Mahakama yazuia mkataba wa TANESCO, DOWANS!

Mahakama yazuia mkataba wa TANESCO, DOWANS!

KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imependekeza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuingia mkataba mpya na Kampuni ya kufua umeme ya Dowans ikiwa ni hatua za muda mfupi kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

Hata hivyo, Mahakama Kuu imeizuia Serikali na Tanesco kuchukua hatua yoyote inayohusiana na mazungumzo au mkataba wa aina yoyote baina yake na Dowans bila ridhaa yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Januari Makamba alisema: "Kamati imependekeza mambo 30 ikiwamo kuwashwa kwa mitambo ya Dowans haraka na serikali itoe fedha zaidi kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL. Hatua hii imefikiwa kama suluhisho la muda mfupi la kupambana na mgawo.''

Makamba alisema pia kwamba kamati imependekeza kupunguzwa kwa megawati 50 kutoka katika migodi ya madini inayotumia umeme wa megawati 125 ili zipelekwe kwa wananchi.

Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga alisema mapendekezo hayo watayakabidhi katika Ofisi za Bunge na kwamba yatatangzwa na Spika, Anne Makinda

Lakini, wakati kamati ikitoa mapendekezo hayo, jana Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam anayesikiliza maombi ya usajili wa tuzo ya Kampuni ya Dowans iliyoshinda iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara(ICC), dhidi ya Tanesco alitoa agizo kuwa lisifanyike jambo lolote kuhusu Dowans nje ya mahakama.

“Naagiza jambo lolote lisifanyike nje ya mahakama wakati ikiendelea na shauri hili. Kama kutahitajika kuwa na majadiliano yoyote basi pande husika zilete maombi mahakamani ili iweze kusimamisha kwanza mchakato huu kusubiri majadiliano hayo."

Jaji Mushi alisema: "Haitakuwa vyema mahakama kuendelea na mchakato wakati na huko nje majadiliano yakiendelea. Kama pande hizo zikiafikiana, basi zinaweza kuja ‘ku-withdraw’ (kuondoa shauri) na kama zitashindwana basi ndipo tutakapoendelea na mchakato.”

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Makamba zinasema kuwa mapendekezo ya kamati hiyo yamefikiwa kama suluhisho la muda mfupi la kupambana na mgawo.

Chanzo chetu ndani ya kamati hiyo, jana kiliiambia Mwananchi kuwa kamati imependekeza kabla ya kuwashwa mitambo hiyo, Tanesco liingie mkataba maalumu wa miezi michache usiokuwa na utata wa kisheria wa kuuziwa umeme na kampuni ya Dowans kulingana na mahitaji.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, katika mkataba huo kamati imependekeza Tanesco iuziwe umeme kwa uniti na kwamba iwe inalipa kila siku kulingana na kiwango inachouziwa.

"Kwa kuwa suala la gharama za uuzaji umeme kwa uniti ni la kitaalamu, kamati imependekeza Tanesco iingie mkataba maalumu wa miezi michache wa makubaliano ya kuuziwa nishati ya umeme na ilipe kulingana na uniti iliyouziwa,'' kilisema chanzo chetu.

Awali, kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati hiyo katika Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam, Makamba aliimbia Mwananchi kuwa: "Leo (jana) wajumbe wa kamati, tunakutana ili kusahihisha herufi, maneno pamoja na kuweka koma na nukta katika ripoti yetu ya mapendekeo ya suluhisho la muda mfupi na mrefu la tatizo la umeme nchini."

Mwenyekiti huyo alisema mapendekezo hayo yalifikiwa juzi katika kikao chao cha majumuisho na Tanesco kilichomalizika saa 2:00 usiku.

Tofauti ya wananchi na wafanyabiashara kuhusu Dowans
Hata hivyo, mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yametolewa kukiwa na msuguano kati ya wafanyabiashara na wananchi. Wafanyabiashara wanataka mitambo ya Dowans iwashwe huku baadhi ya wananchi wakipinga na kutaka itafutwe mitambo mingine kupunguza tatizo hilo.

Kwa takriban wiki mbili, kamati hiyo ilifanya vikao vya ndani na mikutano ya wazi na wadau mbalimbali kukusanya maoni kuhusu suluhisho la muda mfupi na mrefu la tatizo la umeme nchini.

