Mahojiano ya polisi na Sheikh Ponda Issa Ponda

Kuna haja ya uchunguzi wa kina juu ya nani yupo nyuma ya pazia juu ya hili la akina Ponda & Co.
 
Ponda amefikishwa Mahakamani leo na bado hajapandishwa kizimbani ila cha kufurahisha huyu leo lazima alale Segerea au keko, hili nimethibitishiwa na PP wa pale Mahakamani, hakuna dhamana kwa watu kama hawa.

Source: mimi mwenyewe
Kiongozi wa Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda pamoja na wafuasi wengine waliokamatwa, leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka ya madai mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashawishi baadhi ya Waislam kuvamia eneo la Kiwanja katika eneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam, kuwashawishi Waislamu kutojitokeza katika zoezi la Uandikishaji katika Sensa ya Watu na Makazi.

Watuhumiwa hao wamerudishwa rumande wakisubiri taratibu nyingine.

CHANZO: TBC Habari za Saa 7 mchana​

- Wamesomewa mashtaka matano na wote 50 wamerudishwa rumande baada ya kukataliwa dhamana
 
Hii thread ifungwe sasa, Huyu Gaidi Ponda tayari ameshapelekwa mahakamani na leo atalala jela hakuna dhamana na ameandaliwa kidume cha kumbikili.
 
وقف النكات والمتدينين، وأنا هنا أنا أكتب ليس فقط الأكاديمية العربية

Hoya, hi ndo nini hapo...
 
Au akabidhiwe kwa Marekani kama vile waingereza juzi kati walivyompeleka yule sheikh raia wao akashtakiwe USA. Guantanamo miaka 10+ bila kesi, waterboarding nk.
 
Gaidi? Usimpe umaarufu asiostahili. Tusiwavike watu vilemba vya ukoka wakajiona na wao wapo.
 
mkuu kuna mbingu ya segerea usifurahie mtu kulala segedance uliza mh wetu wa gari nye ***** hadi simu anapewa nini huyo kulala
wamhukumu mapema alazwe mungu alipomtafutia wampe maji machafu anywe waombe kupelekwa hospitalini ma dkwakamalize uko kazi akirudi nje siku tatu mmemsahau
 
Matusi ya nini wana JF, je mnajua maana ya gaidi??... Mnatakiwa mtoe arguments na sio matusi, otherwiz we will prove failure...
 
Huyu Gaidi amefikishwa Mahakamani leo na bado hajapandishwa kizimbani ila cha kufurahisha huyu leo lazima alale Segerea au keko, hili nimethibitishiwa na PP wa pale Mahakamani, hakuna dhamana kwa magaidi kama hawa.

Source: mimi mwenyewe

Rekebisha lugha! Sheikh hawezi kuwa gaidi1 Huyu ni mhuni tu. Sheikh ni mtu wa Mungu hawezi hamasisha fujo, uvunjifu wa amani
 

ALHAMISI, OCTOBA 18, 2012 05:06 NA BAKARI KIMWANGA, DAR ES SALAAM

*Atiwa mbaroni Dar, Waislamu wachachamaa
*Watawanywa kwa mabomu ya machozi
*Wakamatwa na mapanga, majambia na shoka
*Zanzibar nako kwachafuka, mabomu tupu

KAULI ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, zimeonekana wazi kuivuruga Serikali, huku polisi wakilazimika kutumia mabomu ya machozi, kutawanya waumini wa Kiislamu waliovamia Kituo cha Polisi cha Kati, ili kushinikiza Ponda aachiwe.

Tukio hilo, lilitokea jana saa 8 mchana, baada ya kundi kubwa kuvamia kituoni, ambapo polisi walilazimika kuwafukuza kwa kutumia mabomu ya machozi.

Kutokana na jeshi hilo, kujipanga vizuri huku likitumia magari yenye namba za usajili PT 2081, PT 1848, PT 2103, walifanikiwa kuzunguka mitaa yote ya katikati ya Jiji kuimarisha ulinzi.

Akizungumza na MTANZANIA, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kusema wanaendeleza msako wa watu walioratibu maandamano hayo.

Alisema katika tukio hilo, watu kadhaa walitiwa mbaroni, akiwamo raia mmoja wa Rwanda aliyekutwa na panga, shoka ndogo na majambia.

"Tumefanikiwa kukamata watu kadhaa na tumewakuta na vitu mbalimbali vya hatari, vikiwamo mapanga, majambia na mashoka madogo madogo…hii inaonyesha wazi, walikuwa wamejiandaa kufanya fujo," alisema Kova.

KUKAMATWA PONDA

Akizungumza kukamatwa kwa Ponda, Kova alisema, jeshi hilo lilimtia mbaroni Sheikh Ponda, kwa madai mbalimbali yakiwamo madai ya kuvamia kiwanja cha Markaz Chang'ombe, pamoja na kumtishia maisha Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba.

Alisema hatua ya kukamatwa Sheikh Ponda, inatokana na kufanya makosa mbalimbali, ikiwemo kuchochea vurugu na amani nchini.

Alisema Sheikh Ponda, aliongoza kundi la wafuasi wake na kuvamia Kiwanja namba 331/3/4 Block ‘T' eneo la Chang'ombe, ambayo ni mali ya Kampuni ya AGRITANZA na kufanya uharibifu wa mali mbalimbali.

