Mahusiano: Jinsi ya Kumfurahisha Mkeo

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo

1. Mapokezi Mazuri

Baada ya kurudi kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale palipowatenganisheni:
• Anza kwa maamkizi mazuri
• Anza kwa Assalaamu na tabasamu.
• Salaam ni Sunnah na ni duaa kwake (mkeo) pia.
• Mpe mkono na ziache habari mbaya mpaka baadae.

2. Maneno mazuri na makaribisho ya kufurahisha
• Chagua maneno mema na jiepushe na maneno mabaya.
• Shughulika nae unaposema au anaposema yeye
• Sema kwa ufasaha na rejea maneno inapohitajika mpaka afahamu/aelewe.
• Mwite kwa majina mazuri anayoyapenda, mfano Mpenzi wangu, honey (asali, tamtam), (habibty), swaaliha (mwanamke mwema), (mwanamke mrembo) n.k

3. Urafiki na maliwazo
• Tumia muda kuzungumza nae
• Mfikishie habari njema
• Kumbuka kumbukumbu zenu nzuri za kuwa pamoja.

4. Michezo na burudani
• Mfanyie mzaha na jiweke katika hali ya furaha
• Chezeni na mshindane katika michezo na mambo mengine.
• Mchukue kuangalia aina za burudani zilizo halali.
• Jiepushe na mambo mabaya katika kuchagua aina ya burdani.

5. Msaada katika kazi za nyumbani

• Fanya kile ambayo wewe mwenyewe unaweza/ unapenda kukifanya ili kumsaidia, hasa anapokuwa mgonjwa au amechoka.
• La muhimu kuliko yote ni kumuonyesha wazi kuwa unathamini/unashukuru jitihada zake katika kazi.
 
6. Kushauriana

• Hususan katika masuala ya familia
• Kumpa hisia kuwa maoni yake ni muhimu kwako.
• Kuyazingatia maoni yake kwa makini
• Kuwa tayari kubadilisha maoni yako kwa maoni yake iwapo yatakuwa ni bora zaidi.
• Mpe shukurani kwa msaada wake wa maoni.

7. Kutembelea wengine

• Chagua watu wenye malezi mema wa kufanya mahusiano nao. Kuna malipo makubwa katika kuwatembelea jamaa na watu wacha Mungu. (Sio kuwatembelea kwa kupoteza wakati)
• Kuwa muangalifu kuhakikisha tabia njema na nzuri wakati mnapowatembelea watu.
• Usimlazimishe kuwatembelea wale ambao yeye hajisikii raha kuwa nao.

8. Muongozo wakati wa kusafiri

• Muage vizuri na kumpa ushauri mwema
• Mtake akuombee dua/Sala
• Watake jamaa wacha Mungu na marafiki kuiangalia familia wakati wa kutokuwepo kwako.
• Mpe pesa za kutosha kwa mahitaji anayoweza kuhitajia
• Jaribu kuwa na mawasiliano nae ama kwa simu, e-mail (barua pepe), barua, n.k.
• Rejea haraka iwezekanavyo.
• Mchukulie zawadi
• Jiepushe na kurejea nyakati zisizotarajiwa au nyakati za usiku.
• Mchukue (safarini) ikiwezekana.

9. Msaada wa Kifedha

• Unatakiwa kuwa mtumizi kwa mujibu wa uwezo wake wa kifedha. Usiwe
• bahili na pesa zake (wala usiwe mfujaji).
• Unapata malipo kwa matumizi yote unayotumia kwa ajili ya kumkirimu (mkeo) hata kwa kipande kidogo cha mkate ambacho unamlisha kwa mkono.
• Unahimizwa sana kumpa kabla yeye hajakuomba.


