JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,013
Napenda pia ifahamike kuwa mimi ni mmoja wa wanachama waanzilishi wa jukwaa hili na ninafurahi kuona limekuwa na kwa kweli its a force to reckon with.
- Hii ni changamoto kubwa sana kwa nchi yetu. Itikadi za kisiasa husaidia kunyoosha sera za vyama. Hivi sasa chama chochote chaweza kuwa na sera yeyote ile kwa kuwa hakuna uti wa mgongo ambao ni itikadi. Lazima vyama vijipambanue kwa itikadi zao. Kwa kukosekana kwa itikadi zinazoeleweka vyama vimekuwa kama 'electoral machines' tu. Kukosekana kwa itikadi kunafanya vyama kudandia masuala. Mfano juzi hapa mmesikia Mkutano Mkuu wa CCM umeazimia elimu iwe bure.1. Unalizungumziaje Ombwe la Itikadi Miongoni mwa Vyama vyetu vya Siasa, ambapo tangia mageuzi ya kisiasa na kiuchumi yaingie nchini, ni vigumu kutofautisha itikadi za vyama vya siasa - kinadharia na kivitendo, hasa ukizingitia ukweli kwamba kwa kila chama, sera na itikadi zinazouzwa au kutekelezwa ni za kiliberali, huku wananchi wengi (hasa vijijini) wakiwa hawana ufahamu juu ya madhara na faida ya itikadi hii ni nini.
Unaiongeleaje sera ya Majimbo ya CHADEMA?
Mkuu hilo halina shida... Hapa lengo ni majibu ya kina kwa maswali yote. Pamoja saana.Maswali marefu sana. Nitajibu kidogo kidogo.
- CCM imeshindwa kupambana na adui ufisadi, CHADEMA tunapambana na tutapambana na ufisadi kwa nguvu zetu zote. CCM inaamini katika soko holela, CHADEMA tunaamini katika soko linalojali. CHADEMA inaamini katika nguvu ya Umma, CCM inaamini katika nguvu ya Dola.Unaona tofauti ya msingi kati ya CCM na CHADEMA ni IPI?
Sijakiona badoNini kinakuvutia ndani ya CCM ambacho hakipo CHADEMA?
- Jamii imefaidika sana na kuwa kwangu CHADEMA. Kupitia Bunge na nje ya Bunge nimeweza kuisimamia Serikali kwenye mengi na hasa masuala ya rasilimali za Taifa kama madini na kufanikiwa kupata sharia mpya ambayo imetoa fursa kwa Watanzania kufaidika na utajiri wao wa madini. Mengi sana ninayofanya nikiwa CHADEMA nisingethubu kuyafanya ningalikuwa CCM.Bado unafikiri wewe kuwa CHADEMA ni tija kwa jamii kuliko kuwa Chama kingine mfano CCM?
Ndio Demokrasia.Unalizungumziaje suala la kuwa na utitiri wa vyama vingi vya siasa vinavyokula pesa za walipa kodi halafu havina tija wala mchango wowote kijamii zaidi ya kutufilisi, je kuna umuhimu wa kuifanyia sheria mabadiliko ili kuwe na limitation mfano, vyama vitatu tu?
Mkuu Zitto nashukuru kwa majibu yako kina kwa swali la kwanza, swali linalofuata
Mkuu Zitto nashauri jibu maswali yaliyo mengi kwa vipengele, kama vile majibu yanaweza gawiwa in 2 or 3 equal groups kwa jinsi mwenyewe utavyoona.Nitajibu tena kidogo kidogo maana hii peke yake ina maswali 13.
- Kutumikia chama chetu kwa nafasi nilizonazo.Nini kipaumbele chako cha sasa kama mwanachama wa CHADEMA?
