Mahusiano na Mitandao ya Jamii

Mahusiano na Mitandao ya Jamii

Miss Kim

Senior Member
Joined
May 3, 2014
Posts
164
Reaction score
273
Habari za mchana wakuu. Poleni na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Nimatumaini yangu kwamba wote hatujambo na wazima wa afya.

Nimejikuta nikiwaza na kuwazua juu ya jambo fulani; mahusiano na mitandao ya jamii. Hivi inakuwaje watu siku hizi kuanika mambo yao kwenye mitandao ya jamii?

Unakuta watu ndo mmekutana na kuwa wapenzi, within a month tayari umeshapost picha IG ama Facebook ukiwa na mpenzi wako mpya looking all lovey dovey, mara una update status kila baada ya masaa mawili ilimradi tu watu wajue na ww umo, 3 months down the line mmeshabwagana na kila mtu kuchukua hamsini zake, picha ulizozianika huko kwenye mitandao inabidi uzifute na kumblock kabisa huyo muhusika.

Hivi kwanini wadada haswa haswa ndo waadhirika wakubwa wa huu ulimbukeni wa mitandao ya jamii? When you fall in love you let the whole world knows and when you fall out of love you go preaching to every John, Dick & Harry about your broken heart & stuff.

Is it really necessary for all that drama? Tunajisahau sana na mwisho wa siku unajikuta umeacha historia mbaya kwenye mitandao ya jamii kwasababu mara nyingi unachokiweka humo kinabaki katika kumbukumbu zao.

Tujifunze na kujirekebisha bandugu.
 
Yaani nimekuwa nikiheshimu sana mitandao, Ktk mitandao nitaweka yale mambo ambayo jamii ikiyaona haitanifikiria vingine..
Kuhusu mimi na mpenzi wangu jamii haihusu kujua...Jamii itajua tuu pale nitakapoolewa ndipo wataona picha pasi na hapo mpenzi wangu yeyote hatoonekana ktk picha Si ya WhatsApp si FB...Sipendi...Sababu mapenzi ya siku hizi mwezi mpo pamoja mwezi hampo pamoja....


ILA kunawatu wanapenda kujionyesha...anyway LIFE STYLE ZAO waache, wakibwagwa watachoreka, wakiwa nae watachoreka...Idadi ya wapenzi itahesabika..

Miss Kim
 
Last edited by a moderator:
Mnaachana bila kuonana na kuachana huko watu wanakuwa broken heart kweli hata msosi haushuki
 
Miss Kim

Kwa hiyo ww ukiachana na mtu unamblock kbs?

Mm kwny mtandao kuna pic za mke wangu na mwanangu...sijawahi kuweka pic ya demu wangu kbs lkn sijablock ma-ex zangu we stil communicate when necessary huwa siachani na mtu kwa shari.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo watu wanafanya majaribio kabla ya wakati,naamini kuwa kama unataka kuw ana mahusiano mazuri unatakiwa kumsoma mtu mle ujana kwanza taratibu kama miezi kadhaa au miaka then mkinogewa ndio mfikirie kusema tukatambulishane kwa wazazi lakini sio FB etc.
 
Binafsi kama mwanamke huwa linanishangaza sana hili jambo. Sitaki kuamini mpaka sasa bado hatujajielewa au hatutaki kujielewa au hatujui nini maana ya mitandao ya kijamii.
 
Kwa hiyo ww ukiachana na mtu unamblock kbs?

Mm kwny mtandao kuna pic za mke wangu na mwanangu...sijawahi kuweka pic ya demu wangu kbs lkn sijablock ma-ex zangu we stil communicate when necessary huwa siachani na mtu kwa shari.

Asante kwa mtazamo wako mkuu.Kwenye post sijajitolea mfano wangu ila nimezungumzia mambo yanayotokea katika jamii haswa kwenye hii mitandao ya jamii. Nakubaliana na ww kwamba kuachana sio mwisho wa kuwasiliana ila kwa hawa wadogo zetu na dada zetu wengine wamegeuza social networks kama sehemu zao za kujinadi, utakuta mtu kila alifanyalo ataliweka humo,ndo maana na mm nimewashangaa kwa sababu hayo si mambo.
 
ahaha dada umenkumbusha nilikua na rafiki yangu facebook jina kapuni yaaani yule dada alikua kutwa my husband this my husband that bla blaaa kibao my wakwe my mavi my ushuziiiii ila tatizo n moja tu kujua mapenzi ukubwani nako kunachangia sio kila ukionacho lulu na ulimbukeni tu umetujaaa wakimwaga hao hao kuwaponda walio kua nao kana kwamba si wao walikua hawapost ovyo ovyo
 
Teh teh teh....kama huna mbio tangulia mbele:A S wink:.
 
ahaha dada umenkumbusha nilikua na rafiki yangu facebook jina kapuni yaaani yule dada alikua kutwa my husband this my husband that bla blaaa kibao my wakwe my mavi my ushuziiiii ila tatizo n moja tu kujua mapenzi ukubwani nako kunachangia sio kila ukionacho lulu na ulimbukeni tu umetujaaa wakimwaga hao hao kuwaponda walio kua nao kana kwamba si wao walikua hawapost ovyo ovyo

Unakuta mtu kapata mpenzi hata mwezi haujaisha ila tayari keshabadili jina lake huko Facebook na IG anajiita MRS flani, picha za mahaba niue haziishi humo, kila walifanyalo lazima jamii tufahamishwe, inatia huruma kwa kweli kwa sababu unakuta ni watu wazima na akili zao ila hawajitambui! jamani wanawake tuamke! Think of the Legacy you will leave behind when you are gone, what will your family & children think of you when they get to see how you used to live your life? Ukifanya jambo changanua kwanza faida na madhara yake and think in long terms!
 
Back
Top Bottom