Mahubiri ya Mwalimu Mwakasege - UDSM

Mahubiri ya Mwalimu Mwakasege - UDSM

Endelea kuniombea na Roho Mtakatifu akuongoze palipo na weakness Bwana aniponye.

Nami nitakuombea nawe pia maana tumeambiwa tusiache kuombeana hata ije siku ya Kristo Yesu. Ulipokwazika basi unisamehe.

Tunahitaji kumuomba Mungu kuliko tulivyowahi kufanya. Yapo mengi yanafanywa na viongozi wa dini yanalenga ukakasi ktk imani. Naamini hata wewe umeyaona.

Queen Esther

Nimekuwa nafuatilia maandiko yako Queen Esther kwa muda mrefu hasa unapoyaambatanisha na neno la Mungu. Nimeona waraka wako mrefu kwa Josephine ukimtia nguvu kwamba avumilie kwa vile anaonewa na yale ni mapambano ya kiroho.
Sipendi kuingia moja kwa moja kukupinga au kukuunga mkono, lakini niwe wazi tuu kuwa nimepata mashaka na huyo umtumikiaye kuwa ni yupi? Yaani kati ya "Yule ambaye ndiye" au "Yule ambaye ni yeye"
 
Usitishie watu na neno la Mungu. Neno la Mungu linajitetea lenyewe. Pia linaangalia nia ya moyo.

Mwl MWAKASEGE sio mtu wa imani potofu amuombee mtu mabaya. Hizo ni imani za naijeria ambazo baadhi yenu mnatembea nazo.

Mwl ni mfuasi kamili wa Kristo Yesu ambaye hata walipomwambia anatoa pepo kwa belzebuul hakuamuru moto ushuke nakuwalamba wahusika. Hata walipomtukana alisema Baba uwasamehe maana hawajui watendalo. Na hakutaka hata mmoja apotee bali wote waifikie toba ya kweli.

We shall know the truth and the truth shall set people free.

Nyie msioelewa mahubiri na kuzunguka huku,na huku ooo!! Mwalimu kahubiri hivi au kasema hivi ndio muache mara moja kupotosha injili.

RAIS ATAPATIKANA KWA MAOMBI, MSITUMIE JINA LA MWL MWAKASEGE VIBAYA KUHALALISHA MNAYOYATAKA.

Dada thibitisha hizi kauli zako na hasa hapo nilipobold

"Kampeni za mwaka huu viongozi wa dini ya KIKRISTO wameongoza kuvunja sheria na taratibu za uchaguzi kwa kuonesha bayana yule wamtakaye".

"Kuna viongozi waliolifanya hili wazi na wengine wametumia akili ila unaelewa moyo unakoelekezwa. Haya nimeyaona katika mahubiri ya safari hii ya Mwl MWAKASEGE"

acha kuzungukazunguka vinginevyo wewe ni sawa tu na Dr. Mihogo anatoa tuhuma za maaskof kupokea rushwa halaf ushahidi hana! Tuwekee ushahidi weka audio/video/au source nyingine ya tuhuma zako.
 
GT habari za asubuhi.

Kampeni za mwaka huu viongozi wa dini ya KIKRISTO wameongoza kuvunja sheria na taratibu za uchaguzi kwa kuonesha bayana yule wamtakaye.