10. Kunukia vizuri na Kujipamba mwili

• Kunyoa nywele za utupuni na kwapani.
• Daima uwe msafi na nadhifu.
• Jitie manukato kwa ajili yake (mkeo)
 
11. Jimai (Tendo la ndoa)

• Unawajibika kulifanya mara kwa mara iwapo huna dharura (ugonjwa n.k)

• Uanze kwa dua zilizo sahihi.
• Umuingilie katika sehemu iliyo sahihi tu (sio sehemu ya nyuma)
• Uanze kwa vitangulizi (vya jimai) ikiwa ni pamoja na maneno ya mapenzi.
• Uendelee mpaka umtosheleze hamu yake.
• Mpumzike na mfanyiane mzaha mnapomaliza
• Epukana na jimai wakati wa damu ya mwezi kwa sababu kufanya hivyo ni kusababisha matatizo ya kiafya.
• Fanya chochote unachoweza kuepuka kuharibu kiwango chake cha haya alicho nacho (haya na staha) mfano kuvua nguo pamoja badili ya kumtaka avue yeye mwanzo huku ukiwa unamuangalia.
• Epuka wakati wa jimai mkao ambao unaweza kumuumiza mfano kumgandamiza katika kifua inayopelekea kumzuilia pumzi, hususan iwapo wewe ni mzito.
• Chagua muda muwafaka kwa jimai na uwe unamjali kwani wakati mwengine anaweza kuwa ni mgonjwa au amechoka.


12.
Kudhibiti Siri

• Jiepushe na kutoa habari za siri mfano wa siri za chumbani, matatizo yake binafsi na masuala mengine ya kibinafsi.



13.
Kuonyesha Heshima kwa familia yake na arafiki zake

• Mchukue katika matembezi kwa familia na jamaa, hususan wazazi wake.

• Waalike kumtembelea na wakaribishe.
• Wapatie zawadi kunapokuwa na jambo maalum (kama sikukuu)
• Wasaidie wanapokuwa na haja kwa msaada wa fedha, nguvu, n.k.
• Endeleza uhusiano mzuri na familia yake baada ya kifo chake iwapo atakufa mwanzo. Pia kwa hali kama hii mume anahimizwa kutoa kile ambacho yeye (mke) alizoea kutoa wakati wa uhai wake kuwapa rafiki ya jamaa zake.

14.
Mafunzo ya Imani ya dini na Kumshauri kwa kumrekebisha

Hii ni pamoja na:

• Misingi ya Imani yenu
• Haki na wajibu wake
• Kusoma vitabu vya imani ya dini yenu
• Kumhimiza kuhudhuria mafunzo ya iamani yenu
• Hukumu za imani yenu zinazowahusu wanawake
• Kumnunulia vitabu vya dini na kaseti kwa ajili ya maktaba ya nyumbani.
 
15. Wivu unaokubalika
• Hakikisha kuwa anavaa vizuri, mavazi kamili anapotoka nyumbani.
• Usimruhusu kuchanganyika ovyo na wanaume wasio- nduguzake.
• Jiepushe na wivu uliozidi mno. Mfano wake ni kama:

1. Kulichambua kila neno na sentensi asemayo na kuyajaza maneno yake kwa maana ambazo hakuzikusudia.
2. Kumzuia kutoka nje ya nyumba hata kama kuna sababu zinazokubalika.
3. Kumzuilia kujibu simu, n.k.

16. Subira na Upole

• Matatizo yanatarajiwa katika kila ndoa kwa hivyo hili ni jambo la kawaida, Lililo kosa ni majibizano ya kupindukia na kuyakuza matatizo mpaka yakapelekea kuvunjika kwa ndoa.
• Hasira lazima zionyeshwe pale makosa makubwa yanapojitokeza...
• Kumsamehe makosa anayokukosea .
• Usimpige pigo la nguvu la kumuumiza au kumpiga usoni au katika sehemu zilizo nyepesi kuathirika katika mwili wake.
• Jiepushe na kumdhalilisha kama kumpiga kwa kiatu, n.k.