- Chadema ni chama cha kitaifa. Kingekuwa chama cha kidini au kikabila kingefutwa. Katika uongozi wa Chadema unapata watu toka mikoa na kabila mbali mbali, pia watu toka dini mbali mbali. Diversity hii haipatikani katika vyama vingi humu nchini. Nadhani mtazamo huu unapandikizwa na watu ambao hawakipendi chama chetu na wanao ona chama kama threat kwa maslahi yao binafsi.Mkuu, ni kweli kuwa CHADEMA ni chama cha kidini/kikabila? Na kama ni kweli, tatizo hilo lishughulikiwe vipi? Kama si kweli, unaweza kuueleza umma wa watanzania una kauli gani juu ya mitizamo hii dhidi ya chama chenu?
CHADEMA ina demokrasia ya aina yake na wanachama tunaridhika nayo. The Party deploys for or against your wishes and every member must oblige a just deployment. Tuna utaratibu mzuri sana wa kujieleza na kutetea hoja zetu ndani ya chama, na baada ya watu wote kukubaliana tuna hakukusha tunasimama wote kwa kauli moja sehem zote tunapo wakilisha chama. Sio katika kupanga safu za uongozi tu, ni sehem zote za uongozi wa chama.Mh. Zitto, unaizungumziaje demokrasia ndani ya chama chako katika chaguzi, teuzi na kupanga safu za uongozi?
Huo mtazamo unaweza kutokana na kulinganisha Chadema na vyama vingine. Ieleweke kua Chadema ni chama tofauti na kina utaratibu wake. Katika chama chetu Viongozi wa mikoa na wa wilaya wana majukumu yao, na makao makuu pia yana majukumu yake.Kwanini CHADEMA haiwatumii viongozi wa Mikoa na Wilaya na badala yake inatuma watu toka makao makuu hata kwa mambo madogo madogo ambayo yangemalizwa na uongozi wa ngazi husika?
Kwa sababu jina lake liko wazi kabisa, M4C ni moja ya operesheni inayo fanikisha watanzania kujiunga katika chama huku wakijua kabisa kua malengo ni kuleta mabadiliko chanya.Mh Zitto, unazizungumziaje harakati za M4C na athari (impact) yake kisiasa na kijamii? Chama kimeweka taratibu gani nzuri za malezi kwa wanachama wapya wanaojiunga kwenye M4C, kama bado, huku si kusuka kamba inayoungua?
Ninashiriki sana kazi za kujenga chama. Nimeshiriki sana operesheni mbalimbali za chama. Nitaendelea kushiriki nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama.Inadaiwa hushiriki kikamilifu M4C, ni kweli? Nini kauli yako dhidi ya tuhuma hizi?
Hatujawahi kufanya utaratibu unaosema isipokuwa kwenye Urais mwaka 2005. Hatujarejea tena utaratibu huo. Mfumo wowote ambao unapanua demokrasia ya chama ni bora zaidi katika kuimarisha chama. Chama kinakomaa kwa wanachama kushindana kwenye chaguzi za ndani. Natumai uchaguzi mkuu ujao wa chama utakuwa na wagombea wengi zaidi ili wanachama wapate uchaguzi wa kweli. Sipendi chaguzi za kupita bila kupingwa katika chama kinachotaka kujenga demokrasia ya nchi.Je, utaratibu wa kupita mikoani katika kutafuta nafasi ya kugombea uenyekiti kama ilivyokuwa wakati wa Mbowe unafaa au CHADEMA irudi katika utaratibu kama wa CCM?
Nasikia suala hili hapa, tupeni ushahidi na tutachukua hatua mara moja.Mheshimiwa Zitto Viongozi/CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kufichua ufisadi. Kuna taarifa kuwa kuna mwanachama wenu katafuna fedha za M4C, ni kweli? Kama ni kweli, ameshughulikiwaje? Kama hajashughulikiwa, ni kwanini mko kimya?
