MAHARI:Acha mfumo dume uendelee Haki sawa maigizo.

Nasikiliza na kusoma kwny media akina mama wamecharuka kwl kwl kua wanataka haki sawa yaani kwny ndoa pia kuwe sawa kimaamuzi tena usiombe ukutane na wanaharakati wa haki za wanawake utajuta,nliwahi kuhudhuria kongamano la TGNP kwa wiki 1 akina mama walikua wamecharuka hasa wanadai haki sawa povu linawatoka nakua mpole maana niko kwny msitu wa akina mama namlaumu alienileta kwny hili kongamano
Najiuliza ivi hii MAHARI tunayodaiwa ya nini km tunapiga vita mila na desturi za m'ume ku-dominate maamuzi kwny ndoa navuta picha mahari unaambiwa milioni 2.5 hapo bado vitu kibaooo unadaiwa alafu wanataka binti yao apate haki sawa mbn huu usawa hamkuuonyesha mwanzoni wakati mnakurupuka kuniuzia binti yenu tena ukiomba wapungeza baba mkwe povu litamtoka "eti unajua nimemlea kwa shilingi ngapi?".
Bado naamini adui wa mapambano ya akina mama kwenye vita hii ni akina mama wenyewe ukwl unabaki huu utaratibu ni kichocheo cha mfumo dume ndo maana kila kumbu2 ya mahari ikija kichwani ujasiri wa kushika fagio unapotea,kuoshoa vyombo na kumpikia inakua mtihani ukiamini nililipa pesa nyingi sana hawa wanaharakati wamekua km "chichidodo" bado naamini ukiona binti kwenu wanataja mahari uolewe jua unauzwa unatakiwa kumsikiliza mnunuzi km wakati ule mnunuzi anamsikiliza muuzaji.
Inawezekana mimi niko na mtazamo hasi ila siogopi kusema kua huu usawa ni maigizo ambayo script zake zimeandikwa na wazungu ambao hatufanani kwny mapokeo ya mila na desturi kabisa ila waigizaji wako bussy hasa kusoma script na kuzifanyia kazi mbaya zaidi wengi wa akina mama anatoka kwny kongamano ana hasira hasa akifika nyumbani "baba yenu kaacha hela ya mboga?"
Niwatakieni kila la heri kwny harakati zenu ila mjue director wenu wa hii movie(mzungu) katulia kule anamuheshimu mumewe vibaya mno anawatia kichaa nyie waigizaji wake na mnavozidi kucharuka ndo wanaume wanapata hasira na mahari zao baadala ya nafuu ndo haya maafa mnayoyaona mama kadai haki anaishia kuumizwa kumbe tatizo ni kule mwanzo mlimpomuambia mtani wangu msukuma alete ng'ombe 100 alafu leo unataka aingie jikoni apike wakati wewe unaenda kusuka kwa jirani.
umenena vema ila kwamimi hata kama sijatoa mahari ujasiri wa kufagia sina wala kupika na ukiona siku nafanya hivyo basi ujue tayari nilishapelekwa kwa kalmanzira au niko kazini namtega mbuzi wangu!
 
tatizo mkituoa bure pia mtatudharau mtaona hatuna thamani. acha tu mlipishwe mahela mengi hata wife akikuuzi ukifikiria mahari uliyotoa unahairisha kutoa talaka.
 
Smile, miss chagga nasikia kwenu mahali wanadai na hela ya sendoff kabisa.!

inategemeana na familia unayoenda kutoa mahari a si wote ........... me kuna baadhi ya familia za kichaga wanakuambia mahari ni upendo kwa mwanae na hawataki kitu ila hii ya pili mara nyingi utajikuta huna say ..........
 
Hapo kwenye mahari wanawake wanahusika vp ktk mfumo dume? Sababu ni ninyi wanaume ndiyo wapanga mahari, na ni ninyi wenyewe ndiyo mnaolalamika, wanawake huambiwa tu au wachache wanaoshiriki ktk kupanga mahari, hivyo ninyi ndo mnaouendekeza mfumo dume. Kama ishu ni kuuza basi mnauziana wenyew(waume kwa waume) tena wamama ndo huwa watetez kiaina flan kuomba mahari ipunguzwe, lakin wanaume uso mbuzi.
 
Haki sawa? Nani kasema bwn, huwezi pingana na asili, hivi me anaweza kufanya dog style wakati wa kugegedana? Kama haiwezekani basi hakuna haki sawa hapo!
 
Kwani TGNP wenyewe wameolewa?