Lakini Jumamosi iliyopita katika kikao cha wazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam baadhi ya wananchi walikataa kuwashwa kwa mitambo ya Dowans huku wasomi, wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara kutaka mitambo hiyo iwashwe ikiwa ni njia ya haraka na suluhisho la muda mfupi la kupatikana kwa umeme.

Hatua hiyo ililenga kuongeza kiwango cha nishati hiyo kilichopungua katika Gridi ya Taifa kutokana na kushuka kwa uzalishaji katika mitambo ya umeme Mtera kulikosababishwa na kupugua kwa maji.

Kwa sasa Gridi ya Taifa ina upungufu wa megawati 297 kwa kuwa vyanzo vilivyopo vinazalisha megawati 540 huku mahitaji halisi yakiwa ni megawati 833 za umeme.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Nchi ina wenyewe hii, maana mizengwe inavyoendeshwa inakutana na visiki visivyoepukika na hatim haki itashinda tu.
Ni jambo la kushangaza kesi iko mahakamani na nje ya mahakama wanavyamya mambo bila kuhishirikisha mahakama ni kitendawili.
 
sasa utawala wa sheria upo wapi?

Hapa hata mimi sielewi ni muhimili upi unaowajibika kwa nani. Serikali ilitoa tamko Bungeni la namna ya kutatua tatizo la mgao. Kabla ya utekelezaji, Kamati ya Bunge imeshaingilia na kutoa tamko lake namna ya kutatua tatizo la umeme nchini.

Mahakama imeamuru mitambo isiwashwe bila idhini yake lakini Bunge linaambia serikali mitambo ya Dowans iwashwe. Hapa nani atakayewajibisha mwenzake, ni bunge au ni serikali au ni mahakama?
 
Hapa hata mimi sielewi ni muhimili upi unaowajibika kwa nani. Serikali ilitoa tamko Bungeni la namna ya kutatua tatizo la mgao. Kabla ya utekelezaji, Kamati ya Bunge imeshaingilia na kutoa tamko lake namna ya kutatua tatizo la umeme nchini.

Mahakama imeamuru mitambo isiwashwe bila idhini yake lakini Bunge linaambia serikali mitambo ya Dowans iwashwe. Hapa nani atakayewajibisha mwenzake, ni bunge au ni serikali au ni mahakama?

Tatizo ni kwamba hata wakifanya ufisadi sisi tutakuja kulalamika tu. Si unaona JK na kundi lake wanasinzia kule Paris kwenye mkutano ambao hata Kamishna wa madini angeweza kuwakilisha nchi. Halafu kila siku tunalalamika JK anasafiri sana na yeye anaendelea kusafiri sana!
 
Yaliyofanywa na Kamati ya bunge kufuatilia na kujua matatizo yaliyoko ni sahihi, lakini unyeti wa suala lenye ni makosa kuruhusu utekelezaji huo wakati kuna kesi mahakamani.
Januari Makamba anachotafuta ni umaarufu hapo kwamba amefanikisha kuondoa tatizo la mgao wa umeme hata kwa kuzunguka nyuma ya mkondo wa mahakama.
Njaa ya mfumo wa ccm
 
yaliyofanywa na kamati ya bunge kufuatilia na kujua matatizo yaliyoko ni sahihi, lakini unyeti wa suala lenye ni makosa kuruhusu utekelezaji huo wakati kuna kesi mahakamani.
Januari makamba anachotafuta ni umaarufu hapo kwamba amefanikisha kuondoa tatizo la mgao wa umeme hata kwa kuzunguka nyuma ya mkondo wa mahakama.
Njaa ya mfumo wa ccm

kamati ya january makamba ni kamati kama kamati nyingine, iache kufanya kazi ya udalali, kwani lazima mitambo hii ya dowans iwashwe ndio umeme upatikane, kwanini watu wamekuwa zezeta kiasi hiki? Kwanini tuwapigie magoti watu ambao wametupeleka mahakamani na tunajua ni watanzania wenzetu? Kamati ya madini inatumikia mafisadi
 
Miye nasubiri kusikia "utawala wa Sheria" utaenda vipi.. maana isije kuwa ni "utawala wa sheria" katika kunufaisha mafisadi lakini ikija kwenye masuala ya maslahi kwa taifa.. unatokomea.
 