Naibu Katibu Mkuu sio msemaji wa chama. Katika kujibu suala la demokrasia katika chama nilisema kuwa kuna utaratibu wa kujadili hoja mbali mbali ndani kwa ndani, yakiwemo matamko ya chama.Zitto wewe ni naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Mara nyingi matamko ya chama yametolewa na Katibu, Mwenyekiti, Mnyika (tangu kabla hajawa msemaji) na mara chache wanasheria km Lissu, Marando na Prof.Safari. Kwanini Zitto umekuwa mbali sana na matamko haya ya CHADEMA ukiwa kama Naibu Katibu mkuu? (Naamini hutojibu ni mgawanyo wa kazi)
CHADEMA ni chama kinachokua kwa kasi sana, na kadiri kinavyokua kinabadilika positively. Moja ya mabadiliko hayo ni idadi ya wanachama, nyingine ni kuweza kushika Uongozi wa Upinzani Bungeni, nafasi ambayo ilikua ya CUF nilipo ingia chama. Chama hivi sasa kipo kila mahala.Unafikiri CHADEMA uliyoikuta mwanzo ndiyo hii ya sasa au kuna mabadiliko? Kama kuna mabadiliko ni yepi na unafanya nini kufanya CHADEMA iwe kama ambavyo ulitaka iwe?
Sina mashaka na hili. Nitafafanua zaidi baadayeUnafikiri namna CHADEMA inavyoendesha siasa zake kuna uwezekano wa kushika dola mapema (2015)? Kama ndiyo kwanini na kama hapana unafikiri mabadiliko gani yanatakiwa kufanyika kuelekea 2015?
Kweli unategemea kuwa chama tawala kinaweza kukisifu chama cha upinzani kwa kuwa na presidential material? Mimi ni Presidential material kwa mfano.CCM wanadai kuwa nyinyi CHADEMA hamna presidential materials, una kauli gani juu ya hili?
Ili Tanzania iwe salama ni lazima CCM ishindwe uchaguzi. CCM ikishinda tena mwaka 2015 itavunja sana moyo wa wananchi na wengine wanaweza kukata tama. Lakini pia CCM imechoka na haina nguvu za kutosha kukabiliana na changamoto za nchi hivi sasa.Una muono gani kuhusu upinzani nchini na nini nafasi ya upinzani hasa CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ukilinganisha na chama tawala CCM?
Ni bahati mbaya sana kuwa hatutumii baadhi ya mafanikio yetu Bungeni kwenye ulingo wa siasa ma hivyo kuwaacha CCM wanachukua credits.
Kwa mfano, ni kwanini mafanikio ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu hatujayafanyia kazi ya kisiasa? Ingawa hatukufanikiwa kumtoa Waziri Mkuu lakini tuliilazimisha Serikali kufanya mabadiliko. Kikwete alisema ni upepo tu, lakini upepo huu ulikuwa na joto kali ukamshinda na tukaacha yeye achukue credit kwa kazi yetu ya uwajibikaji.
Hoja ya juzi ya Mheshimiwa Halima Mdee kuhusu Ardhi inabidi kuifanya ni ajenda ya kisiasa. Hoja ya Mkonge tulikwenda Tanga na ilikuwa na mafanikio makubwa sana. Hoja ya Mabilioni ya Uswiss nayo tunaiachia wanaisemea watu wa CCM kuififiza. Historia inatuonyesha kuwa hoja zote tulizozitumia vizuri nje ya Bunge zilijenga taswira nzuri ya chama ie Buzwagi na EPA. We ignore this at our own peril- Chadema ni chama cha kitaifa. Kingekuwa chama cha kidini au kikabila kingefutwa. Katika uongozi wa Chadema unapata watu toka mikoa na kabila mbali mbali, pia watu toka dini mbali mbali. Diversity hii haipatikani katika vyama vingi humu nchini. Nadhani mtazamo huu unapandikizwa na watu ambao hawakipendi chama chetu na wanao ona chama kama threat kwa maslahi yao binafsi.
" Mhe. Zitto, Viongozi/CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kufichua ufisadi. Kuna taarifa kuwa kuna mwanachama wenu katafuna fedha za M4C, ni kweli? Kama ni kweli, ameshughulikiwaje? Kama hajashughulikiwa, ni kwanini mko kimya?"