Mimi ninaona hawa wanaharakati hasa TGNP ni wasaka tonge tu wanatafuta hela tu kutoka mashirika ya kifadhili ndio maana hawalengi kumaliza tatizo lenyewe sababu likiisha nao ajira zao zitakuwa zimeisha. kama kweli wanadhamira ya kumaliza mfumo dume wange anza na kupiga vita mahari kwani ndio inaya fanya wanaume tuchukulie kama tume nunua mke au huduma na mtu akisha nunua kitu kinabaki kuwa mali yake na matumizi tanapanga mwenyewe, jambo lingine ni utegemezi pamoja na mahari bado mwanamke kila siku anahitaji kupewa kodi ya meza. Laiti hawa wanaharakati wangeanza kupinga haya mambo mengine yangeisha taratibu tu
 
Siku hizi kuolewa ni dili ukishapata Mali tu mke atalazumisha talaka ili mugawe Mali ,zamani wa.wake wakiolewa kkwa mkungu wa ndizi tu
 
Hapo kwenye mahari wanawake wanahusika vp ktk mfumo dume? Sababu ni ninyi wanaume ndiyo wapanga mahari, na ni ninyi wenyewe ndiyo mnaolalamika, wanawake huambiwa tu au wachache wanaoshiriki ktk kupanga mahari, hivyo ninyi ndo mnaouendekeza mfumo dume. Kama ishu ni kuuza basi mnauziana wenyew(waume kwa waume) tena wamama ndo huwa watetez kiaina flan kuomba mahari ipunguzwe, lakin wanaume uso mbuzi.

Mwanamke anahusika sana
1:kwa nini kwny hizi harakati zenu za haki sawa isiwe moja ya ajenda zenu kua hamtaki kuuzwa na mseme MAHARI NO MORE anzieni hapo mbn mnatetea na mikaja ya bibi sijui ni na niniii
2:Wewe ndo muolewaji waambie wanafamilia kua mchumba wako anakuja kijitambulisha lakini hautaki atozwe chochote wewe sio bidhaa.
3:Nyinyi wanawake ndo mabingwa wa kutu-discourage wanaume maana ukiambiwa nataka nije kwenu kabla haujasema 'asante' mnauliza mahari umejiandaa maana kwetu kiboko babe
4:Onyesha ushujaa nikitoa mahari ichukue unirudishie mchumba wako tufanyie vitu vingie sio unakimbilia nayi saloon.
Mchango wenu ni mkubwa sana kuliko wanaume kwny existence ya mahari jichunguzeni kabla hamjasema sisi ndo tunawauza.
 
Qualifier tena izi NGO's ndo wanaweka petroli kwny moto maana wanandaa warsha wanawatia wehu akina mama wakiwalszimisha waje kudai haki zao bila kuwaambia ukwl matokeo rate ya abuse inapanda unapomuona mkeo analeta izo hbr matokeo yake tunasikia vifo na majeruhi bila sababu alafu wakati wanawake wanapata visanga wao wako ofisini kimyaa for sure wapo ki-maslahi yao.
 
Last edited by a moderator:
Afrika kweli tunadanganywa sana. Nenda nchi zilizo endelea uone, kuna masomo hakuna msichana hata mmoja na wala awana muda wakusema heti tuwabebe hili nao wasome kozi hili kuwa na jinsia sawa, hakuna kitu kama hicho, Kuna kazi zingine tangia miaka hiyo hakuna mwanamke kufanya kutokana na taratibu na ugumu wa kazi hizo, lakini huku kwetu tunaletewa haki sawa.

Ndiyo maana hata maendeleo ya kweli ktk kizazi hiki chetu ni ngumu sana kutokana na wanawake kupigania haki sawa. Leo hii unakomalia nitoe mahali mimi mtoto wa kiume, basi nawao watoe mahali hili kuweka uwiano sawa.
 
Kuna yele mama aliyekuwa TAMWA, sasa ivi nasikia anasoma PhD, alikuwa mkali kweli wakati akitetea ishu za kina mama, but trust me, ni jirani pale tabata kimanga, home anajiheshimu na kufanya shughuli zote za wakinamama..huwezi amini, ngoja asbh aamke kwenye media anavyopaza sauti...
 
Kuna yele mama aliyekuwa TAMWA, sasa ivi nasikia anasoma PhD, alikuwa mkali kweli wakati akitetea ishu za kina mama, but trust me, ni jirani pale tabata kimanga, home anajiheshimu na kufanya shughuli zote za wakinamama..huwezi amini, ngoja asbh aamke kwenye media anavyopaza sauti...

Haaahaa ndio nikasema povu linawatoka jukwaani wakirudi nyumbani wako tofauti kabisa wanawaingiza mkenge wake zetu wkt wao ndoa zao ziko shwariii
 
Eti unatoa MAHARI MILION kadhaa halafu baada ya harusi unaletewa shemeji zako kadhaa waishi kwako, kisingizio wanamsaidia dada yao kazi.
 
Back
Top Bottom