.Aliongeza kuwa kwa kuwa yeye ni zao la wananchi wa Msalala, ni jukumu la wananchi kumuamlia hatima yake, na yeye atakuwa mtiifu kwao.Maige alidai inasikitisha kuona kuwa kuna nguvu kubwa za upinzani nchini, hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati wao CCM wamekalia majungu na fitina zisizo na maana.Hivyo, ametahadharisha kuwa wana CCM, wasishangae jimbo hilo likichukuliwa na wapinzani katika uchaguzi mkuu ujao, na wala hatakuwa na hasara.Aliongeza kuwa CCM yenye nyenzo zote za usafiri ikiwemo magari na pikipiki, imeshindwa kuhamasisha watu wilayani kote lakini CHADEMA wasiokuwa hata na baiskeli wamepita jimbo zima wakifanya mikutano yao na kugawa bendera zao kama njugu.Maige alimshambulia Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, akidai kuwa alipeleka taarifa ya uongo na iliyojaa unafiki kwa lengo la kumng'oa kwenye uwaziri na kwamba ndio maana baada ya lengo lao kutimia walitimkia Japan kujipongeza.Alimtaka Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama, kwa kuwa ametekeleza lengo lake la kumng'oa kwenye uwaziri sasa waketi meza ya mazungumzo kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama kwa kuwa kabla ya kupata wadhifa huo walikuwa marafiki na walitembea pamoja kwenye majimbo yote ya Kahama na Msalala kwenye mikutano yao.Naye Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Kahama, Hamad Masoud, alisema suala la ugomvi kati ya wabunge hao litafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya chama ili liweze kufanyiwa kazi.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja aliwapa pole wana Kahama kwa kile alichodai kumpoteza mpiganaji, na zawadi kwa wananchi wa eneo hilo, hivyo kuichezea bahati hiyo ni ujinga kwa wale wasiopenda maendeleo."Nafasi hizi hutolewa na Rais na haulizwi; ndivyo hivyo anapoamua kumpumzisha aliyemteua pia haulizwi. Inapotokea eneo kupata waziri ni fursa nzuri ya kupiga hatua katika maendeleo leo Kahama fursa hiyo haipo tena," alisema Mgeja.

  Tanzania Daima
   
 2. Wizzo

  Wizzo JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  pole maige, hamia kwenye basi kubwa cdm usibanane kwenye hako kabito ambacho kila m2 anataka kua dereva au akae siti ya mbele
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Maige asilete talalila, aueleze umma wa watanzania, dola 700,000 amezipata wapi< Mbona kabla ya kuwa waziri alikuwa hajazipata? asiwafanye wote wajinga
   
 4. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Jimbo kuwa mikononi mwa CCm na na viongozi na watendaji wa CCm kupata posho vina uhusiano gani au ndio yale yale ya Homa Shopping Centre nkatika madini yetu?
   
 5. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa naye anatia aibu sasa... wangapi wameondolewa uwaziri kwani alikuwa na ubia na hiyo nafasi?? Mbona ananung'unika as if ilikuwa ajira?
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Maige mwizi mkubwa wewe leo ndiyo umegundua uozo wa ccm acha uzezeta wewe msukuma.Mbona tunasikia kule bulyankuru gold mine ulikuwa kwenye payroll, umewasaliti wana msalala na kukubali pension ya Bearrick.
   
 7. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Maige anaonekana kuumizwa sana na kunyang'anywa Uwaziri.

  Mimi nampa ushauri wa bure. Kwamba kama ana uhakika kuwa YUKO CLEAN ila tu wenzake ndani ya Chama chao cha Magamba-CCM wamemfanyia fitna,hujuma na majungu basi RUKSA KUHAMIA CHADEMA. Namwomba aingie kwenye mdundo wa CHADEMA wa VUA GAMBA,VAA GWANDA.

  CHADEMA tutakuwa tumejihakikishia jimbo la Msalala kulichukua mwaka 2015. Lakini tutamkaribisha kwa tahadhari kubwa. Kama akileta porojo za Vuvuzela Shibuda tutamtimua. CHADEMA siyo kichaka cha MAFISADI.

  Naamini hata uongozi wa juu wa CHADEMA hautasita kumkaribisha.

  TULIHO BABA NG'WANA MAIGE!

   
 8. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  kweli sheikh yahya R.I.P aliacha urithi mkubwa, watabiri wamekua wengi, tunaomba utabiri wako uwe kweli mheshimiwa mbunge, kife na kusiwepo wa kukifufua
   
 9. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Asahihishe kauli yake, CCM imeshakufa!!! kinachosubiriwa ni mazishi, ndugu wa karibu na mbali kama CUF, TLP na NCCR wamekwisha fika eneo la msiba, wanasaidiana kuandaa mazishi huko Znz, na Bungeni Tz.
   
 10. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Maige amesema kwamba fedha aliyotumia kununulia hilo jumba ni pesa YA MKOPO KUTOKA BENKI WALIYOKOPESHWA KWA DHAMANA YA SERIKALI. Hiyo ni kwa WABUNGE wote .Yeye pesa yake kanunulia nyumba na Wabunge wengine wamefungua BIASHARA ambazo hawalipii hata kodi. Gharama ya nyumba anadai haifiki hizo dola kati ya 400,000-700,000 na amewaambia TAKUKURU waende kwa wakala wa uuzaji nyumba watapata bei halisi ya nyumba hiyo!

  Tunajua TAKUKURU wako kazini baada ya muda mfupi tutapata majibu nani anasema ukweli.
   
 11. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Atakufa yeye CCM ataaiacha, ife kwanini?

  Kwasababau yeye ameumbuliwa?
  who is Maige ndani ya CCM?
   
 12. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Huu ndio undumila kuwili, kama kweli ye alistahili kwanini hakuibua haya manug'uniko yake ambayo kila kukicha sasa anazua toka amepigwa tiper.
   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Waliondolewa ni wengi lalini kumbuka kina Mkulo na Omari Nundu wale ni wastaafu wakati Maige ana zaidi ya miaka 20 afike umri wa kustaafu
   
 14. m

  majebere JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  mchukueni CDM huyu. CCM wamesha mstukia.
   
 15. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  CCM itakufa kwa kuwa amepokwa uwaziri au kwa sababu gani?
   
 16. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  CDM isipokuwa makini muda si mrefu itajikuta imevamiwa na majambazi wengi wa CCM kama ngao ya kujikinga na ouvu wao. That's what they did in Kenya after the ouster of KANU.
   
 17. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mnafiki mkubwa Maige,unabwabwaja kama mwanamke wa uswahilini,kama unaona chama chako hakikufai basi ondoka si unakaa kulalama bila kuchukua hatua.
   
 18. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Anasema Ccm itakufa, anataka ife mara ngapi? Hajui kuwa CCM ni chama ambacho kinaongoza huku kikiwa marehemu?, washukuru sana wananchi wengi wa Tanzania kuwa mbumbumbu tofauti na hivyo sasa wangekuwa wanaongelea pumba zao kaburini.
  .
  "LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".
   
 19. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Na CDM walivyo na papara, sitashangaa kweli wakilichukua hili garasa.
   
 20. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  waziri 'mstaafu' aliyekimbia na masanduku ya kura za urais. Hakuna ajuaye JK alipata kura ngapi wala dr. Slaa wala Tume
   
Loading...