Asante mkuu nimekupata, swali linalofuata;
C. Zitto na kuhusishwa na CCM
Ukitaka kummaliza mwanasiasa yeyote wa upinzani hapa Tanzania mhusishe na ama usalama wa Taifa au CCM. Ndivyo ilivyokuwa kwa Mabere Marando miaka ya Tisini. Marando ameishi kuweka sawa historia ingawa propaganda dhidi yake zilikuwa kali sana kiasi cha kuogopwa kweli kweli. Napita njia hiyo hiyo ya Marando na wanaonipaka matope haya wataona aibu sana ukweli utakapodhihiri.Kumekuwa na shutuma za mara kwa mara kuwa una ukaribu uliokithiri na Chama kuu pinzani kwa CHADEMA yaani CCM. Unasemaje kuhusiana na tuhuma hizo?
Kuhusu Rais Kikwete, kwanza ifahamike Jakaya Kikwete na Zitto Kabwe wana mahusiano yao nje ya siasa na hata siku moja hatujadili vyama vyetu. Rais Kikwete anaamini katika uzalendo wangu.Inasemekana kua ukaribu huo unaweza kuonekana kupitia ukaribu wako na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Unasemaje hapa?
Suala la kusafiri na Rais ni suala la kawaida sana. Nashangaa sana namna linavyokuzwa wakati ni wazi kabisa kua Rais lazima asafiri na wabunge, na anae wateua wabunge ni Spika wa Bunge. Kila Rais, Makamu wa Rais au Waziri mkuu wanapo safiri huambatana na wabunge wa kambi zote mbili.Mkuu, vipi kuhusu kuonekana kwako in public pamoja na rais sehemu tofauti hadi safari za nje ya nchi.
Rais Kikwete hakufika jimboni kwangu kumnadi mgombea wa chama chake. Napenda niwakumbushe, sio mwaka 2010 tu, toka nimekuwa mbunge Rais Kikwete hajawahi kuja kwenye kampeni jimboni kwangu. Hakuna makubaliano yeyote, bali anaheshimu mchango wangu kwenye nchi yangu. Mwaka 2005 hakuja Kigoma Kaskazini. Mwaka 2010 hakuja Kigoma Kaskazini. Lipumba pia hakuja Kigoma Kaskazini kunadi mgombea wake wa CUF.Inasemekana kuwa ni Kwa sababu yako ndio maana rais JK hakumnadi mgombea wa ubunge wa CCM wa jimbo lako katika uchaguzi mkuu uliopita na kwamba ndio maana hukushiriki katika kuungana na wanachama wako katika kumsusia JK siku ile anafungia bunge.
Baadhi ya watu wanapandikiza chuki hizi kwa sababu zao wenyewe. Hawanisumbui maana najua ni kikundi kidogo cha watu wachache wenye malengo yao ovu. Wajue tu kwamba hawawezi kuwadanganya Watanzania ambao wanafanya maamuzi yao sio tokana na propaganda ila kutokana na matendo ya kila mmoja.Vipi madai kuwa unatumwa na CCM ili kupunguza nguvu ya CHADEMA? Kama si kweli unadhani kwanini watu wanakuona kama pandikizi ndani ya CHADEMA?
Sijawahi wala kufikiria kuhamia CCM. Kama nilivyosema hapo awali, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote tofauti na CHADEMA. Namwomba mungu kuwa niondoke duniani nikiwa chama hiki hiki. Siamini katika kuhama vyama. Ninaamini katika mfumo imara wa vyama vingi nchini. Ninaamini katika demokrasia pana.Ni kweli kuwa una mkakati wa kuhamia CCM kabla ya 2015?