Hili linanikumbusha habari ya kuchaguliwa kwa mfalme Daudi kuwa mfalme wa Israel. Mambo yafuatayo yalijitokeza:-
1. Mungu alimtuma Nabii Samwel akampake mafuta mfalme wa Israel
2. Mungu alimtuma Nabii Samwel aende katika nyumba ya Yesse na kati ya vijana wake Mungu amemchagua mmoja kuwa mfalme.
3. Nabii Samwel alipowaendea wazee wa Bethlehem walistuka hata kumuliza Je kuna amani??? Na ndipo alipowaambia na tutoe dhabihu.
4. Wakati IBADA ilipoanza ndipo Nabii Samwel alipoanza kuchagua mfalme mpya kwa kufuata matamanio ya moyo wake na sivyo Mungu alivyotaka.
5. Mungu alimuonya Nabii Samwel asiangalie mwonekano mzuri, urefu wa mtu,nk kwani Mungu haangalii hayo.
Mungu haangalii kama mwanadamu anavyoangalia, haijalishi ni Nabii, Mtume, Mwalimu au Askofu.
6. Tabia ya Mungu ni kuangalia NIA YA NDANI (For The Lord does not see as man sees; for man looks at the outward appearance, but The Lord looks at the HEART) statement of fact.
Tafsiri - Mungu haangalii vile mwanadamu anavyoangalia, kwani mwanadamu anaangalia mwonekano wa nje lakini Mungu anaangalia MOYO).
7. Hivyo basi haijalishi nani katabiri nini, nani kahubiri nini? nani kasema nini. Bado mpango wa Mungu na kusudi la Mungu kwa Tanzania litasimama.
8. BWANA HUYABATILISHA MASHAURI YA MATAIFA, HUYATANGUA MAKUSUDI YA WATU, SHAURI LA BWANA LASIMAMA MILELE, MAKUSUDI YA MOYO WAKE VIZAZI NA HATA VIZAZI.
9. Mwisho tunaona Nabii Samwel akiulizia iwapo kuna kijana mwingine wa Mzee Jesse, na ndipo Daudi akachaguliwa kuwa mfalme.
10. Daudi hakuwa amejiandaa hata kidogo kuwa mfalme, bali ulikuwa ni mpango wa Mungu mwenyewe.

HITIMISHO
Viongozi wa dini wameamua waziwazi kutuhamasisha tumchague mtu fulani kuwa Rais wa 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Viongozi hawa wamesahau wajibu wao kutuongoza kuomba ili Mungu amchague yule aliyeupendeza moyo wake.

Kuna viongozi waliolifanya hili wazi na wengine wametumia akili ila unaelewa moyo unakoelekezwa. Haya nimeyaona katika mahubiri ya safari hii ya Mwl MWAKASEGE.

Jambo hili sio geni hata Nabii Samwel alifanya haya haya na mwisho wa siku Mungu aliyakataa mapendekezo ya Nabii Samwel na ndipo Daudi akawa mfalme wa Israel. TENA AKAWA THE BEST LEADER BAADA YA WOTE WALIOMTANGULIA KUBORONGA.

KWA MAANA HIYO BASI, WATU WOTE TUINGIE KWENYE MAOMBI YA TOBA NA TUMUOMBE MUNGU ATUPE RAIS ALIYEUPENDEZA MOYO WAKE. USISAHAU KUSINDIKIZA MAOMBI YAKO NA SADAKA. Viongozi wa dini tuelekezeni kwenye maombi na sio kwenye majina ya watu. Let the will of God prevail.

EE MUNGU TUSAIDIE. EE MUNGU IBARIKI TANZANIA. EE MUNGU TUPE DAUDI.

QUEEN ESTHER

-------------------------------------------------------------------------

Ukisoma andiko langu vizuri UTAELEWA. Sina sababu ya kumchafua mtumishi wa Mungu Mwl. MWAKASEGE. In fact yeye ndie aliniombea ujazo wa Roho Mtakatifu.

Fanya utafiti wako utagundua majority ya wanaohudhuria mkutano wake tangu mwanzo wanatoka na majumuisho kuwa Mwl. anaonesha bayana kwamba chaguo ni Mhe. Lowasa. Jitahidi kufanya ka research kadogo utanielewa.

Inawezekana kuna haya yafuatayo:-
1. Mwalimu anatumia lugha ngumu watu hawamuelewi.
2. Inawezekana ana kundi la wasikilizaji wanywa maziwa na yeye anawapa MIFUPA.
3. Ni vizuri akatumia lugha nyepesi kwa audience aliyo nayo, naamini Roho Mtakatifu atamsaidia.
4. Mimi ni mmoja wa wanaomuombea ktk mahubiri yake. We pray for the guidance of the Holy Spirit and eloquent speech.

Mwisho ni vizuri kuliweka hili wazi ili ijulikane bayana kuwa MWL MWAKASEGE HANA JINA LA MGOMBEA.
Wote wanaopotosha hili kupitia mitandao ya kijamii na maofisini waache mara moja. Sisi yetu ni maombi Tanzania impate Daudi.

Asante kwa ushauri.

