LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 29,917
- 47,547
Wajuba, kutokana na miaka hii maadili ya ndoa kuporomoka na ndoa hazidumu, kuna haja ya kutoa mahari na kufanya sherehe ya harusi kwa kutegemea michango ya watu? Mbona miaka ya nyuma michango haikuwepo na ndoa zilidumu mpaka kifo? Inakuaje unapanga kufanya sherehe ya mamilioni kwa kutegemea mifuko ya watu? Mbona zamani mtu alijibeba mwenyewe kufanya sherehe ya harusi kwa bajeti yake? Kuhusu mahari, inakuaje utoe mahari halafu ndoa haidumu? Kwingine ukiasi ndoa mahari inarudishwa. Kama tumependana tuoane tu, wazazi wako watapata zawadi kimtindo kutokana na hali zao kiuchumi
