Mahari; Mchakato na viwango vyake

Zamani mahari ilikuwa inatolewa na mwanaume kama asante kwa wazazi kwa kumtunza na kumlinda binti mpaka kufikia wakati huo anapoolewa (ndipo kukawa na hadithi za kama binti anakutwa hana bikira basi mahali inarejeshwa)

Hapa umeeleza vyema kabisa mkuu, na mantiki ya utunzaji wa binti ni kweli ilizingatia kwanza "uanamwali" halafu pili ndio ilikuwa ni kama shukrani kwani baada ya binti kuolewa anakuwa ni sehemu ya milki ya mwanaume.

kwa mantiki hiyo basi na ulimwengu huu uliobadilika ambao tunaoa na kuolewa na watu ambao wameshakuwa na minimum ya mahusiano 10 nyuma kuna umuhimu kweli?
Kama nilivyoeleza hapo awali inaaminika kwamba pindi mwanamke anapoolewa moja kwa moja huwa ni sehemu ya milki ya mwanaume...kufanya hilo litimilike ndiposa unatoa mahari kama hati ya kupewa miliki.

Kama utakuwa unafahamu vizuri nadharia za filosofia, ndani yake huwa kuna suala moja linaitwa "mabadiliko ya kitamaduni", mabadiliko haya huletwa na sisi watu kulingana na matakwa kwa wakati uliopo. Kwa mantiki hii ya mabadiliko ya kitamaduni, suala la mwanamke aliyejitunza ndiye mwenye kustahiki ndoa na mahari ni kama limezikwa.
Hivyo mzani ni kama umebadilika na upande ulioegemea ni ule unaotoa taswira kwamba mahari ni shukrani tu ya ambavyo wazazi wa kike walivyomlea binti yao katika makuzi ya kimo na maarifa. Therefore umuhimu bado upo...
 
Haya yameisha mkuu

Tatizo walilonalo wengi ni stereotypes. Sasa stereotypes huwa hazitokei tu kwenye ombwe. Huwa zinatokana na mambo yanayotokea licha ya uchache au wingi wake.

Ndiyo hayo ya Wasukuma na wanawake weupe (mi nawaita caramel complexioned). Wapo kweli Wasukuma wanaopenda wanawake wa rangi hiyo kama ilivyo tu kwa makabila mengine.

Lakini kwa sababu ambazo hata sizielewi hiyo label ya Wasukuma kupenda vyeupe dawa ime-stick.

Come on now. Lekagi amamihayo ging'we.
 

I thought hutaoa milele?
mzanzibari kakubadili mawazo?
 
Umenifanya nicheke kwa nguvu kweli
 
Ha ha ha, kwa kweli hii sukuma/chaga imekuwa fasheni

Kuna mzee mmoja alioa Arusha miaka ya 70, moja ya sababu wanayosema ni rangi afu kwa mahari ndogo sana. Badala ya kuombwa ng'ombe aliombwa vitu kama pombe ya wazee na vitu vidogo vidogo sana, gharama ilikuwa kama thamani ya ng'ombe wawili tu.

Na ni mkewe hadi leo na wana mabinti weupe, huwa anajidai kwa utani na kusema mnaona, mie nilibadilisha mbegu ya ukoo, sasa hivi tuna mchele wa supa.

 
Ninaamini kwa gharama za kumsomesha binti yangu mpaka Chuo Kikuu, tena with Masters, hakuma mwanaume ambaye anaweza kunilipa. Cha msingi, kama ni lazima sana kulingana na mila basi atalipa the minimal. Kwa mfano, kama ni ng'ombe tatu basi kila ngome ni elfu kumi au shilingi moja!!!!!!!! Msishangae!!! Hapa natimiza mila tu na pia mwanangu hakuna mwenye uwezo wa kumfidia kwa malezi, malazi, chakula, mavazi, huduma lukuki na upendo toka kwa wazazi na kaka zake. Kwa mantiki hii mwanaume atakayemuoa binti yangu ni sawa na kuwa hatalipa cha maana na hii ni kwa kuwa hata siku moja mwanangu ni lazima amheshimu kwa kuwa pia mshahara wote watakula wao wakati nimesomesha mimi!!!!! Sihitaji mshahara wao ni kwa ajili ya maisha yao na watoto Mungu atawajalia. Ninachotaka tu mwanangu aheshimiwe sana, athaminiwe kila upande na kama utafanya kinyume basi ni rahisi arudi kwangu na sitakuwa na cha kurudisha. (up to grade 7 school fees plus matumizi 42m minimum, o-level 30m minimum, university 40m min (assume medicine or laws for five years). Kwa mantiki hii minimum kusoma kwa shule na vyuo vya Tz hadi first degree tu ni almost 120m. Halafu unilipe mil 6 au 3 for what!!!! My daughter's intrinsic value is incomputable!!!
 