Queen Esther
Maelezo meengi kumtungia uongo mtumishi.Laana huwa mnazitafuta.Mtumishi yupo fair kabisa na katumia hekima ya Mungu labda useme ukweli unakuchoma
 
Laana isiyo haki haimpigi mtu.
Ni mungu pekee anayejua kilichomo ktk moyo wa mwl. Mwakasege na ndani ya moyo wangu hata nikaweka hili bandiko.

ni ukweli upi huo unaosema umenichoma????

queen esther

maelezo meengi kumtungia uongo mtumishi.laana huwa mnazitafuta.mtumishi yupo fair kabisa na katumia hekima ya mungu labda useme ukweli unakuchoma
 
Mhhh dada semina za mwl zinahudhuriwa na watu wengi sana physically na via other means huo utafiti na conclusion yako uliyokuja hapo JF sidhan kama ulijiuliza maswal mazito kabla ya kupost hivi huo utafiti umefanya kwa watu wangapi mpaka uwe na authority ya kuja jamvin na kusema hayo uyasemayo.

Unaposema watu hamwelew una uhakika gani ina maana wewe ndiyo kiroho chako kiko juuu sana yaan unataka kutuaminisha kuwa roho mtakatifu anayemtumia mwl yeye hilo la watu kuelewa/kutoelewa halioni so amekutumia wewe kuja kutueleza humu jamvini!

Mwanzon umemtuhumu mwl kwa kusema hivi "Kuna viongozi waliolifanya hili wazi na wengine wametumia akili ila unaelewa moyo unakoelekezwa. Haya nimeyaona katika mahubiri ya safari hii ya Mwl MWAKASEGE".

Then ulipoona umeshukiwa kama mwewe ukaja hivi "Mwisho ni vizuri kuliweka hili wazi ili ijulikane bayana kuwa MWL MWAKASEGE HANA JINA LA MGOMBEA"

Kumbe ukweli unaujuaa eeeh sasa motive behind ya hicho ulichopost ilikuwa ni nini? adui alikuingilia au? kaza mwendo dada ila jifunza kutokana na hili ulilofanya leo dini/imani ni issue sensitive sana unaweza ukafanya kitu ukazani unajenga mwili wa kristo kumbe.........
 
Huyu dada mwenye hii thread sidhani kama anajielewa na anaelewa anachoandika.. Someni heading na contents zote anajichanganya changanya mwenyewe..

Hopeless.. Usitumie dini kuficha ubovu.
 
Laana isiyo haki haimpigi mtu.
Ni mungu pekee anayejua kilichomo ktk moyo wa mwl. Mwakasege na ndani ya moyo wangu hata nikaweka hili bandiko.

ni ukweli upi huo unaosema umenichoma????

queen esther

Umenena vema.Mungu anakijua kilichomo moyoni mwako.Nadhani tumemaliza.Topic closed
 
Maelezo meengi kumtungia uongo mtumishi.Laana huwa mnazitafuta.Mtumishi yupo fair kabisa na katumia hekima ya Mungu labda useme ukweli unakuchoma

Mwambie Zion Daughter yaani Queen Esther amekuja kindakindaki kabisa kutoa tuhuma kwa mwl Mwakasege/viongozi wa dini ya kikristo eti wanavunja sheria na taratibu za uchaguzi! halaf watu wanamwambia ukwel kuwa kakosea anakuja na maneno ohh watu hawamwelewi mwalimu, mwl ana watu wa ngazi ya maziwa yeye anawapa mifupa.Hivi kweli Mungu amlete mtumishi wake amuandalie semina ya siku zoooote 8 halafu Mungu huyohuyo asiweke namna ya aliowakusudia kuweza kuelewa neno lake! Ina maana Mungu hajui anachokifanya?

Ahh mpendwa huyu ni kati ya wapendwa wajivuni niliopata kuwasoma!! yaan anataka kutuaminisha kuwa somo hili yeye kalielewa vizuri kweeeeeeeeeeel kuliko walio weeeeeeeeeeeng anyway ni faida kwa mwili wa kristo.
 
.
Sasa na wewe ulivyototolea mfano wa Daudi/Samweli ulishindwa nini kutofautisha kati ya uteuzi na uchaguzi?
zamani za Daudi hawakupiga kura bali zetu tunapiga kura.
Hapa Ester sii kujaribu kutuchezesha kwata kisaikolojia?
Usijaribu kufanya hivyo tena p/se mamie!!
.
Katumwa na shetani?
 
Ommy Mkomwa
,
Asante sana kwa mchango wako.

Kabla ya mistari uliyonukuu naomba nikukumbushe kuwa Mungu alimkataa Sauli. Tena aliwaonya wana wa Israel kwamba huyu mtu atatembea mpaka na wake zenu. Wao wakasema potelea mbali. Kumbuka Nabii Samwel alipomlilia Mungu kuwa watu hawa wamekataa maagizo ya Mungu; Mungu akamwambia hawajakukataa wewe bali wamenikataa mimi.

Mambo halipokuwa mabaya wakarudi kumlilia Mungu. Mungu ha kumchagua Saul soma hiyo habari kuanzia mwanzo UTAELEWA.

Asante kwa mchango mzuri.

Queen Esther

.
Contradiction:
kwani aliyemtuma Samweli kumpaka Saul mafuta ni nani?
Au kumchagua Sauli mfalme wa waisrael walimchugua kwa kura zao ama njia ipi?
kitu kingine cha kujiuliza hapa je kusudi la Mungu linashindwa? na kama halishindwi kwa nini isiwe ufalme wa sauli ni kwa ajili ya kusudi lake na isingeweza kuwa vinginevyo?
.
 
umenikera kabisa (Queen Esther) serious kuleta hisia zako hapa badala ya kile ulichokisikia ungenyamaza kimya ungeonekana WA maana zaidi kuliko hiki ulichokiandika
 
umenikera kabisa (Queen Esther) serious kuleta hisia zako hapa badala ya kile ulichokisikia ungenyamaza kimya ungeonekana WA maana zaidi kuliko hiki ulichokiandika

WENYE KUNIELEWA WAMENIELEWA SIO LAZIMA NA WEWE UWE MMOJA WAO.

Mambo ya Rohoni hutambulikana na watu wa Rohoni.

Queen Esther
 
umenena vema.mungu anakijua kilichomo moyoni mwako.nadhani tumemaliza.topic closed

amen zion daughter

naungana na wewe topic closed. Message sent kwa wahusika na wapotoshaji wote.

Mwl mwakasege hana mgombea. Agenda yake ni maombi mungu atupe rais aupendezaye moyo wake.

Kusudi la mungu litimie; ufalme wake uje duniani kama mbinguni. Amen

kwaherini.

Queen esther
 
Mtu yeyote anayo haki kumtakia kila la heri mgombea anayemvutia,,,Ktk hayo mahubiri ya Mwakasege hajamtaja mtu yoyote japo uelekeo upo kwa Lowassa kutokana na namna anavyoandamwa,,,pale anaposema Daudi hakujiandaa kwa madaraka anamanisha hata wanaonekana kama inexperienced ktk siasa (ACT,TLP)wanao uwezo Mungu akiamua kuwatumia...anyway,Mungu ukimuomba mkate hawez kukupa jiwe,,,Mungu anajua watanzania tunahitaji nn,,,Nchi yetu haijalaaniwa,kwamba katupa rasilimali nyingi afu tuishiwe kuchekwa na majirani kwa umaskini,,,Mungu atupiganie watakaojarbu kupingana na matakwa ya watanzania WAAIBISHWE MCHANA KWEUPE...AMEN!

HAPANA kabisa,anaposema Daudi hakujiandaa kwa Madaraka anamaanisha Magufuli.Kwasababu Lowassa alijiandaa Tangu 1995,2005 na hata mwaka huu alivyokatwa alijiandaa na Uchu yaani kuonyesha anauhitaji Uraisi!Hivyo Kati ya Vyama vikubwa a 2 CCM na Chdema Mtu ambae hakujiandaa au kuandaliwa kutokana na ulivyosema ni Magufuli na Sio Lowassa.Lowassa alijiandaa sana.Kwa hiyo mwakasege anamzungumzia Magufuli ndo anaweza kuchaguliwa!
Kataa hili kwa hoja!
 