17. Kusamehe na makaripio yanayofaa

• Mhukumu kwa makosa makubwa tu
• Msamehe makosa aliyokukosea .
• Kumbuka mazuri yote anayomfanyia kila wakati anapofanya makosa.
• Kumbuka kuwa kila mwanaadamu hukosea na umuwazie dharura mfano huenda amechoka, ana huzuni, yumo katika siku zake za mwezi au imani/mafungamano yake katika dini bado yamo katika kukua

• Jiepushe na kumgombeza kwa mapishi mabaya Iwapo umekipenda chakula, kula na iwapo hakukupenda wacha na husitoe maoni yoyote.
• Kabla ya kumuwekea wazi kuwa amefanya makosa, jaribu njia nyingine za mzunguko ambazo ni za hekima kuliko kumlaumu wazi wazi
• Epukana na kutumia jeuri au maneno yanayoumiza hisia zake
• Inapokuwa kuna ulazima wa kujadili tatizo subiri mpaka mnapokuwa faragha
• Subiri mpaka hasira zipungue kidogo, hii inasaidia kuweza kudhibiti maneno yako.
 
what a wonderful piece of advice,brother!!! i wish all of us were having this knowledge in our brains and kindness in our hearts
 
duh.....hapa lazima tui book mark hii .....kina baba majumbani waone!
 
Du,hapa ndoa itatulia kama maji na watoto watakaozaliwa - babu ubwa!!!!!!!!

Amazing family!
 
what a wonderful piece of advice,brother!!! i wish all of us were having this knowledge in our brains and kindness in our hearts
Kweli kabisa ndugu yangu.... mara nyingi mkazo ni namna ya kumfurahisha mume tu.Nimeiprint hii niwapatie akina kaka warekebishe mambo kwenye mahusiano yao.
THANK X-PASTER!
 
ndugu tuletee na jinsi ya kumfurahisha mumeo na wadada waone pia, manke inaonekana wanume wanasahaulika sana.

otherwisw, good advice mkubwa. tunashukuru sana
 
Kweli kabisa ndugu yangu.... mara nyingi mkazo ni namna ya kumfurahisha mume tu.Nimeiprint hii niwapatie akina kaka warekebishe mambo kwenye mahusiano yao.
THANK X-PASTER!

mmh, mama yangu, mimi siamini hapo nilipokoleza wino. mbona ukifanya utafiti hata hapa jamii forums pekee, utaona inasisitizwa sana kumfurahisha mke, kumsoma mke, hisia za mke, kumpenda mwanamke nk? au inasisitizwa wapi? labda utusaidie katika hilo.
 
mmh, mama yangu, mimi siamini hapo nilipokoleza wino. mbona ukifanya utafiti hata hapa jamii forums pekee, utaona inasisitizwa sana kumfurahisha mke, kumsoma mke, hisia za mke, kumpenda mwanamke nk? au inasisitizwa wapi? labda utusaidie katika hilo.

Ndugu yangu... ingekuwa ukisemacho ni kweli basi hizo kitchen parties zingepungua kama siyo kufutika.
 
Nimeunganisha na hii, japo ilikwisha toka kitambo.
X-PASTER said:
Kwa kuoana si huchukuana tu mke na mume, Bali mnachukua ulimwengu wenu mzima. Kuanzia hapo mpaka maisha yanu yote mke/mume wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako mpenzi.

Atashiriki katika nyakati zako nzuri, siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.

Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona ni macho yake. Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku, kitu cha mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye, na ukilala bado utakuwa unamuona katika ndoto zako. Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu wake mzima.

Inasikitisha sana katika jamii zetu kila nikizungumza na wana ndoa utasikia matatizo tuliyonayo yanafanana. Ni matatizo tanayowapata kutoka kwa waume zao au wake zao.

Ni hali ya kutisha sana na inafaa tuzingatie sana na wala tusiidharau, kwani utakuta hata watu waliosoma dini au kuelimika kwenye elimu mbali mbali pia wanaongozwa na jazba kwenye kutoa maamuzi. Sio vibaya kuongozana lakini iwe kwa njia ya kusomeshana au kukatazana pale pindi mtu anapotaka kukosea lakini utakuta sio hivyo kabisa.

Baadhi ya majumba yetu wanawake wengi wako hatarini kwa kukosa uongozi mzuri wa waume zao. Furaha inatoweka ndani ya nyumba kwa wanaume kukosa imani kwa wake zao na kujiona wao ni mabwana hawapaswi hata kutoa msaada mdogo unapohitajika. Je, nyumba kama hiyo itakuwa na mapenzi kweli au watu wataishi tu kuendeleza maisha kwa kuwa wamezaa, au kwa kuwaogopa viongozi wao wa dini na wazee wao?