Baadh ya makabila kama nnakotoka, mahar anataja mjomba na, huwa ni fedha taslimu nazo hukabidhiwa kwa mwanamke usiku wa harusi. Na kitendo hiko hufanywa na shangazi wa mwanamke tu
 

"Pemba eee Pemba

Naskia ni kuzuri, Jioni kuna upepo

Upepo unanukia, marashi ya karafuu"

Kwani ng'ombe wanapanda mtumbwi?

Au kwa "cheupe dawa" mahari hata yanaweza kufanywa kwa hisa kwenye NY Stock Exchange Market huko!
 
Rangi, elimu ya darasa la saba hivi muhimu sana (at least binamu zangu niliona wakati wanaolewa, mmoja hakumaliza la saba alikuwa hata familia haibageini kwa kujidai)

Vingine ni pamoja na kuolewa kwa kuchumbiwa(sio kutoroshwa-kulehiwa wala kubwakwa-kupondiwa), tena sifa huwa kubwa zaidi pale ambapo mchumba wala humfahamu, labda ni wa kijiji jirani kakuona gulioni akakufuatilia hadi kwenu then akaja kuchumbia. Chezeiya wamekuja na Phonex kama 4 zimepaki nje, sio waje wamebebana, kila mmoja aje na yake, ooh my God ni zaidi ya X6.

Vingine vinavyoongeza soko la binti kwenye kubargain mahari ni pamoja kama hajazaa, akiwa kazaa bargaining power inapungua.

Pia kuna vitu kama body size, meno, mwanya maana hizi vinajumuisha kwenye definition ya uzuri.


Kwahiyo unakubali kwamba ka rangi ni very important aspect ya kukuza mahari eeh? Hata kama sio siku hizi ila ilikuwa hivyo Ng'wanik angu"
 
Naomba nikupe like kwa hapa Gaijin maana kitufe cha like sijui kimeenda wapi. Somo zuri sana
 
Last edited by a moderator:


Duh! Kumbe mkorogo wataushtukia eee

Ngoja nikaze buti kwenye kidato basi, manake huo utipwa tipwa siuwezi
 
Nakutogagwa kwakweli!Lol
 
Baadh ya makabila kama nnakotoka, mahar anataja mjomba na, huwa ni fedha taslimu nazo hukabidhiwa kwa mwanamke usiku wa harusi. Na kitendo hiko hufanywa na shangazi wa mwanamke tu
Dah asante sana mkuu, hivi kuna story nilisikia kuna sehemu mahari ni madebe mawili ya pombe, ni wapi huko?
 
Duh! Kumbe mkorogo wataushtukia eee

Ngoja nikaze buti kwenye kidato basi, manake huo utipwa tipwa siuwezi
"Oyo duhu, wichubhula" hahahahaa
 
Usije ukasoma sana ukamshinda mwalimu mkuu wa shule ya msingi, mwenyekiti wa kijiji au medical assistant wa dispendary ya kijiji. Watashindwa kupima umesoma hadi elimu gani.

Wakisikia fulani anasoma wanauliza, ameshasoma kama mwalimu mkuu? Wakijibiwa umemzidi wanashindwa kuelewa ni elimu gani unayosomea.

Duh! Kumbe mkorogo wataushtukia eee

Ngoja nikaze buti kwenye kidato basi, manake huo utipwa tipwa siuwezi
 
Naomba nikupe like kwa hapa Gaijin maana kitufe cha like sijui kimeenda wapi. Somo zuri sana

Kwa kuongezea tu ili kuweka mambo kwenye perspective

Mahari kwa Waislam inarudishwa iwapo mwanamke atataka ndoa ivunjwe bila ya kuhusika kwa makosa ya mume

Kwa mfano, mwanamke akisema ndoa basi kwa vile hana mapenzi na mume wake, au hajiskii kuwa kwenye ndoa.

Anarudisha mahari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…