Sasa wewe ulitaka asiseme maono yake? Kwahiyo wachungaji wa mungu wakipata upako wa kuonyeshwa jambo wataka wakae kimya na wasikueleze kwamba mama jusi wamemtokea na kumwambia atazaliwa mtoto kwenye zizi la ng'ombe. Neno kwenye zizi la ng'ombe moja kwa moja lilimuelezea mtu huyo ajaye kwani si wote wenye kuzaliwa kwenye mazizi ya ng'ombe labda tu wewe mtoa mada. The same hapa. kama Mwakasege ametoa ishara zenye kufanana na zizi la ng'ombe kwa Lowassa sioni wapi ametumia udini kumtaka. Nenda kafanye kampeni wacha habari za kupinga maono ya watumishi wa mungu. Hakuna mahali imeandikwa kwamba wahubiri wasitoe ishara wazipokeazo toka kwa mungu kipindi cha uchaguzi.
 
Acha kuwalisha maneno watumishi wa Mungu! Siasa isikutoe ufahamu kiasi hiki!

Mkuu ccm imevurugikiwa, wote wenye maslahi wanajaribu kukioa chombo chao amabacho very soon inazama, jana kwa mara ya Kwanza kabisa namwona mzee warioba amevaa shati la ccm yuko jukwaani kumnadi mgombea wao.
 
Mungu kamwe hawezi kukubali Fisadi Lowasa na Genge lake waongoze hii nchi, fisadi Lowasa alishakataliwa na Mungu tangu siku ya kwanza, kwanza ni tangu siku alipozaliwa na ndiyo maana hata Mungu kamlaani anatembea kama Mtu wa miaka 90 wakati hata miaka 65 hajafikisha, na bado pigo la mwisho ktk kwa Mungu kwa fisadi Lowasa linakuja na karibuni ataanza kutembelea tumbo!

TanZania ni mpango wa Mungu na siku zote Mungu ataiepusha TanZania yetu na Waovu kama fisadi Lowasa na Genge lake, itabakia kuwa hivyo mpka mwisho wa Dunia!

Ndg nafikiri hujielewi kabisa nakukumbusha tu kidogo Kashfa ya escrow ni ya mtu unaye mwita fisadi Lowasa?,Epa na nyingine nyingi ambazo humevaa miwani mbao hutaki kuona .Wale mawaziri walioachishwa kazi sio mafisadi? Naomba jibu.
 
Mtumishi nae anaweza kuwa na mapenzi yake tu kama ulivyo wewe na mimi ila ukweli unabaki kuwa hutoingia na yeyote kwenye chumba cha kura utakuwa wewe na akili yako tu...Na nadhani kila mtu ameshamjua atakaeenda kumpigia kura siku hiyo...Na ni kweli tumshirikishe Mungu katika hili ila naye ametupa akili na uelewa wakuweza kufanya maamuzi sahihi .

Ninaamini Mungu hawezi kuruhusu huyu shetani aendelee kuitawala Tz, Kashamteua mteule wake atuvushe hapa lilipotufikisha hili jinamizi.
 
Napenda mtu anayejibu kwa hoja na sio ushabiki. Je Saul alikuwa chaguo la Mungu???

Queen Esther
Usiletee dini ndani ya siasa .na wasiwasi kama unapepo na sio roho mtakatifu..juzi tuu hapa umetuumu Lowasa kuingiza siasa kwenye dini.Mara hapo hapo unatuletea dini kwenye siasa .shindwa na ulegee pepo mchafu..na Lowasa ndio raisi wetu
 
Ndg nafikiri hujielewi kabisa nakukumbusha tu kidogo Kashfa ya escrow ni ya mtu unaye mwita fisadi Lowasa?,Epa na nyingine nyingi ambazo humevaa miwani mbao hutaki kuona .Wale mawaziri walioachishwa kazi sio mafisadi? Naomba jibu.

Muhusika Mkuu wa escrow ni fisadi Rugemalira ambaye yuko genge moja la fisadi Lowasa, ukisikia fisadi Lowasa anasema ,,marafiki zangu" ujue anawaongelea akina Rugemalira, Rostamu Aziz, Karamagi &Co. kwa kifupi hakuna ufisadi wowote mkubwa hapa nchini ambao fisadi Lowasa na Genge lake hawahusiki kwa namnA moja ama nyingine na ndiyo maana CCM walimuondoa hata Balozi wa Marekani alisema na nchi yake inamjua Lowasa kama fisadi mkubwa hapa nchini!
 
Back
Top Bottom