Hapa pana kitendawili, tega nitegue. Kamati, bunge, mahakama, ikulu ni taasis ipi inaguswa zaidi na inaliweka taifa mbele kabla ya mambo mengine! Yetu macho
 
Hivi ikijakugundulika kwamba ushauri wa Januwari umekiuka sheria na kutia serikali hasara, ni mhimili upi utakaowajibisha mwingine. Serikali itawajibisha bunge?
 
Hivi kwa JK, Pinda, Makamba,et al solution ya umeme ni DOWANS tu!!
 
Hivi jamani ni nani hasa director, producer wa hii tamthilia ya dowans duhh!! Yaani nimefuatilia mpaka basi. Kweli ni kiboko hapa ndio nimeamini ukistaajabu ya musa ya firauni je?
 
Kaaz kwel kwel! Mi huwa nasemaga hivi....and the saga continues!
 
Nadhani J Mnyika ni mjumbe kwenye kamati ya nishati, yeye ana msimamo gani?
 
Kazi ya kamati ya Bunge ni nini? Je kamati ya Bunge inaingilia shughuli ambazo siyo zake? Je ni nani hasa mtekelezaji? Je, Tanesco wameshindwa kufanya kazi yao? Je, Tanesco wana-proposal gani kuhusu huu umburukenge unaoendelea?


Je kila Tom, Dick and Harry amekuwa mtaalam wa mambo ya nishati? Je sheria inasema nini kama raia yeyote yule anataka ku-supply grid ya taifa? Mimi nataka niwe na mitambo yangu binafsi sasa maana naona umeme bongo ni mtaji tangu IPTL ilipoanza naona wenzangu wanachota tu na Bunge linawasaidia.
 
Sasa Pinda hakujua kwamba kuna kesi mahakamani. Kweli viongoze wetu vibonzo kweli kweli. Pinda huyo huyo ndiye aliyezuia mjadala wowote!

Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi yetu, Nchi imekosa uongozi mahiri na imewekwa kwenye auto-pilot.

JK, Pinda, Yule makamu wa Rais bubu (hivi anaitwa nani vile...!?), Makinda!

God help us....2015 is TOO FAR!
 
kha...vituko hivi sasa! kila mmoja anashika mnofu kadri ya uwezo wake. Kamati ya Bunge, Serikali, Mahakama! Sasa hapa ndo tutaona a true test of 'utawala wa sheria' Tanzania. Kunaweza kukawa na mgongano wa sheria kwenye hili? Maana nchi ipo kwenye giza, na serikali inatakiwa kusuluhisha tatizo. Serikali inataka kujikomboa kutoka kwenye meno ya wananchi kama waajiri wake kwa kuwasha mitambo ya Dowans. Sheria inasema nini juu ya hili? Na maamuzi ya Mahakama yanaweza kuwa juu ya sheria zilizopo? Kwa mfano public procurement Act?
 
Nadhani hapa ndio patamu. Kwanza mahakama imezuia namna yoyote ya wengine kujihusisha na huu mjadala wakati a) maombi ya Dowans yapo mahakamani kwa kusajiliwa kama hukumu ya ICC inavyotaka na b) pingamizi ya wanaharakati ipo mahakamani.

Baada ya hapo ndio mengine yafatie.
 
Na Saed Kubenea - Imechapwa 02 March 2011

Siri za mawakili wao zavuja Wahofia TANESCO kushinda


tanesco_231_0.jpg




Taarifa zinasema hoja ya kuwapo rushwa katika mkataba kati ya Dowans na TANESCO zilitosha kuishawishi Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), kutupilia mbali madai ya kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa hukumu ya ICC, hoja ya rushwa ilijitokeza wakati wa kusikiliza shauri hilo. Haikuwa katika hati ya kiapo ya mjibu madai. Katika hali hii mahakama isingefanya rushwa kuwa hoja kuu.

Taarifa zinasema hoja ya rushwa iliingizwa mahakamani humo na mawakili wa TANESCO wakati walipohoji Henry Surtees – mfanyakazi wa Rostam Aziz katika kampuni yake ya Caspian Limited, jambo ambalo mahakama ilisema, "isingeweza kulibeba" na kulitolea uamuzi.

