Nini ni Dira ya Kabwe Zuberi Zitto kwa Tanzania?
Tanzania ambayo kila Mtu ana fursa sawa ya kujiendeleza na kuliendeleza Taifa bila vikwazo vyovyote. Tanzania yenye heshima mbele ya Mataifa ya dunia, wenye watu wanao thamini Utu wa binadam wote duniani, yenye watu werevu wanao tambulika nyumbani na kimataifa, na wenye siha njema. Mwono chanya kuhusu nchi yao na majirani wao. Napenda kuona Taifa imara na bora barani Afrika. Taifa lisilo na taswira ya ufisadi. Taifa la kujivunia. Inawezekana.
Kama leo ungechaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya katiba ya sasa ukiwa amekuta maadui wale watatu (ujinga, umaskini na maradhi) wakineemeka hasa wakiwa wamepata mwenzao ufisadi, ungetumia jeshi gani/mbinu gani kupambana na maadui hawa?
Kwanza kuibadili Katiba hiyo ingekuwa suala la kwanza maana huwezi kupambana na ufisadi kwenye Katiba ambayo ni mbaya.
Pili ningeimarisha sana miiko ya uongozi na kuweka bayana kwamba yeyote anayetaka uongozi wa Umma atumikie umma, biashara aweke pembeni. Hata nchi zilizoendelea zinafanya hivi (conflict of interest code). Hii ndio inaimarisha ufisadi.
Tatu, uwazi wa mali za viongozi, uwazi wa mikataba yote ya kunyonya rasilimali na uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.
Ukishaweka misingi hii na hasa misingi ya uwazi na uwajibikaji kazi ya kupambana na rushwa inakuwa rahisi sana. Hivi sasa tunashindwa kwa sababu hao wanaopaswa kupambana na rushwa wao wenyewe wana maslahi na wanazuia mabadiliko. I am anti status quo person all my life and we need just that.
Suala la mgongano wa maslahi nimeliandikia mara kadhaa na hata jana kuna makala kwenye RaiaMwema kuhusu suala hili. Pia niliandika muswada binafsi Bungeni kuhusu suala hili na niliuweka hapa JF napia kwenye blog yangu zittokabwe.com. Hili ni suala linahitaji sana msukumo ni kuondoa ufisadi nchini.
Kwanini Tanzania ni Maskini? Mkakati gani wa anaouona kuwa unaweza kutambua vipaumbele vya kuondokana na umasikini wa Tanzania?
Tanzania ni masikini kwa sababu viongozi wetu wamechagua tuwe masikini. Njia moja kubwa na ilio endelevu ya kutokomeza umasikini Tanzania ni kuwekeza walipo Watanzania wengi na kuwapa fursa za ajira na ujira, fursa za kuzalisha utajiri kwa kuongeza uzalishaji mali.
Umasikini wa Tanzania utaondoka kwa kuwa na Maendeleo Vijijini. Ili kupata rasilimali za kuwekeza vijijini ni lazima kuondokana na upotevu mkubwa wa rasilimali za nchi kutokana na matumizi mabaya (kama posho), ufisadi, wizi na udokozi, pia kuzuia ukwepaji mkubwa wa kodi. Kazi ndio kipimo cha Utu itakuwa ni kauli mbiu muhimu ili kurejesha ‘attitude' ya kufanya kazi badala ya kuwa Taifa la wanyemelea-kipato (rent-seekers).
Kama kijana, umetembea nchi kadhaa duniani, kwa muono wako ni wapi wananchi, viongozi, serikali na taifa kwa pamoja tunakosea katika kulisongesha gurudumu la maendeleo Tanzania?
Hatuna wivu wa maendeleo. Tumekata tamaa. Hatuna ‘ambition' za kuacha legacy kama walivyo kina Mahathir, kina Meles nk. Hatuna attitude ya maendeleo. Watu wenye madaraka hawana mawazo mapana, hawaoni mbali., na hawana constancy and consistency katika strategies zao za kuendesha nchi. Ukienda kwenye blog yangu soma a post imagine Tanzania utaona potential ya nchi hii.
Ikiwa ndani ya uwezo wako i.e tuchukulie umepata urais; ni njia gani ambayo unaweza kutumia kufuta na kumaliza Udini ambao unaanza kujidhihirisha kwenye siasa za Tanzania?
Udini ni state of mind. Tatizo Tanzania tumekuwa kwenye state of denial.
Malalamiko ya Udini katika nchi yameanza siku nyingi sana. Njia ni moja tu, Serikali kutoshughulika na masuala ya Dini na viongozi wa dini kutojiingiza kwenye siasa za vyama bila kupoka uhuru wao wa mawazo au wa kujiunga na vyama vya siasa. Ukiwa na Serikali inayotenda haki kwa watu wote bila kujali wana Sali au wanaSwali hapatakuwa na malalamiko haya.
Hii sio mara ya kwanza tunaona vurugu za kidini kwenye nchi. Kwani mmesahau suala la maduka ya nguruwe miaka ya tisini? Mmesahau suala la mwembechai la miaka hiyo hiyo? Mmesahau mauaji ya Arumeru? Muhimu ni Serikali kuwa imara kuhakikisha tunapiga vita ‘chuki' kisheria na kutenda haki kwa watu wote bila kujali dini zao. Udini ulivyo sasa ni kansa inayotutafuna kidogo kidogo. Nimeshuhudia mwenyewe udini mkali sana wakati wa kampeni mwaka jana Jimboni kwangu ulioendeshwa na dini zote kuu - Waislam na Wakristo kila mmoja kwa mwono wake.
Nimesoma jana makala ya MwanaKijiji kuhusu namna ya kushughulika na suala hili. Kuna haja ya kuzungumza kwa uwazi bila jazba suala hili. Ningekuwa ni Rais leo ningeunda Tume ya Ukweli na Maridhiano kujadili kwa uwazi na mapana yake suala la Udini. Tusipochukua hatua nchi hii itapasuka vipande. Haya mambo ya Gesi na Mafuta haya ndio yatatumika na maadui wa nchi yetu kutugawa.
Tuwe Makini sana. Tusione tu hizi vurugu kwa juu juu. Tuzungumze