Nilikutana na mama mmoja na katika mazungumzo naye, alikuwa akilia kwa uchungu na kusema:

"Sisi tumeolewa kwa ajili ya kuwa na furaha au kuwa ni wafanyakazi wao wa ndani hawa wanaume?"

Anasema yeye kazi yake ni kufua, kupiga pasi kulea watoto na kupika. Mume akiingia ni kula kulala na kutoka kwenda kwa marafiki tu, hana mapenzi hata ya kumwambia mkewe: "Mke wangu leo chakula kizuri au mke wangu umependeza" Ni neno dogo sana lakini lina athari kubwa sana ndani ya moyo wa mke wako.

Kwa upeo wangu naona yote haya yanasababishwa na ukosefu wa elimu na ubinadamu na kuto kuwa na huruma kwa mwenzi wako.

Wanaume hawapewi mafunzo ya kutosha wanapotaka kufunga ndoa jambo ambalo ni muhimu sana wafunzwe vipi kuishi na wake zao.

Kwa mwanaume inaonekana kama vile ni kutawaliwa pale mwanaume anapokutwa anaosha vyombo, kupika, kufua na kuogesha watoto nyumbani.

Jambo hili limeghafilikiwa kwa viongozi wa dini na hata wazee ambao aghlabu wao wanatoa mawaidha na mahubiri mengi kuwaonya wanawake zaidi kuliko wanaume kiasi ambacho kinawafanya wanaume wasitambue makosa yao na waache kufanya ihsaan na wawe na Rehma kwa wake zao. Siku zote nyumba ikivunjika anashutumiwa mke tu ilhali pengine ukorofi unaaza kwa mwaname mpaka kufikia hali ya kuachana.

Tuna jukumu ya kulifikiria jambo hili hasa wale ambao wanaishi nchi za nje (Ulaya na Marekani) kwani wanawake wanazidi kuwa wajeuri na kukosa nidhamu kwa vitimbi vya waume zao majumbani mwao.

Daima jaribu uwezavyo kuwa mtu mzuri kwa mkeo/mumeo kwa njia ya maneno na vitendo. Ongea nae, mchekee, tafuta ushauri wake, muulize juu ya mawazo yake, tumia wakati maalum na yeye na daima kumbuka kwamba mume/mke bora ni yule anaye jali familia yake.

Ni kawaida kwa wanandoa kuahidi kuwapenda na kuwaheshimu mwana ndoa mwenziwe mpaka mauti yawatenganishe. Naamini kwamba ahadi hii ni nzuri au ni bora kabisa, lakini haitoshi! Haitoshi kumpenda mkeo/mume tu. Lazima upende anachokipenda pia. Familia yake, anaowapenda yeye uwapende pia. Usiwe kama mwenzangu mmoja ambaye hakufurahiwa kuja kwa wazazi wa mke wake kukaa kwa wiki chache. Alimwambia wazi mkewe "Mimi siwapendi wazazi wako". Bila ya kusita mkewe alimtazama machoni kwa hasira na kusema, "Na wako pia siwapendi".

Mapenzi yasiishe hapa duniani tu, tunaamini kuna maisha baada ya mauti ambapo wale ambao walifanya wema katika dunia hii wataungana na wanandoa wenzio uko mbinguni (Peponi).

Basi ni jukumu letu sote kuziangalia tena na tena ndoa zetu na kuondoa tofauti ndogo ndogo zinazo jitokeza kila leo.
 
Jazakallah bikhairi. Haya ndio mambo ya kushare katika jamii kama hili, na sio kuweka mambo yasiyofaa na kuharibu maadili. Tumekee na somo lingine zaidi, hongera kwa kazi nzuri
 
Waislamu wenzangu tungeyafuata unayotufundisha hakika ndoa zetu zingekuwa ni zenye amani tele na hakika kila mmoja wetu angeonja pepo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom