MAHARI:Acha mfumo dume uendelee Haki sawa maigizo.

McDonaldJr

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
6,392
2,000
Nasikiliza na kusoma kwny media akina mama wamecharuka kwl kwl kua wanataka haki sawa yaani kwny ndoa pia kuwe sawa kimaamuzi tena usiombe ukutane na wanaharakati wa haki za wanawake utajuta,nliwahi kuhudhuria kongamano la TGNP kwa wiki 1 akina mama walikua wamecharuka hasa wanadai haki sawa povu linawatoka nakua mpole maana niko kwny msitu wa akina mama namlaumu alienileta kwny hili kongamano
Najiuliza ivi hii MAHARI tunayodaiwa ya nini km tunapiga vita mila na desturi za m'ume ku-dominate maamuzi kwny ndoa navuta picha mahari unaambiwa milioni 2.5 hapo bado vitu kibaooo unadaiwa alafu wanataka binti yao apate haki sawa mbn huu usawa hamkuuonyesha mwanzoni wakati mnakurupuka kuniuzia binti yenu tena ukiomba wapungeza baba mkwe povu litamtoka "eti unajua nimemlea kwa shilingi ngapi?".
Bado naamini adui wa mapambano ya akina mama kwenye vita hii ni akina mama wenyewe ukwl unabaki huu utaratibu ni kichocheo cha mfumo dume ndo maana kila kumbu2 ya mahari ikija kichwani ujasiri wa kushika fagio unapotea,kuoshoa vyombo na kumpikia inakua mtihani ukiamini nililipa pesa nyingi sana hawa wanaharakati wamekua km "chichidodo" bado naamini ukiona binti kwenu wanataja mahari uolewe jua unauzwa unatakiwa kumsikiliza mnunuzi km wakati ule mnunuzi anamsikiliza muuzaji.
Inawezekana mimi niko na mtazamo hasi ila siogopi kusema kua huu usawa ni maigizo ambayo script zake zimeandikwa na wazungu ambao hatufanani kwny mapokeo ya mila na desturi kabisa ila waigizaji wako bussy hasa kusoma script na kuzifanyia kazi mbaya zaidi wengi wa akina mama anatoka kwny kongamano ana hasira hasa akifika nyumbani "baba yenu kaacha hela ya mboga?"
Niwatakieni kila la heri kwny harakati zenu ila mjue director wenu wa hii movie(mzungu) katulia kule anamuheshimu mumewe vibaya mno anawatia kichaa nyie waigizaji wake na mnavozidi kucharuka ndo wanaume wanapata hasira na mahari zao baadala ya nafuu ndo haya maafa mnayoyaona mama kadai haki anaishia kuumizwa kumbe tatizo ni kule mwanzo mlimpomuambia mtani wangu msukuma alete ng'ombe 100 alafu leo unataka aingie jikoni apike wakati wewe unaenda kusuka kwa jirani.
 

McDonaldJr

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
6,392
2,000
Kuna kelele hapa zinaendelea za haki sawa wakati ndoa bado changa na mtani katoa nyingi sana...haahaa mimi wakitaka mzigo mkubwa lzm tuulizane vizuri kwnz km mtoto wao nae mwanaharakati pia maana patachimbika eti

Vp kwani mkuu, wamekupiga mzigo mnene??
 

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,938
2,000
Wengi wa hawa wanaharakati uwa wanakuwa hawana ndoa...unajua aliyesema mafahari wawili hawakai zizi moja hata hakukosea...oa mwanamke wa haki sawa oune moto wake....tatizo hiyo haki sawa wanaielewa vibaya ndo maana inashindikana.....mwanaume ni mwanaume na mwanamke ni mwanamke....hapo hata jinsia tu zinaonyesha hatuposawa.....kuna majukumu ya mwanaume na kuna majukumu ya mwanamke katika familia...lazima tuweke mipaka katika majukumu ili umuhimu wa kila mmoja uwepo...... Msiseme haki sawa semeni tuheshimiane.......usawa haujawahi kutokea duniani tusidanganyane jamani....huo mnaouita usawa unawajendea kiburi kwa waume zenu mwisho wa siku mnaachika mchana kweupeee.....hao wanaowaambia haki sawa jua hiyo ni kazi yao, so mnawaingizia hela kwa kuufanya upumbavu wao...kama mnataka usawa mkadai kwanza kwa mungu then mje duniani.....maandiko yenyewe yanasema hawa aliletwa kuwa msaidizi wa adamu ...sasa nyie hamtaki nini?
 