Swali hili na lililotangulia yanaonyesha kuwa hizi kweli ni tetesi tu. Sasa kama unasema nina mkakati wa kuhamia CCM. Tena kuna tetesi nimeanzisha chama na nataka kuhamia huko, sasa mimi nina vyama vingapi nitakavyohamia. Sijawahi hata kufikiria kuanzisha chama cha siasa. Chama changu ni CHADEMA na sitaondoka CHADEMA. Kinachonisikitisha ni kwamba kuna viongozi wa CHADEMA wamekula sumu hii na bila woga wanaisema kana kwamba ni kweli.Vipi tetesi kuwa wewe na Kafulila mmeanzisha chama na una mkakati wa kutimkia huko?
Hili watasema watu wa Kigoma wenyewe. Sio watu wa jimboni kwangu tu bali watu wa mkoa mzima wa Kigoma. Kigoma ya mwaka 2005 na Kigoma ya mwaka 2012 ni sawa na kichuguu na mlima Kilimanjaro. Tunaendelea kusukuma maendeleo zaidi ya Mkoa huu. Nafurahi sana kuwa sehemu ya mabadiliko haya ya mkoa wangu. I am very proud.Unaweza orodhesha utofauti wa Kigoma ya sasa na Kigoma kabla ya Zitto kuwa mbunge wake?
Sina ukaribu na Serikali ya Ujerumani.Mkoa wa Kigoma unanufaika/utanufaikaje na ukaribu wako na serikali ya Ujerumani?
CHADEMA ni chama imara sana Kigoma Kaskazini. Kina mtandao kila kitongoji na kina viongozi mahiri kwenye vijiji. Tunachohitaji ni kupata mgombea mzuri.Umeandaa mikakati gani kuhakikisha Chadema inatetea vema hicho kiti chake?
Sijaandaa mtu. Nachukia siasa za kuandaa watu. Mimi sikuandaliwa kugombea Kigoma Kaskazini. Nilitaka kuwa Mbunge na nikaomba ridhaa. Yeyote anayetaka kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini lazima aanze sasa kushiriki kazi za chama chetu, tumjue na tumpime na wengine kasha Mkutano Mkuu wa chama katika Jimbo utateua mmoja aliyebora kabisa.Kuna mtu ambaye umemuandaa kugombea nafasi ya Ubunge Kigoma Kaskazini? Ni kwa tiketi ya chama gani? Kama yupo tunaweza mfahamu au bado ni siri kwa sasa? Vipi ndugu Yared Fubusa ana nafasi gani kuelekea 2015?
Nitafuatilia suala kwenye kamati yangu. Sikuwa nimelitilia maanani.Mgodi wa chumvi wa Uvinza uliouzwa kwa bei ya hisani kwanini hawalipii yale maji ya chumvi ambayo yapo ardhini toka kugunduliwa kwake miaka ya 1800's ("Brine") kwa kutumia "flow meter" kama mwananchi wa kawaida wa Kigoma Mjini ambaye analipia maji ya KUWASA kutoka ziwa Tanganyika? Je, wawakezaji hao waliuziwa hata mkondo wa maji ya chumvi yaliyopo ardhini wakati wao hawakuwa wagunduzi?
Ndugu Kafulila anafuatilia suala hili kwa kina sana. Kuna kazi inaendelea hivi sasa kuhusu suala hili sipendi tuiseme hadharani.Pamoja na kuuziwa kiwanda hicho kwa bei ya hisani, kwanini bado wanaendelea kutumia nishati ya kuni kutoka kwenye miti asili ambayo hawakupanda wao badala ya kutumia nishati mbadala?
Ufahari wa Utu wao. Leo watu wa Kigoma hawaoni aibu kujitambulisha hivyo. Haikuwa hivyo miaka ya nyuma. Hili ni kubwa sana kwangu kuliko mamia ya kilometa za barabara au makumi ya megawati za umeme au Uwanja wa ndege wa Kimataifa.Katika vipindi vyote hivi vya ungozi wako wananchi wa Kigoma Kaskazini ungependa wakukumbuke kwa lipi?