Mahusiano mtandaoni: Je, yanafaa au hayafai

Mahusiano mtandaoni: Je, yanafaa au hayafai

sinza kwetu

Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
29
Reaction score
23
Mitandao hii ya kijamii imekuja na mambo mengi ikiwemo mahusiano. Watu wanakutana, wanachangia mada, wanaelewana, mwisho wanatafutana kuonana, na mahusiano yanaenda nje ya mitandao.

Tumeshuudia mitandao kama Jf ikiwezesha watu kuwa marafiki, watu kuwa wapenzi na pia kuwa washirika wa kibiashara au kazi.

Lakini mahusiano haya pia yamesababisha uadui, majuto, ugomvi, visasi, uchafu wa tabia, ukahaba, magonjwa, utapeli na mengineyo.

Kuna wanaoitumia vizuri mitandao ikawafaidisha mfano wakapata fursa za biashara, wakapata wenza wa maisha na wakaishi na wenza wao kwa furaha na amani, wakapata marafiki wa kweli, wakaeleza mambo yao kupata ushauri na kutoa ushauri.

Lakini wapo wanaoitumia vibaya mitandao kwa kueneza chuki, husda, umbeya, majungu, kufanya ufuska, kuwinda wanaume/wake za watu, kuchonganisha members, kujifariji kwa kuigiza maisha yasiyo ya kwao, kugawa watu makundi huku wakijifanya wao ndio wazuri kumbe ndio wabaya hawafai ata, kuwapakazia wenzao ubaya, kufanya utapeli wa mapenzi mpaka mali. Na bahati mbaya mpaka wanaume nao wameingizwa kwenye mkumbo huu mbaya unaoendelea.

Je, mnaonaje haya mahusiano mitandaoni.. Yanafaa kutumiwa na watu kwenye real life au kutumia mitandaokuchangia na kupata tu taarifa na habari inatosha kisha kuendelea na mambo yako??

 
Wewe mwalimu ndio umeamua kuandikia wino mwekundu? Watuumiza macho bhana....

Btw nice topic
 
Kwenye maisha kuna umuhimu wa kuweka mipaka, hata mitandaoni pia. Si kila mtu anataka kuonana na watu mitandaoni. Wengine hupenda kuja hapa anonymously na kuchangia au kusoma yale ambayo kwenye jamii inakuwa ngumu kuyaona. Wapo wanaokuja kuwinda na kufanikiwa. Lakini wengine ni suala la burudani kama kusoma magazeti.
 
big_in please usipendelee kutumia rangi nyekundu kama unaandika marefu hivyo, nyekunde ni rangi ya kusahihisha tu maana inaumiza macho ya msomaji, ninashauri tu mkuu. Peace.
 
Last edited by a moderator:
big_in please usipendelee kutumia rangi nyekundu kama unaandika marefu hivyo, nyekunde ni rangi ya kusahihisha tu maana inaumiza macho ya msomaji, ninashauri tu mkuu. Peace.

Mkuu sio mm
 
Last edited by a moderator:
binafsi imemsaidia sana nimeendelea mno,pili mtaani/job naonekana bongea mtu nina mapoint kumbe comment/threads za humu zinaaansaidia sana.
pia nachoweza kusema hata ule mda wangu wa ziada baada ya kuongea na watu home/ofissini natumia kuingia mitandao ya kijamii.
Nachoweza kusema my phone&tablets are my best friends.(BFF'S)
 
Inategemea unavyo yatumia ila yote yana uzuri wake na ubaya wake....
 
Kila kitu Duniani kina Hasi na Chanya kwa wakati huo huo , ukiwa chanya utavuna chanya tu , Hta wanaokutana kwenye Majumba ya Ibada nao wanakutanaga na Matapeli vile vile , Binafsi Mitandao ya Kijamii ( sio JF) Imenipatia Marafiki wa Jinsia yangu lakini , na Tumekuwa Marafiki ....wa mawasiliano ya hapa na pale sio kukutana viti Virefu Nope, au kuhadithiana mambo ya Mahusiano Nope, Maisha tu kila mtu akiwa na Mipaka na Mambo yake .....Ila kwa wale wanaotaka Urafiki wa KE na ME wanapaswa kuwa Makini Mno ! Makini kweli kweli ohoo!
 
Back
Top Bottom