Alisema uvamizi huo, ambao ulikuwa ukiongozwa na Sheikh Ponda, walifanikiwa kuteka eneo hilo, wakidai wanakomboa mali za Waislamu zilizouzwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), huku uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi hilo, ukibaini kiwanja hicho kina hati miliki namba 93773, ambayo ilitolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Alisema mbali na hilo, nyaraka mbalimbali zilitolewa pamoja na mikataba ya kuuziana, ikiwemo kubadilishana kati ya BAKWATA na kampuni ya AGRITANZA.

"Pamoja na kutiwa mbaroni Sheikh Ponda jana (juzi), majira ya saa 4 usiku, pia tumewakamata watu 38 katika eneo la Chang'ombe, ambao kati yao wamo wanawake saba na wanaume ni 31.

"Jeshi la Polisi, hata baada ya kuwaita viongozi wa BAKWATA, waliweza kuthibitisha makubaliano yao ya kisheria, ikiwemo kampuni ya AGRITANZA, kumiliki eneo hilo kihalali. Hivyo watu wote tuliowatia mbaroni, wakiongozwa na Sheikh Ponda, wanakabiliwa na shtaka la kuingia na kufanya uharibifu wa mali katika eneo hilo.

"Sambamba na kukamatwa kwa Sheikh Ponda, Oktoba 16, mwaka huu saa 4 usiku, karibu na eneo la maficho yake, ambapo aliletwa na pikipiki...polisi ilifanya oparesheni maalum ya kuwaondoa wavamizi katika eneo hilo linalomilikiwa na AGRITANZA.

"Pia Sheikh Ponda, pamoja na kufanya vurugu na hata kusababisha kuvurugika kwa amani jijini Dar es Salaam, jeshi letu limefanya uchunguzi wa kina na kubaini taasisi yake anayoiongoza ya Jumuiya na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, hajasajiliwa kwa msajili wa makampuni nchini, wala Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

"Amekuwa akifanya maandamano kinyume cha sheria na hata kutishia umwagaji damu Dar es Salaam, kipindi chote tulikuwa katika uvumilivu wa kufuatilia nyendo zake kila kukicha,...licha ya hali hii, Oktoba 12, mwaka huu, Ponda pamoja na wafuasi wake, walisababisha kuvunjwa makanisa usiku wa manane, uharibifu wa magari na wizi na upotevu wa vifaa katika makanisa… haya yote yameongozwa na Ponda na madhara yake ni makubwa.

Vitisho dhidi ya Mufti Simba

Kuhusu vitisho dhidi ya Mufti Simba, Kova alisema Sheikh Ponda, amekuwa akitoa kauli za vitisho zikiwamo za kukusudia kumng'oa madarakani, akiwa hai au amekufa jambo ambalo ni kosa kisheria.

Alisema katika kipindi cha miezi miwili sasa, Sheikh Ponda amekuwa akitoa matamko hayo, ambayo yanasababisha hofu kwa jamii.

"Sheikh Ponda, anachokifanya katu hatuwezi kuvumilia, kwani kuendelea kumuacha ni kuvunja sheria, amekuwa akiingilia uhuru wa mahakama kwa kudai watuhumiwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na kufikishwa mahakamani, waachiwe mara moja ndani ya siku saba.

"Moja ya kielelezo ambacho tumemkamata nacho, ni barua ya Oktoba 10, mwaka huu ambapo alitoa vitisho kwa mmiliki wa kiwanja namba 17/56, kilichopo eneo la Mchikichi Kariakoo na kudai kuwa, ni mali ya Waislamu," alisema Kova.

Kumkejeli Rais JK

Alisema kwa muda mrefu sasa, Sheikh Ponda, amekuwa akitoa vitisho na kuchochea chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

"Sheikh Ponda, amekuwa akihubiri na hata kufanya mihadhara inayochochea chuki dhidi ya Serikali na hata kutoa kauli za kumkeji Rais Jakaya Kikwete, …kila mmoja wetu, anatakiwa kutambua nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na sio kutoa vitisho kama anavyofanya Ponda," alisema.

Wafuasi wa Ponda

Kamanda Kova, alitoa onyo kwa makundi yanayoratibiwa na Sheikh Ponda, huku akiwataka wafuasi wake kujisalimisha wenyewe Polisi, kabla hawajatiwa mbaroni.

"Natoa onyo na kwa mujibu wa taarifa zetu, tunaelezwa kuwa, hivi sasa kuna vikundi ambavyo vinafanya kazi ya maandamano, huku wengine wakiwa wasaidizi wa Sheikh Ponda, tunataka wajisalimishe wenyewe," alisema Kamanda Kova.

ZANZIBAR

Habari zilizopatikana jana jioni kutoka mjini Zanzibar, zinasema kumezuka fujo kubwa, katika eneo la Mji Mkongwe, baada ya kuwapo taarifa za kukamatwa kiongozi wa Kundi la Uamsho.

Kiongozi huyo, Sheikh Faridi Hadi Ahmed, anadaiwa kukamatwa na watu wasiojulikana.

Hali hiyo, ilisababisha eneo lote la Mji Mkongwe, kugeuka uwanja wa vita, baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi kutawanya mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu.

Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 
Back
Top Bottom