Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 261
Nusu saa iliyopita (2/3/2011), katika mahakama kuu ya tz Dsm, jaji Mushi ametoa hukumu kuwa Tanesco/Serikali wasifanye makubaliano au maridhiano yoyote hadi waombe idhini kutoka mahakama yake.
Uamuzi huo unafuatia maombi ya mawakili wanaowakilisha wanaharakati wanaopinga kusajiliwa na kulipwa kwa tuzo ya Dowans.
Hii hukumu inajumuisha nia yoyote ya kuingia makubaliano kuwasha mitambo ya Dowans au makubaliano yoyote yanayohusu kupunguza au kusamehe tuzo ya Dowans
Pia ametoa hukumu kwamba hatakiwi mtu yoyote kuzungumzia au kutoa ufafanuzi hadharani kuhusu Tuzo hiyo ya Dowans. Hukumu hiyo ilikuwa kwa mujibu wa mmoja wa Objectors aliyeisomea mahakama gazeti la Mwananchi la tarehe 25 February 2011 ambalo lilimnukuu Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans (Stanley Munai) aliyekuwa anawafafanulia waandishi wa habari kuhusu jinsi hukumu hiyo ilivyokuwa halali na kwamba Tanesco hawatakiwi kukata rufaa
Kesi itatajwa tena tarehe 30 Machi 2011

KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imependekeza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuingia mkataba mpya na Kampuni ya kufua umeme ya Dowans ikiwa ni hatua za muda mfupi kukabiliana na tatizo la umeme nchini.
Hata hivyo, Mahakama Kuu imeizuia Serikali na Tanesco kuchukua hatua yoyote inayohusiana na mazungumzo au mkataba wa aina yoyote baina yake na Dowans bila ridhaa yake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Januari Makamba alisema: "Kamati imependekeza mambo 30 ikiwamo kuwashwa kwa mitambo ya Dowans haraka na serikali itoe fedha zaidi kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL. Hatua hii imefikiwa kama suluhisho la muda mfupi la kupambana na mgawo.''
Makamba alisema pia kwamba kamati imependekeza kupunguzwa kwa megawati 50 kutoka katika migodi ya madini inayotumia umeme wa megawati 125 ili zipelekwe kwa wananchi.
Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga alisema mapendekezo hayo watayakabidhi katika Ofisi za Bunge na kwamba yatatangzwa na Spika, Anne Makinda
Lakini, wakati kamati ikitoa mapendekezo hayo, jana Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam anayesikiliza maombi ya usajili wa tuzo ya Kampuni ya Dowans iliyoshinda iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara(ICC), dhidi ya Tanesco alitoa agizo kuwa lisifanyike jambo lolote kuhusu Dowans nje ya mahakama.
"Naagiza jambo lolote lisifanyike nje ya mahakama wakati ikiendelea na shauri hili. Kama kutahitajika kuwa na majadiliano yoyote basi pande husika zilete maombi mahakamani ili iweze kusimamisha kwanza mchakato huu kusubiri majadiliano hayo."
Jaji Mushi alisema: "Haitakuwa vyema mahakama kuendelea na mchakato wakati na huko nje majadiliano yakiendelea. Kama pande hizo zikiafikiana, basi zinaweza kuja ‘ku-withdraw' (kuondoa shauri) na kama zitashindwana basi ndipo tutakapoendelea na mchakato."
Source: Gazeti la Mwananchi