Kwa maelezo haya, ama mawakili wa TANESCO hawakuona, hawakujua, hawakuthamini hoja ya rushwa; au waliipuuza kwa makusudi. TANESCO iliwakilishwa na Rex Attoneys ya Dar es Salaam.
Surtees ndiye ICC ilisema alitumwa na Rostam Aziz nchini Marekani, 7 Oktoba 2006, kusaini mkataba kati ya Richmond na Dowans, huku akiwa na nyaraka zote muhimu za mkataba kati ya TANESCO na kampuni hiyo.

Taarifa zinasema serikali, mbali na kumpatia Surtees mkataba kati ya Richmond na TANESCO, ilimpatia muhtsari wa kikao cha kamati ya majadiliano kati ya TANESCO na serikali na nyaraka nyingine muhimu ili kurahisisha kazi yake, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Usalama wa Taifa (TIS) ya mwaka 1976.

MwanaHALISI lilimhoji wakili wa Mahakama Kuu, Tundu Lissu juu ya uwezekano huo na kushindwa au kupuuzwa kwa hoja kuu ya rushwa.
Katika mahojiano hayo, Lissu anasema hatua ya mawakili wa TANESCO kushindwa kueleza kuwepo rushwa ndani ya kesi ya msingi, ndiko kulikochangia TANESCO kushindwa.
Lissu ambaye pia ni mbunge wa CHADEMA (Singida Mashariki) anasema, "Kuna ushahidi usiopingika kwamba, mawakili wetu waliolipwa zaidi ya dola 2.4 milioni (sawa na Sh. 3.6 bilioni), hawakufanya kazi yao kama inavyotakiwa."

"Hatua ya mfanyakazi wa Rostam, Bw. Henry Surtees kupata nyaraka za serikali bila kibali cha katibu mkuu kiongozi, ni rushwa ya madaraka. Hata mahakama imeelezwa urahisi huu wa mambo ulitokana na Rostam Aziz kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi katika wizara ya nishati na madini," ameeleza Lissu.

Lissu ambaye alishiriki katika kesi ya kampuni ya City Water dhidi ya serikali na kushinda anasema, "Kwa maoni yangu, kazi waliyofanya mawakili wa TANESCO siyo ya kitalaamu. Siamini kuwa hawajui kazi yao. Haya mambo ya rushwa yamejitokeza sana wakati wa kuhoji mashahidi, lakini hayakuwamo katika hati ya utetezi; jambo ambalo limelifanya suala hilo kutopewa uzito wakati wa hukumu."
Anasema kesi ya Dowans dhidi ya TANESCO ilikuwa rahisi kushinda kwa kuwa ilifanyika kwa kutumia sheria za Tanzania.
Anasema, "Ni vigumu kuamini kwamba ushiriki huu wa Rostam Aziz, Edward Lowassa, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha ulikuwa na lengo zuri la kulisaidia taifa kumaliza tatizo sugu la umeme."
Lissu anasema "kuna uwezekano mkubwa kwamba viongozi hawa walitumia tatizo la umeme kama kisingizio cha kuliingiza taifa katika mikataba ya kinyonyaji ambayo imeligharimu fedha nyingi na kuwatajirisha wao na maswahiba wao wa kibiashara."

Ni katika mazingira haya, Lissu anasema, watetezi wa TANESCO wangeshinda kama wangetumia sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ya mwaka 2007.
Sheria hiyo inakataza vitendo vya rushwa katika mikataba na manunuzi ya umma, kujipatia manufaa kwa kutumia nafasi za utumishi wa umma na matumizi mabaya ya madaraka ya umma.
Lissu anasema, "Hata kula njama tu kufanya matendo yaliyokatazwa na sheria hii, ni kosa. Zaidi ya hayo, adhabu ya makosa sio tu ni faini na, au kifungo jela; bali kutaifishwa; na au kufilisiwa kwa mali iliyopatikana kwa njia ya rushwa."

Tarehe 28 Novemba 2006, akiwa nchini Canada, Karamagi aliwasiliana na mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Balozi Fulgence Kazaura akimfahamisha Richmond imehamishia mkataba wake kwa kampuni nyingine na kumtaka kuangalia uhalali wa hatua hiyo chini ya makubaliano kati ya TANESCO na Richmond.
Naye Balozi Kazaula akitekeleza maagizo ya Karamagi, alimwandikia Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Adriaan van Der Melwe wakati huo, akitaka kufanya kazi aliyotumwa na Karamagi. Adriaan van Der Melwe, akitekeleza maagizo ya Balozi Kazaula, alimwandikia katibu wa shirika, Subira Wandiba ili aeleza kama taratibu zimekiukwa au hapana.
Siku hiyohiyo Wandiba alijibu barua ya mkurugenzi wake kwa kusema, "…kufuatana na mkataba wa 23 Juni 2006, Richmond hairuhusiwi kuhamisha mkataba wao kwenda kampuni nyingine yeyote."
Kuhusu hilo, Lissu anasema, "Hawa watatu wa kwanza walikuwa wanashikilia nafasi za uongozi wa kuchaguliwa na wananchi kama ubunge na uwaziri. Kamishna Mrindoko anashikilia nafasi ya kuteuliwa.
"Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, wahusika wote hawa walikuwa ni ‘viongozi wa umma' kwa tafsiri ya kisheria ya maneno hayo. Hivyo ilitosha kujenga hoja mahakamani kuwa hapa kuna rushwa," ameeleza.
Akiongea kwa kujiamini Lissu alisema, "Hatua ya Lowassa kuipa kazi Richmond wakati akijua kwamba haikuwa na sifa, ni rushwa. Hata kuandaa mazingira ili mtu mwingine aweze kulipwa kupitia mgongo wa Dowans, ni rushwa."
Anasema, "Haiwezekani waziri mkuu na waziri wa nishati wavunje taratibu na sheria zilizowekwa na serikali yenyewe, ikiwamo sheria ya manunuzi ya umma, halafu useme hapa hakuna rushwa. Inawezekana mawakili waliogopa kusimamia hoja hii, kwa sababu mwisho wa siku wangewataja akina Lowassa, Karamagi na Msabaha."
Wakati hayo yakiachwa tangu mwanzo wa shauri, mawasiliano yaliyonaswa na gazeti hili kati ya mawakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama na John M. Miles, ambayo yamenakiriwa kwa wakili mwenzao Elizabeth Karanja, wamiliki wa Dowans wamepatwa na kiwewe wakihofia kutopata tuzo ya Sh. 94 bilioni waliyopewa na ICC. Katika mawasiliano hayo, wakili Fungamtama anasema, "Nionavyo, TANESCO wanaweza kupinga hukumu hii kwa kutumia vipengele vya sheria ya usuluhishi ya Tanzania ambavyo vinazungumzia maslahi ya umma na mambo yaliyo kinyume cha sheria."
Mawasiliano hayo ya 9 Desemba 2010, saa 3:47 asubuhi, yamechukuliwa na wachunguzi wa mambo ya sheria kueleza kile walichoita "mawakili wa Dowans kupata kiwewe."

Fungamtama ambaye pia ni wakili wa Rostam Aziz, alikuwa akijibu baruapepe ya Miles ya tarehe 7 Desemba 2010 saa 8:41 usiku. Miles alitaka ufafanuzi kutoka kwa Fungamtama iwapo kuna uwezekano wa sheria za Tanzania kuzuia malipo kwa Dowans.
Ijumaa ya 17 Desemba 2010, saa 2:58 asubuhi, mmoja wa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans, Guy Picard, kutoka Canada, alipeleka baruapepe kwa wahusika wa Dowans katika kesi hiyo, akitaka kujua iwapo ni kweli Mahakama Kuu ya Tanzania imefungwa hadi Februari kama anavyosikia.
Baruapepe hiyo iliandikwa kwa Elizabeth W. Karanja, Stanley Munai, Henry Surtees na mkurugenzi mtendaji wa Dowans ambaye hakutajwa jina (md@dowans.com). Picard pia alituma nakala kwa Miles, Amish Shah na Fungamtama.
Siku hiyohiyo usiku wa manane, Miles alimjibu Picard kwa kukiri kwamba ni kweli Mahakama Kuu itafungwa na hilo litachelewesha tuzo yao kusajiliwa lakini hilo litawaruhusu waende London, kuisajili. Mawasiliano mengine kati ya Fungamtama, Amish Shah, Elizabeth W. Karanja, Stanley Munai, Henry Surtees yalifanyika 21 Januari 2011, saa 2:09 asubuhi na tarehe 23, 24, 27 na 9 Februari 2011. Katika moja ya mawasiliano hayo, Fungamtama anasema, "…niko imara kupambana na wanasheria wa TANESCO katika hoja yoyote watakayoileta kupinga hukumu hii."
 
Back
Top Bottom