McDonaldJr

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
6,392
2,000
Wengi wa hawa wanaharakati uwa wanakuwa hawana ndoa...unajua aliyesema mafahari wawili hawakai zizi moja hata hakukosea...oa mwanamke wa haki sawa oune moto wake....tatizo hiyo haki sawa wanaielewa vibaya ndo maana inashindikana.....mwanaume ni mwanaume na mwanamke ni mwanamke....hapo hata jinsia tu zinaonyesha hatuposawa.....kuna majukumu ya mwanaume na kuna majukumu ya mwanamke katika familia...lazima tuweke mipaka katika majukumu ili umuhimu wa kila mmoja uwepo...... Msiseme haki sawa semeni tuheshimiane.......usawa haujawahi kutokea duniani tusidanganyane jamani....huo mnaouita usawa unawajendea kiburi kwa waume zenu mwisho wa siku mnaachika mchana kweupeee.....hao wanaowaambia haki sawa jua hiyo ni kazi yao, so mnawaingizia hela kwa kuufanya upumbavu wao...kama mnataka usawa mkadai kwanza kwa mungu then mje duniani.....maandiko yenyewe yanasema hawa aliletwa kuwa msaidizi wa adamu ...sasa nyie hamtaki nini?

Umenena kaka tatizo akina mama wameingia kucheza hii ngoma bila kujua stahili yake hawa wanaharakati ni chanzo cha matatizo kwa kweli alafu kidini iko wazi sana ila wanaleta ubishani huwa naogopa sana nikisikia hii dhahama ya haki sawa maana ake ni kwenda kinyume kabisa na mgawanyo wa majukumu ila ipo siku wataelewa
 

nanjilinji

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
1,154
1,500
Pamoja na yote wenzetu wanataka huku na huku. Watutegemee kwa kila jambo ati wewe ni kichwa cha nyumba, tutoe mahari ila wanataka usawa, wanataka tupike kwa zamu, tuoshe vyombo kwa zamu, ukiomba k anakupa kwa masharti na ukiitafuta zilipo za kuombwa unaonekana msaliti. Wazungu usawa wanao kwa vile hii kitu mahari hakipo.
 

Fadhili Paulo

Verified Member
Sep 1, 2011
3,220
2,000
Mimi naapa sitakaa nitoe mahari hata iweje na hata binti yangu sitataka aolewe kwa mahari.
 

1son

Member
Aug 17, 2013
62
125
Sipendi atakuwasikia hawa actors was Hui tamthilia wamekuwa chanzo cha migogoro ya ndoa nyingi
 

McDonaldJr

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
6,392
2,000
nanjilinji ndio maana nasema wameingia ngomani pioneer wa hizi vurumani tunatofautiana utamaduni mbaya zaidi ndoa zao ni tofauti sana kama hizi za mkataba alafu maisha yao yametawaliwa na mitazamo tofauti uku kwetu akina mama wengi bado tegemezi bila kujali kua wana kazi au kipato bado majukumu ya msingi yako kwa baba zipo familia mama ana kipato kikubwa lakini baba ndo analea familia ingawa sio familia zote ila nyingi ni ivo Fadhili Paulo haaahaa utakosa mke...,kwenye ilo la kumuozesha binti yako bila mahari ni busara nakumbuka kuna dada angu aliambiwa na babu yangu ataje mahari yake akasema hataki kitu na aliolewa bila mahari
 
Last edited by a moderator:

High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,138
2,000
Ni maajabu ya mungu milioni mbili ya mahali
wakati watu tulianza na hiyo hela kama mtaji na saizi tuko mbali
 

McDonaldJr

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
6,392
2,000
Ni maajabu ya mungu milioni mbili ya mahali
wakati watu tulianza na hiyo hela kama mtaji na saizi tuko mbali

Haaahaa nenda kaguse sasa ivi mahari utakimbia ndio maana vijana imefikia hatua tunaishi na mabinti wa watu kimya kimya mara mimba basi mambo yanaenda kienyeji hiyo hela tunanunua unga na dagaa
 

Fadhili Paulo

Verified Member
Sep 1, 2011
3,220
2,000
sasa utamchukuaje mtoto wa watu kienyeji enyeji?

Hapana simchukuwi tu, napeleka barua kwao na posa (elfu 10) natoa, watapanga mahari nawambia poa, kisha kwaheri. Mkuu mahari zimekuwa ni vyanzo vya manyanyaso na mateso katika ndoa nyingi sana Tz
 

usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
500
Mada kama hizi hukuti wanawake wakitia mguu! Wako mbio mbio kutaka tuwasaidie kupika ila mabinti zao wanawauza, pato kubwa la familia linategemea mwanaume, nyumba kujenga anaangaliwa mwanaume, kusomesha watoto mwanaume. Wao pesa yao ni salon tu! Usawa utatoka wapi hapa? Cc Lala1, Nivea, Kaunga, snowhite na wengineo, njooni huku!
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom