"Maharage ya Mbeya maji mara moja" ni kauli ya kweli? Ni kwenye maharage tu au hadi kwa wanambeya? Kama kauli huumba, Jibu sahihi ni Oktoba 2020!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,599
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, ambalo jibu lake rasmi litapatikana baada ya October 28, 2020, ila kama una majibu, unaweza kuchangia kujibu na sio lazima tusubiri hadi hiyo October 2020.

Angalizo:
Naomba kuanza hili bandiko na angalizo la mawazo masafi, tusome bandiko hili tukiwa na mawazo masafi, ukiwa ni mtu wa mawazo masafi utasoma kile kilichoandikwa na sio unachofikiria,
Mfano Katerero ni Kijijini mkoani Kagera ni Siku ya Gulio Katerero ni moja ya hadithi kwenye somo la Kiswahili Darasa la 4 enzi zetu, hivyo ukizungumzia mambo ya Kijiji cha Katerero kwa wenye mawazo masafi mtaelewana. Hii mada yangu ni kuhusu maharage ya chakula, yale ya kupika ambayo ndio kitowea kinachoongoza kutumika Tanzania.

Kuna hoja kuwa kauli huwa zinaumba, sasa kuna hii kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja", Jee kauli hii ina ukweli wowote kuwa ukipika maharerage ya sehemu nyingine zote, ili yaive lazima uongeze maji zaidi ya mara moja, lakini ukipika maharage ya Mbeya, ukiweka maji, ni mara moja tuu hadi yanaiva?.

Kama kauli hii ni kweli kwa maharage ya Mbeya, maji ni mara moja tuu, jee ni kwa maharage tuu au hata kwa wana Mbeya wenyewe yaani Wambeya, nao pia ni ukiwa na shida yoyote, maji ni mara moja tuu, wanatepeta, wanalainika, na kufikia maamuzi ya kukubali au kukataa jambo lolote, mara moja tuu, kirahisi rahisi, kiulani?.

Nauliza hivi kufuatia siasa za Mbeya kuwa ni very interesting. Kwa kawaida huwa tukielekea uchaguzi Mkuu, hadi humu jf huwa kunapandishwa uzi maalum kwa "Siasa za Mbeya " kufuatia siasa za Mbeya kuwa very interesting zenye msisimko wa ajabu!.

Kipindi hiki cha miaka 4 ya awamu ya tano, tumeshuhudia harakati nyingi za wazi na za chini chini zikiandamana na changamoto za kisiasa jijini Mbeya ikiwamo kumsweka lupango Mbunge wa Mbeya, ili watu wamchukie kwa kumuona ni mhalifu, kwa hoja hizo hizo kama za maharage ya Mbeya, lakini wana Mbeya badala ya kumchukia ndio kwanza wanazidi kumpenda!.

Kikafuatia kituko cha mwaka kwa kufanya ibada ya kishetani ya kula nyama za maiti kwa kutengeneza jeneza tupu na kulifunika kwa bendera ya Chadema kisha kulizika, ili kuashiria kifo rasmi cha Chadema Mbeya, kitendo ambacho kilitafsiriwa kama kufuru kwa Mwenyenzi Mungu, hivyo wajuzi wa mambo wakabashiri kuwaka kwa hasira ya Mungu juu ya waliofanya kitendo hicho cha kufuru.

Badala ya hasira ya Mungu kuwaka kwa CCM Mbeya walikofanya uhayawani huo, ndio kwanza nyota ya CCM jijini Mbeya inavyazidi kung'aa baada ya juzi kati, Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya akiandamana na madiwani lukuki waliojitambua, walipojiengua Chadema Mbeya na kuibukia CCM Dodoma na kutangaza kujitoa Chadema na kujiunga CCM.

Leo online TV ya Ayo, imefanya mahojiano na Mbunge wa Mbeya, Mhe. Joseph Mbilinyi, Sugu na hiki ndicho Sugu alichosema.

Nimemsikia mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu kupitia ayo tv akidai alipigiwa simu na Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru Ally ili ajiunge nao lakini amemkatalia.

Sugu amedai kuwa sura yake siyo ya CCM na kwamba wanaohamia chama tawala ni wale Wajinga wajinga.

Hizi lugha za kihuni hazipaswi kutumiwa na wabunge wamwachie Hajji Manara.

Maendeleo hayana vyama!
Kama ni kweli Katibu Mkuu wa CCM ndiye anawapigia simu kuwato..oza wahame, kiukweli hii ni aibu kubwa!.

Ila maneno haya ya Sugu, yanaongeza hamasa, shamra shamra na mashamsham ya siasa za Mbeya kuelekea October 28, 2020, haswa kwa kuzingatia kigogo mmoja wa CCM anayejipitisha pitisha Mbeya hadi na majeneza, kama ikitokea CCM ikampitisha huyo kigogo wa majeneza, halafu wana Mbeya wakampiga chini, then hii kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja" itakuwa ni maharage tuu lakini wana Mbeya sio maji maji, mtepeto, bali ni wagumu kama jiwe au kisiki cha mpingo.

Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu, Kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja" Ina Ukweli?, Ni Kwenye Maharage tu au Hadi kwa Wanambeya?:

Je, October 28, 2020 Wana Mbeya WaTatulia, au kwa sababu wameisha zoea shida hadi wameota Sugu hivyo badala ya KuTulia, wao wataendelea za Sugu zao walizozoea?

Kauli Huumba!, Jibu la kama WanaMbeya ni kama Maharage ya Mbeya ya maji mara moja au au hapana ni October 28, 2020!.

Mbeya Oye!.

Paskali
Update.
Ni kweli kabisa, maharage ya Mbeya, maji mara moja!. Na sio maharage mboga tuu, hata .. ya kubadili mboga, ni maji mara moja!, kubwa kuliko ni hata kwenye siasa, Wanambeya ni maji mara moja!, wameamua kuachana na kutiana Sugu na badala yake wameamua ku Tulia na Tulia!.
Mbeya Oye...!.
P
 
Hakuna kitu kigumu kama kuuficha ukweli! Na ukweli wenyewe ni huu hapa na tunaujua na upo ndani yetu unaishi na kutawala!
masoudkipanya_B9A_6OMDjZT.jpeg
 
Mama ni kweli watu wanafanya biashara ya namna hiyo, basi hii haiishii kwenye siasa tu bali hata katika imani za kidini itatafsiriwa na kutendeka hivyo ukizingatia baadhi ya viongozi wa dini na wao wanashutumiwa kuwatengenwzea mazingaombwe waumini wao na mmoja aliwahi kusikika akimwambia muumini wake... "lia lia/piga kelele", sasa kama mambo yapo hivyo bora kizazi kifutike kije chenye hofu ya Mungu kuanzia viongozi hadi waongozwa.
 
Mbeya mjini na Iringa mjini wapiga kura wao wanajitambua ila mwaka huu maandalizi ya CCM yamekuwa ya kisayansi zaidi.

Ngoja October ifike tuwe mashuhuda!
 
CCM au C hao sio watu. Ni vitu ambavyo havina uhai.Lakin Wanambeya ni watu wana uhai na wanabadilika kulingana na wakati.CCM imetawala mbeya kwa Muda mrefu lakin saiz Wanambeya washabadilika sio wajinga tena.Kwa mtutu na bunduki kwa mahakama,Kwa tume hii CCM inaweza kupita Mbeya lakin Kamwe Wanambeya hawawezi kuwa CCM.Wanambeya aakimkubali mtu wanamkubali kwa kwa pamoja na wakimkataa wanamkataa kwa pamoja.

Kwa hiyo Pasco usije ukaipima Mbeya kwa uchaguzi wa Mwakahuu ulio na shaka kubwa.Kama CCM itashinda basi mbunge hatopata ushirikiano wa raia.Mfani ni Mbunge wa Mbeya vijijini,yani akipita sokoni hata wazee wenzake hawampishi achilia mbali vijana,lakin Sugu akipita mahali unaona uzuri wankuwa kiongozi.

WanaMbeya sio wanaCHADEMA, ni wanamabadiliko.Wanataka mfumo tofauti ndio maana hadi sasa CCM huku bado haikubaliki.Madiwani waliohama kama atapita yeyote basi ni kwa mtutu wa bunduki na maji ya kuwasha ila si kutangazwa kihali maana hawawezi kushinda.Ponapona yao ni vyeo wanavyopewa.Mfano Shitambala aligombea Ubunge Mbeya vijijini akapita,wakamhonga mamilioni akakubali kushindwa saizi ni katibu mkuu wa CCM mkoa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za Mbeya zinabadilika kutokana na wakati na majira nakumbuka Mwalimu Mpesya alikuwa mbunge aliyependwa sana wakati ule lakini mabadiliko yalivyokuja wana mbeya walibadili upepo kufuata Mwana Mbeya ambaye nafikiri alifundishwa na huyo huyo Mpesya kama sikosei pale Mbeya Day wakati huo.

Tuwape nafasi wana Mbeya wachague wanayemtaka kura ya turufu inamnyemelea mwana mama . kwa kuwa tu wanaona hakuna mambo yaliyofanyika toka Mwana Mbeya aingie zaidi ya siasa za hapa na pale.
 
Tulia mwepesi sana, hana mtaji wowote wa kura Mbeya Mjini, sioni ni kwa vipi anaweza kushindana na Sugu ambaye uchaguzi mkuu uliopita ndie mbunge alieongoza kwa kupata kura nyingi zaidi ya wote, hao CCM na polisi wao itabidi wambebe kweli kweli, kazi wanayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya Pascal nyuzi zako huwa ni tata kwa mtazamo wa juu juu, ila makini sana kwa undani na maana yake.

Nami nashindilia nyundo za kutosha, Je wanawani ile kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja" Ina Ukweli?, Ni Kwenye Maharage Tu Kama Mboga au Hadi Kwa Wanambeya?: Wanambeya tujitutumue na kulithibitisha hili hapo October!

Wakidai kuwa HAWAPANGIWI, waambieni na SISI HATUTUSHIKI maamuzi ni YETU wana Mbeya.
 
Hamna, Mbeya hamna kitu rainiiii..kule moto utawaka....wanyakyusa achana nao kabisa hizo ni machine zinazohema.
 
Kama watahesabu kura za ndani ya sanduku basi Tulia Ackson asubirie jumbo la Ikulu tu. Ila kama watalazimisha kutangaza matokeo feki basi wana Mbeya hawatavumilia na patachimbika.

Huo ujinga wa kuiba matokeo wakafanyie Dodoma na Singida ila siyo Mbeya
 
Kwa post ya mama majeneza naamini hawaafikian ndani juu ya mbeya,
Lakini hii aina yako ya propaganda be paskal naona kama n hoja mzunguko inayokata huku na huku

Rufaa kwenye tabia huwa na uzito sana kwenye propaganda lbda utafanikiwa kushinda basi leo umetumika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom